Abdul Nondo amewapiga "KO" maofisa Uhamiaji

Abdul Nondo amewapiga "KO" maofisa Uhamiaji

Nondo bhana kumbe kana damu ya siasa ubabani na umamani!!.......Yaani hata DNA ikikataa bado kanabakia na uanasiasa wake?!!......Sasa wewe Nondo kwanini ulijiteka?

Kujiteka inahusiana vipi na uraia wake? Hauoni hata hiyo kujiteka anabambikiziwa?
 
Hao uhamiaji wengi ni wakimbizi mule sema basi....nyan haoni.....k...n. ...d. U....lake bichwa.
Ukiwachambua watabaki 3 tu ambao ndio raia wadanganyika...
Wale wote ni Askari sio raia wa tz.
 
Ngoma imerudi nyumbani wenye kujua siasa za zengwe wamechukua game.Sijui km hivi front wataziweza.Mbaya huwa wanaachia game njiani bila kulipa hasara.
 
Wiki kadhaa zilizopita niliandika ya kwamba sakata la Abdul Nondo litawavua nguo serikali na jeshi la polisi na hakika inaenda kutimia. Leo mwandishi mzoefu Luqman Maloto ameandika machache kuhusu sakata hilo.

Idara ya Uhamiaji ilimtaka Abdul Nondo athibitishe uraia wake kwa kuwasilisha cheti chake cha kuzaliwa, vyeti vya wazazi wake, babu zake na bibi zake. Lilikuwa agizo la hovyo mno.
Hata hivyo, historia ipo na inaishi. Mpaka sasa maofisa hao wameshachapwa KO (Knock Out) na Abdul.

UNONDO WA ABDUL UBABANI

Unondo wa Abdul upande wa baba yake unaelezwa vizuri na Sheikh Khamis Hababi wa Kigoma Ujiji. Sheikh huyu anaijua vizuri familia ya Abdul Nondo.

Sheikh Hababi anasema: "Huyu Kijana (Abdul Nondo) ni Mjukuu Wa mzee Omar Athuman Kagobe. Mzee Kagobe ni mwanajeshi wa zamani (veteran) aliyepigana vita kuu ya pili ya dunia, na ndiye aliyeileta TANU Kigoma. Wakati wa kudai uhuru Nyerere alipofika Kigoma amewahi kufikia kwa mzee Kagobe mara mbili akiwa na Bibi Titi na Sheikh Suleiman Taqadir. Nyerere alikula, kunywa na kusaidiwa nauli na familia ya kina Abdul Nondo.
"Nyumbani kwa Sheikh Kagobe ndipo alipofikia pia Sheikh Abdallah Saleh Al Farsy mara mbili na Sheikh Hassan bin Amir.

"Bibi yake mdogo Nondo ndiye Mama yake Sherry Taki, aliyekuwa mjumbe wa Kamati kuu ya CCM, na mama huyu ndiye aliyemuuliza Nyerere kama atawanyang'anya Wahindi, waarabu na Wazungu majumba na Mashamba, baada ya Uhuru. Nyerere akasema hapana, Utawala wa TANU hautofanya hivyo (ingawa alifanya hivyo baada ya uhuru)."

TAFAKURI

Kwahiyo Uhamiaji wanaposema Nondo si raia wanamaanisha Babu yake (mzee Kagobe) si raia. Mtu aliyepigana vita kuu ya dunia hakua raia? Mtu aliyeintroduce TANU Kigoma (ambayo ndio CCM leo) hakuwa raia. Mtu aliyemlisha na kumlaza Nyerere mara mbili nyumbani kwake hakua raia? Kwamba Nyerere alikuwa akipewa msaada na mtu asiye raia.

Bibi yake mdogo Abdul, mama Sherry Taki nae hakuwa raia, licha ya kuwa mjumbe wa kamati kuu ya CCM? Yani CCM iliruhusu mtu asiye raia kuwa mjumbe wa kamati kuu?
Ni wazi alama ya uraia wa kijana huyu haiwezi kufutika kamwe katika historia. Familia ya kijana huyu imechangia uhuru wa nchi hii, imechangia kuzaliwa kwa taifa hili, imechangia kuzaliwa kwa TANU na hatimaye CCM.

UNONDO WA ABDUL UMAMANI

Unondo wa Abdul upande wa mama yake unaelezwa kinagaubaga na Maalim Razaq Seleman.
Anasema: "Huyu kijana (Nondo) mama yake ni wa ukoo Mzee Haruna Taratibu aliyesisi TANU Dodoma. Mzee Taratibu alisaidia kuanzishwa kwa TANU kipindi ambacho watu wengi hasa wafanyakazi walikua wanaogopa kujihusisha na siasa. Kati ya mwaka 1954 hadi 1958 kilikua kipindi kigumu mno katika harakati za kudai uhuru.
"Mwalimu Nyerere mwenyewe aliwahi kusema 'Hicho kilikuwa kipindi kigumu sana katika historia ya Chama chetu na ni watu wachache sana walikuwa na ujasiri wa kujiunga na chama na kukifanyia kazi.'

"Mmojawapo wa watu waliokua na ujasiri huo ni mzee Taratibu (babu yake mdogo Nondo upande wa mama). Mwaka 1953, Haruna Taratibu, alikuwa na umri wa miaka 23 tu, akifanya kazi Public Works Department (PWD) Dodoma kama fundi mwashi (mason). Pamoja na umri wake mdogo alijaribu kuunda chama cha wafanyakazi kwa kuwahamasisha na kuwakusanya vibarua walioajiriwa katika kazi za ujenzi (wengi wakitokea Kigoma).

"Kwa sababu ya harakati hizo za kutaka kuanzisha chama cha wafanyakazi, Taratibu alionekana na wakoloni kama mtu mkorofi na mzusha vurugu. Hata hivyo Taratibu hakufanikiwa kuanzisha chama hicho na matokeo yake akapewa uhamisho kwenda Singida kama adhabu.
"Mwandishi Nguli wa Historia, Mohamed Said katika kitabu ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)...: (Phoenix Publishers, Nairobi, 2002) ukurasa wa 216, anaeleza kuwa mzee Taratibu alivutiwa sana na harakati za MAUMAU nchini Kenya na alizoea kufuatilia matukio yake katika gazeti lake alilokuwa akilipenda sana, ''Baraza', gazeti la Kiswahili la kila wiki kutoka Kenya.

"Ilikuwa katika Novemba 1954 wakati Taratibu alipokuwa akipekuapekua gazeti hilo ndipo alioposoma habari kuhusu TANU. Taratibu aliuliza pale Singida mjini kama kuna tawi la TANU. Taratibu alifahamishwa kuwepo kwa tawi la TANU pale mjini na katibu wake alikuwa mzee mmoja kwa jina la Mzee Kinyozi.

"Taratibu alikata kadi yake toka kwa huyo mzee na akawa mwanachama wa TANU. Asubuhi iliyofuata Taratibu aliingia ofisini kwake na akaiweka kadi yake ya uanachama wa TANU yenye rangi nyeusi na kijani juu ya meza yake, kila mtu aione. Ofisa Mzungu wa PWD Singida hakuweza kuvumila ufedhuli kama ule, alishauri Taratibu apewe uhamisho kurudi Dodoma alikotoka, kabla hajaeneza sumu yake kwa Waafrika wengine.

"Kwa kifupi mzee Taratibu alijitoa kwa hali na mali kuianzisha TANU bila hofu ya kushughulikiwa na serikali ya kikoloni, licha ya kwamba alikuwa mfanyakazi. Hatimaye alichaguliwa kuwa mjumbe wa sejretarieti na kamati ya siri ya TANU (kwa pendekezo la Oscar Kambona), na baadae alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa TANU kanda ya kati, Rais akiwa Alexander Kanyamara, Katibu Abdu Mohamed Mwamba, Mweka Hazina Omari Suleiman, huku Binti Maftah Karenga, Bakari Yenga, Maalim Khalfan, Idd Waziri na Said Suleiman wakichaguliwa wajumbe."

TAFAKURI

Leo mjukuu wa mzee huyu aliyepigania uhuru anaambiwa si raia.
Mimi kama kawaida yangu nacheka. Ona nacheka tena. Yaani nacheka mno. Nacheka zaidi dogo anavyowagonga KO watu wakubwa wasiotumia 'hikma' na weledi kwenye kazi zao. Eti vyeti vya kuzaliwa vya babu na bibi zako wa upande wa mama na baba. Nina siku nyingi sijasonya!!!!!

MAELEZO YA PICHA

Kutoka kushoto ni Idd Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramiya, Mwalimu Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu wakiwa stesheni ya reli Dodoma mwaka 1955.
Ndimi Luqman MALOTO
 
Huyo mwigulu mwenyewe hana cheti cha mama yake atoe ujinga huko,,, serikali ya magufuli ni ya ajabu sijapata kuona
 
Kama hakuna ushahidi wa kuonyesha kwamba Nondo aliwahi kuomba uraia wa nchi nyingine basi hawana kesi.

Inawezekana kabisa Babu na mjukuu wakawa na uraia tofauti.

Ila inawezekana mimi uelewa wangu ni mdogo, Je kuwa raia wa nchi fulani ni lazima babu na bibi yako wawe raia wa nchi hiyo??? mfano nikizaliwa tu na baba mtanzania je sipaswi kuwa mtanzania????

Tu-assume tu kuwa hata kama mababu wa Nondo hawakuwa watanzania je inahusiana nn na Nondo mwenyewe???
 
Du, mpaka naona aibu utafikri ni mimi ndie nasemwa
 
Hivi wakati huo hao wazazi wake na wazazi wa wazazi wake vyeti vya kuzaliwa vilikuwa vikitolewa?
 
Kama hakuna ushahidi wa kuonyesha kwamba Nondo aliwahi kuomba uraia wa nchi nyingine basi hawana kesi.

Inawezekana kabisa Babu na mjukuu wakawa na uraia tofauti.
sasa hayo ya vyeti vya kuzaliwa vya babu na bibi yamekujaje tena??? au ndio ulimbukeni+ushamba+udikteta uchwara
 
Habari wadau,
nawatakia weekend njema

Nani amesahau kilichomkuta mzee Salim Ahmed Salim (PhD). Mzee wa watu baada ya kuitumikia OAU kwa weledi mkubwa sana, akataka aje alitumikie taifa lake, kilichofuata ITV sasa! si wakasema ni mwarabu, heee

Hatujasahau ya dogo Bashe. wakati wakivutana kule Nzega nani agombee ubunge. Ghafla dogo akawa siyo raia - HK akaingia mjengoni. Mwisho wa siku, Nzega inagawanywa, kipande Base, Kipande HK

Kwa mzee Jenerali. sasa sijui tatizo ilikuwa jina au nini. By the way, mwanzoni nilikuwa najua ni jenerali wa jeshi. Mara paaap, siyo mtanzania, Duh

Sheikh Ponda Issa Ponda, baada ya kuwaponda sana chama doa, uraia wake ukahojiwa.

anyways, kumbukumbu inaweza kuwa ndefu sana

ninachojiuliza, ni jinsi gani unaweza kuwa raia wa nchi ambayo haikuwepo? yaani kwamfano, baba yako na bibi yako walizaliwa kabla ya kuja Mjerumani. na pia kabla ya uhuru. Maana tunajua TZ ni ya juzi tu hapo

Naombeni serengeti ndogo bariiidi sana
weekend njema tena
 
FB_IMG_1523023941584.jpg
KUHUSU URAIA WA ABDUL NONDO - PART 2

Jana Sheikh Khamis Hababi wa Kigoma Ujiji alieleza historia ya familia ya kijana Abdul Nondo inayotoa ushahidi kuwa ni watanzania. Historia hiyo ilianzia tangu wakati wa vita kuu vya pili vya dunia, uasisi wa TANU na hatimaye kamati kuu ya CCM ambapo familia ya Nondo ilishiriki kote huko.

Leo Maalim Razaq Selemani anaelezea upande wa pili wa historia ya Abdul kwa ukoo wa mama yake.

Anasema;
"Huyu kijana (Nondo) mama yake ni wa ukoo Mzee Haruna Taratibu aliyesisi TANU Dodoma. Mzee Taratibu alisaidia kuanzishwa kwa TANU kipindi ambacho watu wengi hasa wafanyakazi walikua wanaogopa kujihusisha na siasa. Kati ya mwaka 1954 hadi 1958 kilikua kipindi kigumu mno katika harakati za kudai uhuru.

Mwalimu Nyerere mwenyewe aliwahi kusema ''Hicho kilikuwa kipindi kigumu sana katika historia ya Chama chetu na ni watu wachache sana walikuwa na ujasiri wa kujiunga na chama na kukifanyia kazi.''

Mmoja wapo ya watu waliokua na ujasiri huo ni mzee Taratibu (babu yake mdogo Nondo upande wa mama). Mwaka 1953, Haruna Taratibu, alikuwa na umri wa miaka 23 tu, akifanya kazi Public Works Department (PWD) Dodoma kama fundi mwashi (mason). Pamoja na umri wake mdogo alijaribu kuunda chama cha wafanyakazi kwa kuwahamasisha na kuwakusanya vibarua walioajiriwa katika kazi za ujenzi (wengi wakitokea Kigoma).

Kwa sababu ya harakati hizo za kutaka kuanzisha chama cha wafanyakazi, Taratibu alionekana na wakoloni kama mtu mkorofi na mzusha vurugu. Hata hivyo Taratibu hakufanikiwa kuanzisha chama hicho na matokeo yake akapewa uhamisho kwenda Singida kama adhabu.

Mwandishi Nguli wa Historia, Mohamed Said katika kitabu ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)...'' (Phoenix Publishers, Nairobi, 2002) ukurasa wa 216, anaeleza kuwa mzee Taratibu alivutiwa sana na harakati za MAUMAU nchini Kenya na alizoea kufuatilia matukio yake katika gazeti lake alilokuwa akilipenda sana, ''Baraza,'' gazeti la Kiswahili la kila wiki kutoka Kenya.

Ilikuwa katika Novemba 1954 wakati Taratibu alipokuwa akipekuapekua gazeti hilo ndipo alioposoma habari kuhusu TANU. Taratibu aliuliza pale Singida mjini kama kuna tawi la TANU. Taratibu alifahamishwa kuwepo kwa tawi la TANU pale mjini na katibu wake alikuwa mzee mmoja kwa jina la Mzee Kinyozi.

Taratibu alikata kadi yake toka kwa huyo mzee na akawa mwanachama wa TANU. Asubuhi iliyofuata Taratibu aliingia ofisini kwake na akaiweka kadi yake ya uanachama wa TANU yenye rangi nyeusi na kijani juu ya meza yake, kila mtu aione. Ofisa Mzungu wa PWD Singida hakuweza kuvumila ufedhuli kama ule, alishauri Taratibu apewe uhamisho kurudi Dodoma alikotoka, kabla hajaeneza sumu yake kwa Waafrika wengine.''

Kwa kifupi mzee Taratibu alijitoa kwa hali na mali kuianzisha TANU bila hofu ya kushughulikiwa na serikali ya kikoloni, licha ya kwamba alikuwa mfanyakazi. Hatimaye alichaguliwa kuwa mjumbe wa sejretarieti na kamati ya siri ya TANU (kwa pendekezo la Oscar Kambona), na baadae alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa TANU kanda ya kati, Rais akiwa Alexander Kanyamara, Katibu Abdu Mohamed Mwamba, Mweka Hazina Omari Suleiman, huku Binti Maftah Karenga, Bakari Yenga, Maalim Khalfan, Idd Waziri na Said Suleiman wakichaguliwa wajumbe.

Pichani kutoka kushoto ni Idd Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramiya, Mwalimu Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu wakiwa stesheni ya reli Dodoma mwaka 1955. Leo mjukuu wa mzee huyu aliyepigania uhuru anaambiwa si raia kwa sababu tu amekuwa kinyume na watawala.

Jana Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma mjini alisema kuna mtu amewatuma Uhamiaji kumdhalilisha Nondo. Lakini ukweli ni kwamba mtu huyo hana uhalali wa uraia kuliko Nondo. Hana.!

Malisa GJ
 
Back
Top Bottom