Abiria kutokuchimba dawa holela wakiwa safarini...

Abiria kutokuchimba dawa holela wakiwa safarini...

Magita

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2013
Posts
319
Reaction score
144
Wanahabari wenzangu leo nimeshuhudia mwenyewe katika bus la Tayassar T.273 BVA kutoka Tanga kuja Dar, kuna abiria mmoja aliomba msaada ili bus lisimame tukiwa pale Mbwewe ili akachimbe dawa, majibu yaliyotolewa na wahudumu wa bus hilo walimwambia kuchimba dawa hadi Mizani-Wami juu, sawa yule kaka alivumilia hadi Mizani-Wami juu, tulipofika pale Mizani vile vyoo vya kuchimba dawa huduma yake kumbe imesimama kwa muda wa wiki 1 ili kupisha marekebisho ya jengo.

Baada ya kuona kuwa ile huduma haipo, kondakta akatutangazia kuwa kuchimba dawa mpaka Vigwaza Petrol Station hii ni kulingana na sheria ya sasa ya kuchimba dawa kiholela! Yule kaka akavumilia hadi Chalinze, lakini tulipofika katika Kijiji cha Mbala akashindwa kuvumilia ndio akatishia kujisaidia ndani ya gari! Baada ya pale nikamuomba dereva asimamishe gari kwa ajili ya dharula hii!

Sasa wana JF swala hili mnalionaje maana bus litalokutwa linachimba dawa holela faini yake 50,000? na kulingana na vituo vya kuchimbia dawa muda mwingine viko mbali.
 
Anaweza kuwafungulia hao wamiliki wa hilo basi kesi ya madai kwa udhalilishaji.
 
Anaweza kuwafungulia hao wamiliki wa hilo basi kesi ya madai kwa udhalilishaji.

Walimwambia kuchimba dawa holela faini yake bus litashikwa faini ya 50,000 punde inapobainika
 
Sasa kama umebanwa na tumbo la uharo inakuwaje hapo?Hii ni balaa.....
 
lakini sina uhakika huyo mshikaji angeweza kukojoa hata kwenye kichupa baada ya kuona hawamuelewi.mimi nikisafiri sitakagi hata kunywa vimiminika ovyo kuepuka adha kama hii.:wave:
 
Sasa kama umebanwa na tumbo la uharo inakuwaje hapo?Hii ni balaa.....

Hao ndiyo viongozi wetu tulio nao. Kwa kuwa wao wanasafiri na AC on saa zote, hawa hawana haja ya kujiuliza nnani alianzisha mpango huu wa kuchimba dawa sehemu sehemu.
Hivi, fikiri, kama kweli umeshikwa na tumbo hilo, utafanyaje? Sheria hizi za kibabe zikomeshwe jamani. Hatusemi kwamba tuharibu tu mazingira, tena ilikuwa inawadhalilisha mama zetu sana kwani wapo wapuuzi waliokuwa wanapiga cha--bo sehemu kama hizo. Serekali sikivu, ingeweza kwanza kuweka mazingira safi hapo na kuwaajiri hata vijana wakayaweka safi na tukalipa hata kitu kidogo kusaidia usafi. Unapiga marufuku kuchimba dawa wakati hujapiga marufuku tumbo la ghafla la kuhara! What a pity to this government. Siamini kama waziri analijua hili. Huenda ni kichaa fulani tu katamka hili.
 
Msiwe mnakulakula ovyo muwapo safarini ili kupunguza kunyakunya hovyo
 
Watutafutie msamiati mwingine maana 'kuchimba dawa' ndo haifanyi kazi tena!
 
lakini sina uhakika huyo mshikaji angeweza kukojoa hata kwenye kichupa baada ya kuona hawamuelewi.mimi nikisafiri sitakagi hata kunywa vimiminika ovyo kuepuka adha kama hii.:wave:

Mleta mada hajatwambia kama huyo jamaa alitaka kukojoa au 'kukata gogo' sipati picha, maana km ni hiyo ya pili kichupa hakina nafasi labda ukirengeshe kwa mbele then uko kwingine utafute means nyingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom