A day in the Buddhist college

punguzo

Member
Jul 9, 2011
51
0
Kaka, Kama meditation inasaidia kuona mambo yajayo, ni kivipi wakufunzi/ ma-master wenu hawakuweza kugundua maovu yenu, kama kutoroka, au kushiriki katika ibada za ajabu za dini nyingine? Kuwahisi wageni wabaya? Kumiliki siraha? Au kwanini hawakuweza kuzuia mambo mabaya yasitokee hasa kwa wanafunzi wao?
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
140,697
2,000

Meditation ni jambo binafsi zaidi na sio ishu za kutenda miujiza na bado akili ya mwanadamu ni very sophisticated Kwamba unapodevelop meditation powers una uwezo wa kujikinga na mashambulizi yoyote ya kihisia kiroho na kufikirika
Kama umenisoma vizuri haya yaliyotokea yote haya kama mtu huna practice maalum hufiki popote
La mwisho ni Kwamba hebu tafuta post ya ZIMEBAKI STORY utapata majibu vizuri
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
140,697
2,000
Tulimaliza miaka miwili ya kwanza na kurudi Tanzania mwaka ambapo nilikuja kugundua kuwa tayari nimeshadata na mambo ya Buddhism na meditation hivyo kipindi cha kusubiri majibu niliondoka tena kwenda Kenya kupitia Mombasa kwenda kujifunza Krishna consciousness! Hiki ni kitu kipya kabisa. Nilikaa temple ya Mombasa kwa wiki moja tu na baadae kuhamia Nairobi Mathare Rd Hare Krishna temple
Tofauti na kwenye Buddhism tulikokuwa tunachant Buddha's name -Amitofo/Amitoh'una huku tulichant hivi

Hare Krishna hare Krishna
Krishna Krishna hare hare
Hare Rama hare Rama,
Rama Rama hare hare

Hii ilikuwa ni kama salamu na muongozo ambapo kwenye salamu ilikuwa tu ni hare Krishna kama amitofo kwnye Buddhism au Bwana asifiwe kwenye ukristo na salamu alyekum kwenye Uislam nk
 
yang

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
618
500
Mkuu umenichekesha sana hasa hapo Kwa maiti 😂
Hivi ni nini Maana ya dot nyekundu katika paji Lao la uso Hawa Buddhist
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
140,697
2,000
Tulimaliza miaka miwili ya kwanza na kurudi Tanzania mwaka ambapo nilikuja kugundua kuwa tayari nimeshadata na mambo ya Buddhism na meditation hivyo kipindi cha kusubiri majibu niliondoka tena kwenda Kenya kupitia Mombasa kwenda kujifunza Krishna consciousness! Hiki ni kitu kipya kabisa. Nilikaa temple ya Mombasa kwa wiki moja tu na baadae kuhamia Nairobi Mathare Rd Hare Krishna temple
Tofauti na kwenye Buddhism tulikokuwa tunachant Buddha's name -Amitofo/Amitoh'una huku tulichant hivi

Hare Krishna hare Krishna
Krishna Krishna hare hare
Hare Rama hare Rama,
Rama Rama hare hare

Hii ilikuwa ni kama salamu na muongozo ambapo kwenye salamu ilikuwa tu ni hare Krishna kama amitofo kwnye Buddhism au Bwana asifiwe kwenye ukristo na salamu alyekum kwenye Uislam nk
Tulikuwa tunachant hare Krishna in deep mpaka mtu unahisi upo dunia nyingine kabisa ni chanting za ajabu sana
Kitu ambacho sikukipenda kabisa kwa wakrishna ni masanamu ya miungu Yao ambayo yalikuwa devilish yakionyesha ukatili mkubwa
Kulikuwa na sanamu la Shetani likichimba kifua cha mtu kwa kucha ndefu kali na kuutoa moyo huku damu zikichuruzika na yule mtu akiugulia mno. Haya mambo yapo kwenye ibada za waabudu Shetani
Sanamu lingine ni lile lenye nyoka na vichwa 12 hili lilikaa/liliwekwa pembe nne za temple na Picha zake kubwa pia
Ukiachana na hayo masanamu jamaa Wana mafundisho mazuri mno na wanatoa Misaada sana kwa jamii ambapo Kulikuwa na kitengo maalum cha kulisha maeneo fukara kilichokuwa kikiitwa FOOD FOR LIFE ambapo tulipika chakula Kila siku na kwenda kugawa mitaani kwa utaratibu maalum. mtaa maarufu ukiwa mtaa wa korongocho huko Kulikuwa na ushetani wote wa dunia hii
Lakini vilevile tulikuwa tunafanya councelling kwa wakora(hawa ni zaidi ya komando yosso).walikuwa wanavuta gundi na petrol ni watu wa kuogofya mno

Kitu cha kushangaza kuhusu Kenya ni Kwamba kuna wakora wengi ni wazungu. Hawa waliharibu kwao na kukimbilia Kenya pale temple tulikuwa nao wanne tuliowatoa mitaani. Kipindi hicho Kenya ilikuwa haifai kwa ujambazi wizi na mauaji ya kutisha. Nakumbuka tulinusurika kifo lakini tukaporwa masufuria ya vyakula tena kwa kutumia matatu

Nilikaa Kenya miezi mitatu nilijifunza Krishna consciousness na kufanya kazi ya kujitolea kwenye kitengo cha food for life Ambako unakutana na maisha ya kutisha kabisa. Watoto wadogo walivyoharibika na kuharibiwa kwa Kila kitu kuanzia kubakwa kulawilitiwa kufundishwa kutumia madawa kuua kuiba nknk.
Majibu yalitoka na tuliofaulu tulirudi South Africa kwa maandalizi ya kwenda nchi za Asia kwa mafunzo ya juu zaidi sasa
 
witnessj

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
16,714
2,000
Mkuu pale kwenye maiti ya kiume ilivyodi... Halafu ikawaje? nasubiria jamani mwendelezo....
 
G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,098
2,000
Tulimaliza miaka miwili ya kwanza na kurudi Tanzania mwaka ambapo nilikuja kugundua kuwa tayari nimeshadata na mambo ya Buddhism na meditation hivyo kipindi cha kusubiri majibu niliondoka tena kwenda Kenya kupitia Mombasa kwenda kujifunza Krishna consciousness! Hiki ni kitu kipya kabisa. Nilikaa temple ya Mombasa kwa wiki moja tu na baadae kuhamia Nairobi Mathare Rd Hare Krishna temple
Tofauti na kwenye Buddhism tulikokuwa tunachant Buddha's name -Amitofo/Amitoh'una huku tulichant hivi

Hare Krishna hare Krishna
Krishna Krishna hare hare
Hare Rama hare Rama,
Rama Rama hare hare

Hii ilikuwa ni kama salamu na muongozo ambapo kwenye salamu ilikuwa tu ni hare Krishna kama amitofo kwnye Buddhism au Bwana asifiwe kwenye ukristo na salamu alyekum kwenye Uislam nk
Leo kuna kitu nakiamini hapa,hapa Mwanza nina rafiki yangu m1 mzee wa kihindi maalufu tu,katika urafiki wetu uliotokana na biashara alikua anakodi gari yangu mala kadhaa kutembelea na tulikua tukiongea mengi ya maisha kama marafiki,siku moja akaniambia kuna mtume wao amekuja sehemu yao hapo ya ibada kama nitapenda na mimi niende pale kujifunza mengi,jamani ilikua sa1 za jioni ktk sinagogi lao pale makoroboi,tulipoingia kitu kilichonishangaza ni umati mzima uligeuka nyuma kututazama japo sikustuka kitu nikaja kustuka wakati ibada ikiendelea kua nimeingia mahala si pangu,na walikua wakicheza vijana kule mbele ya sinagogi kama madhabahuni wakimzunguka huyo mtume wao na alikua amenyoa nywele zote nikashindwa kujua ni mzungu au muhindi,ila waliokua wanaimba hiyo Hare Krishina walikua mchanganyiko na vijana wa kiafrika toka kenya! Sikuweza kumaliza ibada hiyo maana niliona wazimu,na wakati namuaga huyo rafiki yangu mishale ya saa mbili hv akanitoa nje hapo kulikua na meza ina vitabu vingi vimeandikwa lugha tofauti tofauti na kiswahili pia,akaniambia pata kitabu kimoja uwe unajisomea kumjua mungu wetu,ni kweli nilikinunua na hapo ndo nikajilidhisha zaidi kua niliingia mahala kwa kupakulupukia,nilikaa na hicho kitabu kama wiki moja hv lakini kila nikisoma nakua napigwa kama na bumbuwazi na ninastuka kujua hadithi ya ninachokisoma sielewi kitu,nakua naenda mbele na kurudi nyuma lakini sielewi kabisa kitabu kinamaanisha nini na nikaamua kukitupa.hiyo ilikua mwaka 2008
 
Rolandi

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
894
500
Tatizo la haya mambo ya supernatural ukishayajua unapata msukumo wa kuapply in real life,nakumbaka kama miaka kumi iliyopita wakat nikiwa shule katika pitapita zangu nlipata kujifunza SPELLS(sjui neno lake lakiswahili) kadhaa,basi nkiwa nna soo shule ama home naziandika kwenye karatasi jeupe then nachoma moto ama kutia katika maji kisha yale majivu ama maji nayamwaga eneo ambalo mwalimu atapita,basi lile soo linapotea katika mazingira ya kutatanisha hata kama ilikuwa ni ishu ya kufukuzwa kabisa shule
Hiyo spell matata! Nishaisikia lkn sijajaribu. Ziko almost za kila kitu. Naona kama ni ushirikina hivi!
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
140,697
2,000
Tumalizie simulizi yetu sasa
June ya 1999 tuliondoka Tanzania wanafunzi 5 tuliofaulu kuendelea kwa masomo ya juu zaidi Taiwan, lakini tukipewa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja cha kuzunguka na kufanya practical kwenye temple mbalimbali za Taiwan, Singapore, Malaysia Indonesia, Bangkok Hong Kong nk
Tulizunguka kote huko tukifanya ibada presentations na kujifunza mila na desturi za kibudha kwa kila nchi.....! Tulikuwa na wakati mzuri sana baada ya mateso yote ya South Africa.. Tulifanya mengi kwa kwakweli kuanzia shughuli za kijamii mpaka za kiroho nknk

Kuna tukio la Malaysia hili ningependa nilisimulie pia
Ilikuwa siku moja tunatoka mji mmoja unaitwa Surabaya kurudi Kuala lumpa kwa ndege hali ya hewa ilikuwa mbaya sana na ukikaribia Kuala Lumpur kuna Kilima ambacho husababisha ajali nyingi za ndege.

Ikabidi tuombwe kufanya chanting.. Wanaume tukaingia kazini tukachant ile kikwelikweli.. Nilichant mpaka nikajisahau hatari iliyokuwa mbele yeti. Baada ya kama dk 15 hivi rubani alipata upenyo katikati ya wingu nene na tukatua salama
Mapokezi tuliyoyapata siku ile sitakaa Nisahau..wiki ileile kuna ndege iligonga kile Kilima na kuua abiria wote pamoja na rubani

Tulimaliza kipindi cha mpito na kutakiwa kufanyiwa ordination ambayo ni kuchomwa kichwani dot 3 na moto wa mshumaa mdogo. Vinauma saana na baada ya hapo hizo alama hazifutiki kamwe...kufikia hapo niliomba PO na kurudi Tanzania kuanza maisha mapya uraiani

Ndio mara ya kwanza nimesimulia kwa undani kabisa habari za Buddhism na meditation kuna vingi sijagusia kama habari za Taoism confuscious na sect nyingine ndogo ndogo Zenye mahusiano na Buddhism
 
saadmad

JF-Expert Member
Aug 12, 2011
521
250
Habari nilipita kwa bahati nikavutiwa na uzi naomba ufafanuzi kidogo kuhusu hii chanting n giving offerings kwa milefo,na hungry ghost kisha breakfast sababu nilipata bahati kidogo wakati nasoma foundation of faith n ethics kama sub course katika taaluma yangu na tukasoma kidogo ubudha so sijaelewa elewa hapo mkuu!!
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
140,697
2,000
Habari nilipita kwa bahati nikavutiwa na uzi naomba ufafanuzi kidogo kuhusu hii chanting n giving offerings kwa milefo,na hungry ghost kisha breakfast sababu nilipata bahati kidogo wakati nasoma foundation of faith n ethics kama sub course katika taaluma yangu na tukasoma kidogo ubudha so sijaelewa elewa hapo mkuu!!
Chukua muda uisome yote kuna Kila jibu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom