A day in the Buddhist college

Mkuu mshana jr kuna tofauti kati ya ibirisi na Lucifer???!

Kuna post kule jukwaa la dini nitawaomba tena mods waitoe kule wailete huku inajibu Kila kitu

1440014018911.jpg
 
Last edited by a moderator:
Aiseee!!!nmejua tofaut tiyar

Tukiendelea ni Kwamba zile ibada za kuchoma pesa kimsingi hazikuwa na mahusiano na Buddhism ya moja kwa moja ndio zilikuwa za siri Mno na hazikufanyika Lila Jumapili bali siku maalum

Kama nilivyosema awali kuwa tuliongozwa na sheria kali kwenye Kila kitu lakini pia tulikuwa na amri tano zinazofanana nyingi na amri kumi kwenye ukristo

1.Usiuwe chochote
2.Usiibe/usimiliki kisicho chako
3.Usiseme uongo kwenye lolote
4.Usizini(labda uandikiwe na Dr Kama tiba)
5.Usitumie kilevi cha aina yoyote

Amri ya kwanza ilihusika na kutokula nyama yaani chochote chenye uhai lakini kuna mazingira ambayo Buddhist aliruhusiwa Kula nyama nayo ni
-Hakuna Jinsi nyingine ya kuishi
-haikuchinjwa kwa akili yako
- hukuona ikichinjwa
-huli kwa ajili ya hamu za mwili

Kwenye amri ya kuiba ilikuwa hivi, Ili tendo la wizi likamilike hupitia hatua kama tano hivi
-Mawazo au fikra za wizi
-kuweka mipango sawa
-kutimiza lengo
-kuficha baada ya kuiba
-kumiliki Kuuza kugawa au kutumia

Amri ya tatu ilikuwa ni kufundishwa kwenda kinyume na mazoea ya kiasili ya ufahamu wa binadamu! Kujitetea kwa kusema uongo na kudanganya. Kwamba ita nyeusi nyeusi au njano njano.....japo kuna mazingira yaliruhusu kudanganya kama kwa njia Hiyo utaokoa uhai

Amri ya nne sisi kama Ma novice hatukutakiwa kabisa kuishi Maisha ya uasherati kwakuwa hicho ni kikwazo kikubwa sana kwenye Maisha ya kibuddha meditation na dhana nzima ya enlightment

Amri ya tano nayo ilikuwa hivyohivyo pombe na vilevi ni kikwazo kikubwa Sana kwenye path ya self cultivation...vilevi vinaharibu akili na kuleta madhara mwilini huku vikichagiza matendo mabaya
 
Mmh. Hapo namba 4. Kama cjakuelewa vile tiba kivipi?

Siku hizi hiyo ni unsupported format kwakuwa porn pics na videos zipo kila mahali lakini hata miaka ya karibuni kabisa imean wayback 90,s kwenye boarding schools hasa za wanawake kulikuwa na ugonjwa maarufu wa kuchekacheka na tiba yake ilikuwa ngono
 
Mungu wangu! wengine tuna kaugonjwa ka kucheka cheka lakini hamna uhusiano na hiyo tiba. Kuanzia leo sicheki tena ukauzu tu.
 
Mkuu mshana jr kwenye Ibada ya kuchoma pesa nini hasa malengo yake???!,

Ni khafala,ni Baraka na kutoa Pesa kwa budha na kupata zaid???
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mshana jr kwenye Ibada ya kuchoma pesa nini hasa malengo yake???!,

Ni khafala,ni Baraka na kutoa Pesa kwa budha na kupata zaid???

Haya hayana uhusiano kabisa na buddhism bali ni mambo ya kimila na kishirikina zaidi
 
Last edited by a moderator:
Ubudha si ushetani lakini pia hauna Uungu ndani yake
Unajua kuna shetani(ibilisi) na Lusifer hawa wawili wote ni roho walioasi toka mbinguni
Shetani ndiye aliyemdanganya(kumwambia ukweli? )hawa Kisha akalaaniwa
Lucifer yeye alitaka kuwa kama Mungu yaani apate mamlaka na uwezo wa kimungu! Lakini akashindwa na kutimuliwa mbinguni

Kwahiyo Shetani alilaaniwa na kufukuzwa kutoka Eden lakini Lucifer yeye hakulaaniwa bali allifukuzwa toka mbinguni....kufika huku duniani shetani akawa ni roho kamili ya ibilisi inayodanganya na kupotosha watu
Lakini Lucifer yeye akachukua umbo la mwanadamu na kuendelea na mkakati wake wa Kupata uwezo na akili zaidi Ili Amfikie Mungu ndipo hapo synagogue la kwanza la luceferianism lilianzishwa na as time goes on wakatokea kina Illuminati Freemasons Buddhism confuscious nknk

hatar sana lol
 
Tatizo la haya mambo ya supernatural ukishayajua unapata msukumo wa kuapply in real life,nakumbaka kama miaka kumi iliyopita wakat nikiwa shule katika pitapita zangu nlipata kujifunza SPELLS(sjui neno lake lakiswahili) kadhaa,basi nkiwa nna soo shule ama home naziandika kwenye karatasi jeupe then nachoma moto ama kutia katika maji kisha yale majivu ama maji nayamwaga eneo ambalo mwalimu atapita,basi lile soo linapotea katika mazingira ya kutatanisha hata kama ilikuwa ni ishu ya kufukuzwa kabisa shule
 
Tuendelee na simulizi
Chuoni tulikuwa na nyakati za furaha pia
Siku za Jumapili kwakuwa ilikuwa kama visiting day tulipata wageni wengi sana na chakula kilikuwa kizuri
Jumatatu pia kwakuwa ndio siku ya mapunziko
Tukialikwa kwenye matamasha na mashindano ya martial arts
Lakini cha Ajabu kuliko zote ilikuwa tukialikwa kwenye misiba

Huko kulikuwa kuzuri Sana kwakuwa baada ya kumchoma marehemu(cremanation) tuliandaliwa misosi ya maana Sana, Yani tulikuwa hatuoni soo kabisa kuiandaa maiti mwanzo mwisho mpaka kuichoma moto kishapo kwenda Kura as if tuko kwenye Sheree.... Binafsi nilichoma zisizopungua 20. Naomba niseme tu Kwamba sikuwa na hisia zozote juu ya wale marehemu

Chuoni pia tulikuwa na likizo na kipindi cha likizo tulipelekwa sehemu mbalimbali kutembea kama watalii kabisa! Nimetembea nchi na miji mingi sana kwasababu ya hiki chuo

Kuna thread nyingi nimesimulia sana kuhusu wafu mochwari na maiti ni kupitia chuo hiki ndio nilijifunza yote hayo kwa nadharia na kwa vitendo! Mochwari ni sehemu inabeba mambo mengi ya kuogofya mno ya kutisha kushangaza lakini pia sometimes kuchekesha

Kwa mfano siku moja nikiwa session mochwari ililetwa maiti moja ya like ikiwa almost uchi ikikamilika Kila idara sasa wakati inafanyiwa utaratibu wa kuwekwa kwenye barafu ilalazwa pembeni mwa maiti ya kiume nayo ikiwa uchi kabisa.... Aisee hivi mnajua ile maiti ya kiume ilidindisha?
 
Tuendelee na simulizi
Chuoni tulikuwa na nyakati za furaha pia
Siku za Jumapili kwakuwa ilikuwa kama visiting day tulipata wageni wengi sana na chakula kilikuwa kizuri
Jumatatu pia kwakuwa ndio siku ya mapunziko
Tukialikwa kwenye matamasha na mashindano ya martial arts
Lakini cha Ajabu kuliko zote ilikuwa tukialikwa kwenye misiba

Huko kulikuwa kuzuri Sana kwakuwa baada ya kumchoma marehemu(cremanation) tuliandaliwa misosi ya maana Sana, Yani tulikuwa hatuoni soo kabisa kuiandaa maiti mwanzo mwisho mpaka kuichoma moto kishapo kwenda Kura as if tuko kwenye Sheree.... Binafsi nilichoma zisizopungua 20. Naomba niseme tu Kwamba sikuwa na hisia zozote juu ya wale marehemu

Chuoni pia tulikuwa na likizo na kipindi cha likizo tulipelekwa sehemu mbalimbali kutembea kama watalii kabisa! Nimetembea nchi na miji mingi sana kwasababu ya hiki chuo

Dah! mkuu uko mbali mno, daftari yako ya historia ya maisha yako itakuwa ya kusisimua,kuogofya na kufurahisha lakini pia kuna mambo mengi binafsi napata elimu kupitia hii stori yako, unajua wengine tunautazama huu ulimwengu katika mtazamo tofauti na ulivyo....mmh ni hatari.
 
Back
Top Bottom