A very touching PM (ina mguso wa ajabu mno)

Mkuu mshana kuna ndugu zangu wanashida ya macho ( mtoto wa kwanza wa kiume na wa kwanza wa kike) inawezekana kabisa ni jaribu kutoka kwa mizimu maana uncle wangu huyo amekataa kabisa kutambika.
Ni jaribu kubwa Lakini pia msimamo wake ni mzuri kwakuwa hataki kujiingiza kwenye vifungo na maagano
 
Kiukweli furaha yote ya familia imeisha kabisa!
Ni swala la muda muda tu wakati si milele na hakuna jaribu lisilo na mwisho.... Kumbuka aliyopitia Ayubu Lakini alisimama na Mungu wake mpaka mwisho
 
Hii shida mizizi yake imesambaa sana. Mungu mwema mno
Atatupa msaada kwa kweli.
 
Mungu ndio kila kitu
Namnukuu tena.... Msinyoe denge pembe za vichwani wala msiharibu pembe za ndevu zenu ,msichanje chale YOYOTE katika NYAMA ya miili yenu kwa ajili ya WAFU wala MSIANDIKE alama miilini mwenu.... Mimi ndimi Bwana (Mambo ya Walawi 19: 27-28)
Hivi kiduku na denge kuna utofauti?
 
Mshana, unaposema kwamba ulichoandika hakina uhusiano na mambo yanayoendelea hapa nchini nakataa. Sio kwamba nimeelewa kwamba ulichoandika kinahusu mambo yanayotokea. Lakini naelewa kwamba hakuna jampo linalotokea 'kwa bahati mbaya' Lazima lina chanzo cha 'kiroho' iwe ya shetani au ya ki- Mungu. Kwa hiyo mambo mengi mabaya yanayotokea hapa nchini ni matokeo ya uovu wa kishetani lakini Mungu anayaachia yatokee ili tutambue kwamba kuna watu kati yetu wametenda uovu ili tuombe. Tatizo ni kwamba sasa hivi ni watu wachache sana wanaoomba inavyopasa.

Miaka ya nyuma zilitokea ajali mbaya kwa mfululizo. Watu wakaomba kwa bidii. Ajali zikapungua sana. Nadhani waombaji wali-relax. Sasa zmeanza tena. Lakini ni lazima tukubali kwamba kuna watu wanatumia mashetani kumwaga damu za wenzao kwenye ajali kama kafara: kupata vyeo au kupata mali.

Na hayo uliyoandika kuhusu watu kuwa watumwa wa matambiko, mazindiko na kutafuta uganga ni mambo yaliyoenea sana. Mtu anapata tatizo, anajua kwamba kweli limetokana na ushirikina (uchawi) lakini anadhani suluhisho ni kwenda kuaguliwa kwa mganga. Kama Biblia inavyosema 'tunaangamia kwa kukosa maarifa' Mganga 'anamilikiwa' na majini (mashetani) kwa hiyo kamwe hataondoa majini yaliyowekwa na mchawi ambaye naye ni mfuasi wa shetani. Anachofanya ni kuwapa majini yanayomtesa mtu 'sadaka' ya damu kusudi yatulie yasimtese tena. Lakini baada ya muda yanarudi kumtesa japo ni kwa staili ingine (safari hii yanaweza kumkosesha kipato wakati tatizo la kwanza lilikuwa ni kuumwa n.k.)

Njia pekee ya uhakika ya kuondoa majini na magonjwa na mateso mengine yote ya kichawi, kimizimu, kiganga n.k. ni kuombewa kwa Jina la Yesu basi.
 
umeandika vizuri ila sio kuombewa ndio njia pekee ila njia pekee ni kukubali kumpokea yule muombezi wetu yaan Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wetu yeye atatufundisha hata kujiombea wenyewe unaweza kuombewa lkn mwisho wa siku ukajikuta yanakurudia sababu yule mwembezi hayuko ndani mwetu hatujakubali awepo nimeongezea tu barikiwa.
 
Jamani hadi kwa Mungu?kwa iyo ukijikuta huna hicho kipawa ndo hutotoa zaka milele?
Kuna kule kutoa kwa kawaida, yani mpaka uhubiriwe sana halafu kuna kutoa kwa mazoea kwamba ukienda utatoa halafu kuna kutoa kwa kuguswa leo neno limekolea utatoa kingi na kinyume chake... Halafu kuna kutoa kwa karama ama kipawa, yani haangalii majira kipato wala mazingira
 
Tafakari nzuri.Mungu atusaidie yani kwenye swala la zaka kiukweli wengi tunamwibia Mungu(hatutoi?)Nifanyeje ili niwe mwepesi kuitoa manake mtu ukipata hela unaipigia mahesabu ya kudunia tu zako hauiesabu.
Tune ur mind kuwa 10% sio yako. Unadaiwa, ukiwaza hivi huwezi sahau......

Binafsi najifunza pia, mshana jr

MUNGU akubariki sana
 
Mkuu mshana kuna ndugu zangu wanashida ya macho ( mtoto wa kwanza wa kiume na wa kwanza wa kike) inawezekana kabisa ni jaribu kutoka kwa mizimu maana uncle wangu huyo amekataa kabisa kutambika.
Dah aiseeeee.

ukijinyenyekeza kwa MUNGU ukampa usukani , atakupigania. Biblia yasema vita yake bwana ni atashinda???
 
Back
Top Bottom