Abiria Pekee Aliyenusurika Kwenye Ajali ya Ndege, Aelezea Ilivyokuwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Abiria Pekee Aliyenusurika Kwenye Ajali ya Ndege, Aelezea Ilivyokuwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 2, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mtoto Bahia Bakari abiria pekee aliyenusurika kwenye ajali ya ndege iliyoua abiria 152

  July 02, 2009

  Mtoto aliyenusurika kimiujiza kwenye ajali ya ndege ya Yemen Airways iliyodondoka kwenye bahari ya Hindi karibu na visiwa vya Komoro na kuua watu 152 ameelezea jinsi alivyonusurika kimiujiza kwenye ajali hiyo. Bahia Bakari mwenye umri wa miaka 14 ndiye abiria pekee aliyenusurika kwenye ajali ya ndege ya Yemenia, Airbus A310 iliyotokea alfajiri ya jumanne wiki hii.

  Bahia aling'ang'ania mabaki ya ndege na kuelea juu yake kwa masaa 12 katika hali ya hewa mbaya na bahari ambayo imejaa papa wengi kabla ya waokoaji kufika na kumuopoa.

  Mtoto huyo ambaye hali yake inaendelea vizuri baada ya kupewa matibabu nchini Komoro amerudi kwao Ufaransa kuungana na baba yake.

  Kassim Bakari, baba wa msichana huyo, akiongea na vyombo vya habari vya Ufaransa alisema kuwa nilipoongea naye kwa simu aliniambia "Tuliona ndege ikiangukia kwenye maji, nilijikuta kwenye maji, niliwasikia watu wakiongea lakini sikuweza kumuona hata mtu mmoja. Nilikuwa kwenye kiza sikuona chochote".

  "Baba sikuweza kuogelea vizuri, niling'ang'ania juu ya kitu, sijui ni kitu gani" alisema Bahia akimwambia baba yake.

  Bakari ambaye ana watoto wengine watatu alisema kuwa aliposikia habari za ajali ya ndege hiyo, moja kwa moja alifikiria kuwa hatamwona tena mkewe na mtoto wake wa kwanza.

  "Ni msichana mwenye aibu sana, sikufikiria kama angenusurika namna hii, Siwezi kusema hii ni miujiza bali ni matakwa ya mwenyezimungu" alisema Bakari.

  Bakari alisema kuwa Bahia hadi sasa hajaambiwa kuwa mama yake amefariki.

  "Walimwambia kuwa mama yako yupo chumba cha jirani ili kutomshtua lakini ukweli ni kwamba mama yake amefariki na sijui nani ataweza kumwambia" alisema baba wa mtoto huyo.

  Waokoaji walimuokoa Bahia kwenye bahari ya Hindi kilomita 16 toka kwenye pwani ya Visiwa vya Komoro.

  Waokoaji hao walisema kuwa Bahia alikuwa dhaifu sana wakati anaokolewa, hakuweza hata kulishika boya alilorushiwa na hivyo kumfanya mzamiaji kupiga mbizi na kumpandisha kwenye boti ambako alifunikwa na blanket na kupewa maji ya moto yenye sukari anywe wakati anawahishwa hospitali.

  Watu wengi wamestaajabu jinsi mtoto huyo alivyonusurika ajali hiyo na kuelea kwa jumla ya masaa 12 kwenye bahari ambayo imejaa papa wengi tena akiwa hana hata life jacket.


  Source: nifahamishe.com
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  maajabu ya mungu hayo
   
 3. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kweli ni maajabu, pengine Mungu bado anampango naye!
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,315
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  atakalo Mungu linawezekana......nasi tuamini tu ....hakika yeye atafanya...huyu mtoto akamsifu na kumshhukuru sana Mungu......hakika anaweza
   
 5. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,741
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Mungu ana miujiza mingi ya ajabu. Huu ni muujiza wa ajabu. Mungu amekuwa mwaminifu katika maisha yake.
   
 6. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  More than 12 hours,ina maana watu wa usalama wa anga hawakuwa na taarifa ya ndege kupotea au kuanguka?
   
 7. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  this is just a miracle
   
 8. J

  Janjaman Member

  #8
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 21, 2009
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni muujiza tu wa mungu.
   
 9. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ni vizuri kuwa binadamu tunatambua kuwa yote hupangwa kwa uwezo wa mwenyezi Mungu.
   
 10. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  mungu anaweza yote utukufu na ukuu niwake jina lake lihimidiwe amen
   
 11. F

  Froida JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Huwezi kuamini lakini ndivyo ilivyokuwa Mungu ni wa ajabu na anamakusudi yake, Bahia Bakari Mungu akusaidie ukuwe vyema na upone salama
   
 12. L

  Lusajo Kyejo Member

  #12
  Jul 6, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 33
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Acheni Mungu aitwe Mungu
   
Loading...