FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 716
Sijarudia upotoshaji.
Nimesema
Elewa tofauti ya Net worth na GDP.Hii ni point muhimu sana.
Huyu Slim hela zake zote ndiyo hizo bilioni hamsini na kitu, hizo ni hela / mali zake zote.
Tanzania GDP yetu (uzalishaji wa nchi kwa mwaka mmoja tu) ndiyo takribani nusu yake.
Sasa kusema Slim ni tajiri mara mbili ya Tanzania ni sawasawa tuchukue mali zako zote, tuseme dola milioni moja, halafu tuzilinganishe na mshahara wangu wa mwaka mmoja, dola laki tano, halafu tukasema wewe ni tajiri mara mbili yangu. Wakati wewe umetumia miaka 60 kupata dola milioni moja na mimi nimepata dola laki tano katika mwaka mmoja tu.
Lakini kwa kuelewa kwamba Slim ni mtu mmoja, nikaona kurekebisha facts huku kusichukuliwe kama niko complacent na umasikini wetu.
Kwa sababu hata kama habari ingekuwa kwamba kuna Mmexico huko ana mihela na mali alizo accumulate maisha yake yote ambazo zina net worth iliyo twice our GDP, bado ni habari mbaya.
Kwa hiyo hamna contradiction wala upotoshaji hapo.
Si kweli kwamba Slim ni twice as rich as Tanzania kama nilivyofafanua katika hiyo posti ndefu hapo juu.
Lakini ukweli huu usitufumbe macho tukaona sawa mtu mmoja kuwa na net worth iliyo twice our GDP. Ukitaka kuudharau ukweli huu just because perspective inayoongelewa haijacompare GDP kwa GDP au net worth kwa net worth, wewe ndiye utakuwa unapotosha.
Umenena kweli kabisa kaka, ila naomba kuuliza swali ingawa naandika kwenye giza UMEME hamna hapa natumia simu ya mkononi.
Je ARDHI ya Tanzania ina thamani gani?
Maziwa ya maji (lakes) Mlima Kilimanjaro na fukwe za bahari zina thamani gani?
Kitu kinakua na thamani kama kinaweza kuzalisha au kuleta faida, kama hakiwezi basi hakina THAMANI.
Yap, Networthy na GDP ni sawa na kulinganisha pilipili na machungwa, hapo tupo pamoja.