ili kuwa huru inabidi kutubu na kumrudia Mungu pamoja na kutoa sadaka ya fungu la kumi (10% ya unachopata) ili kubatilisha sadaka uliyoitoa kwenye madhabahu ya shetani
nb:
sadaka ya fungu la kumi ni endelevu; (kwa watu wote) jenga tabia ya kutoa sadaka ya fungu la kumi kanisani (10% ya unachopata) na Mwenyezi Mungu atakufungulia milango ya Baraka katika maisha yako. Binafsi nimefanikiwa sana kwa kufuata utaratibu huu Bwana Yesu ni mwaminifu na hutimiza neno lake kikamilifu
Malaki 3: 7-12
7 Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?
8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.
12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.
Nawasilisha