Abakwa, anyongwa, azikwa shimoni

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
[h=3][/h] [h=2]Mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Hogolo, wa umri wa miaka 14 (jina limehifadhiwa) ambaye ni Mkazi wa Mtaa wa Ikulu Kijiji cha Hogolo wilayani Kongwa ameuawa kwa kunyongwa na kuzikwa kwenye shimo nyuma ya nyumba yao karibu na choo baada ya kubakwa.[/h]

Uchunguzi wa aali unaonesha kuwa chanzo cha mauaji hayo yaliyofanyika Jumamosi iliyopita ni wivu wa kimapenzi kwani marehemu enzi za uhai wake, anadaiwa alikuwa amevunja uhusiano na mpenzi wake wa muda mrefu, Heri Aboubakar na kuanzisha uhusiano mpya na Wilfredy Muhaha maarufu Kabo.

Hata hivyo bado haijafahamika muuaji halisi wa marehemu huyo licha ya polisi kuwashikilia watu kadhaa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo akiwemo mpenzi wake wa sasa, Muhaha.

Mbali na Muhaha wengine wanaoshikiliwa Polisi ni Ashad Jafari ambaye ni mkulima na mkazi wa Mtaa wa Nyerere Hogolo ambaye ni rafiki wa marehemu na Rino Mazoea, mkulima na mkazi wa Ikulu Hogolo wilayani Kongwa ambaye ni kaka wa marehemu.

CHANZO: GUMZO LA JIJI
 
miaka 14 ana mpenzi tayari hadi kiasi cha kuachana na kuanza uhusiano mwengine?!!! Mungu amrehemu. RIP. Ameen
 
hii ni hatari sana kwa maendeleo ya taifa letu kama watoto wa miaka chini ya kumi na nane wanajihusisha katika ngono badala ya masomo! hivi Tanzania na nchi nyingine changa hizi habari za aibu zitaisha lini kwenye vyombo vyetu vya habari? Maisha bora kwa kila mtanzania yatatoka wapi kama nguvu kazi ya taifa inaangamia kwa umalaya na kukosa nyenzo muhimu ya elimu katika maendeleo?
 
zamani mtoto wa kike akivunja ungo tu anaozeshwa...nyie mnashanga kigoli huyo mkubwa kabisa
 
Mungu utuhurumie,Mungu utokoe, tazama watoto wako wanaangamia kwa tamaa ya wazinzi na kama haitoshi wanaona wawahukumu kwa kuwaua. lakini mpaka lini? uwaadhibu waarifu kwa kadri ya makosa yao na wale wakosaji wanaoendelea kutembea na watoto wa watu na hasa wenye umri mdogo uwasaidie waache dhambi hii na uyabadili maisha yao wawe walezi wema tunawategemea katika taifa letu hili tunalozurumiwa na ubinafsi wa watu wa chache kila kukicha.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa na uwahurumie watu wako kwa kadri ya fadhila zako.
 
Back
Top Bottom