Jarida la Ebony liliponea chupuchupu kufungiwa biashara kwa kosa la kutumia picha ya Yesu mwenye asili ya Afrika (Black Jesus)

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Walichapisha toleo la Machi mwaka1969 la Jarida la Ebony na kuweka picha ya Yesu Mweusi kwenye jalada.
Watu wengi katika jumuiya ya watu Weusi walikasirika sana hadi kutishia kughairi usajili wao.
Walilalamika wakasema Dunia imefika mwisho mpinga Kristo yuko kazini walimtumia Johnson picha za yesu Mzungu ili akachapishe picha za yule Mzungu ambaye wengi wanaamini ni "Yesu wa Kweli (Mzungu)".

Tunapo fundishwa kuwa Yesu ni mweupe katika akili za watu Weusi ni mojawapo ya mipango ya vita vya kisaikolojia iliyopata mafanikio makubwa zaidi katika historia ya binadamu.

Fikiria kwa kina na ujiulize swali lifuatalo:
Ikiwa kila kitu hadi rasili mali vilichukuliwa kutoka kwa watumwa (kusoma, utamaduni, lugha n.k.) kwa nini Ukristo walituachia tuabudu pamoja wakati wao walituona sisi kama Punda?
Sababu ya kweli kwa nini mabwana wa watumwa wa Afrika waliona ni muhimu kubadili watu Weusi kuwa Wakristo.

Katika kipindi cha kwanza kabla wazungu kuwageuza watu Weusi kuwafanya Wakristo kitu cha kwanza walitangaza Watu weusi si binadamu walio kamilika inatakiwa wabatizwe na waokoke.
Kwa sababu hizi wakoloni wazungu na mabwana weupe walisema kwamba watu Weusi kwa kweli hawawezi kamwe kuingia katika ufalme wa Mungu (waliodhaniwa kuwa wataingia mbinguni ni watu weupe wote) yaani wazungu wote wataingia na wataishi mbinguni.
Iliamika hivyo kutona maneno ya ubaguzi wa rangi juu yetu sisi watu Weusi wale wazungu waliowageuza mababu zetu kuwa Wakristo wao waliamini kwamba wazo la mtu mweusi kuingia mbinguni lilikuwa la kipuuzi ilikuwa nisawa mtu aseme kwamba mbwa anaweza kuingia mbinguni.

Tunapoutazama ukweli, mabwana wa watumwa weupe na wakoloni hawakutuletea Dini ili kuokoa roho za watu Weusi waingie mbinguni. .
Ukweli wa mambo ni kwamba Biblia ilitumika kuwatengeneza Waafrika katika akili zao waachane na kilakitu wahangaikie kuingia katika Ufalume wa Mungu.
Hata huko Amerika Watumwa weusi walipewa dini ya Kikristo iliyowafundisha kuamini Mungu niwa wazungu tu. (Mungu mweupe, masihi mweupe,.malaika weupe na manabii weupe).
Sababu ya kuwaletea Dini ilikuwa ni kuwaondolea kujikubali na kuingiza hadithi ya uungu wa kizungu katika akili zao za pamoja za watumwa wa Kiafrika kuamini kwamba Mungu,Yesu,Malaika na manabii wrote ni wazungu.

Picha hizi za miungu "weupe pekee" zilitengenezwa kimakusudi ili kuingiza imani potofu ya uungu mweupe katika akili za watumwa Waafrika.

Picha za mwana wa Mungu mweupe kimakusudi hutengeza dhana yenye mantiki kwamba ikiwa mwana wa Mungu ni mweupe basi Mungu (baba) lazima pia awe mweupe. Hitimisho hili la kimantiki limesababisha watu wengi Weusi kumwabudu Mungu mweupe kwa umakini.
Wakoloni weupe na watumwa walijua kwamba kwa kuwafundisha watu Weusi kumwabudu masihi mweupe na Mungu mweupe kwa uangalifu kwamba iliwafanya watu weusi wawa heshimu na kuwaogopa watu weupe wajitume bila kutumikishwa ili kuwavutia watu weupe.
 
Watakuja kuuliza picha????


00B1C57A-84D9-4A19-B77B-17BADD9EF6D0.jpeg
 
“Jesus was black,Ronald Reagan was the devil and the gorvenment is lying about 9/11”-Huey Freeman!!! Pia imenikumbusha episode ya Its a Huey Freeman Christmas when Huey tried to potray about black Jesus!!! Pia imenikumbusha episode ya The passion of uncle Ruckus!! I wish mtoa mada ungekuwa umewahi kuicheki hii comic series inaitwa THE BOONDOCKS Cc Chaliifrancisco
 
Aiseee yaani anakufanya mtumwa halafu anakubatiza ili upate kwenda peponi. Huku akikudharau na kukufananisha na kima lakini dharau zote hizi anataka uwende peponi nae
Kiukweli inawazisha sana, kwa vitu walivyotufanyia ilihitaji sijui akili gani kwa mtu mweusi kuukubali ukristo na uislam....
 
Kwa kweli inabidi tutafakari sana, yalivyokuja mapinduzi ya viwanda kawakutaka kuleta huku ndio kwanza ata wagunduzi wetu walikatwa mikono lakini Africa hii kila kijiji haijalishi kipo mbali kiasi gani lazima awe mkristo au mwislam
SmartSelect_20220727-215134_Instagram.jpg
 
Aseee, but ni bora kuabudu ili mwisho wa wakati akiwepo akuweke kundini badala ya kuacha kuabudu ilihali hujui lolote na siku ya mwisho hata km hayupo hautakuwa umepoteza kitu.
 
Aseee, but ni bora kuabudu ili mwisho wa wakati akiwepo akuweke kundini badala ya kuacha kuabudu ilihali hujui lolote na siku ya mwisho hata km hayupo hautakuwa umepoteza kitu.
Ushapoteza uhuru wako wa hapa duniani
 
Kiukweli inawazisha sana, kwa vitu walivyotufanyia ilihitaji sijui akili gani kwa mtu mweusi kuukubali ukristo na uislam....
Aliukubali kwa mijeredi mizito kama alivyokubali kujenga mijengo mikubwa,reli na kuwalimia mashamba 24/7 nonstop.Hapa itabidi hili nalo litazamwe upya ili tupate mwelekeo mpya!

Kuna mchungaji mmoja ni kama nilimuelewa.Anasema mtu asikudanganye eti anakuombea kikubwa anatakiwa akufundishe jinsi ya kuomba ili basi ujiombee mwenyewe.kwahiyo unawezekana Mungu yumo ndani yetu haya mengine tunapotezewa mida!
 
Ushapoteza uhuru wako wa hapa duniani
Chief, kupoteza uhuru wako ninoale unapokuwa huna uhuru wa kufanya jambo lolote na huwezi kuingia, kutoka kwenda popote hiyo ni sehemu ya kukosa uhuru.

Mpaka muda huu unapoandika/ninapoandika na kutoa mawazo yangu ni sehemu ya uhuru wa kifikra na mawazo ambayo Allah amenitunuku.

Waliopoteza uhuru unajua walipo muda huu.
 
Chief, kupoteza uhuru wako ninoale unapokuwa huna uhuru wa kufanya jambo lolote na huwezi kuingia, kutoka kwenda popote hiyo ni sehemu ya kukosa uhuru.

Mpaka muda huu unapoandika/ninapoandika na kutoa mawazo yangu ni sehemu ya uhuru wa kifikra na mawazo ambayo Allah amenitunuku.

Waliopoteza uhuru unajua walipo muda huu.
Naona hatujaelewana.....hizo sheria tu za hio imani unayoifata tayari ni utumwa
 
Aseee, but ni bora kuabudu ili mwisho wa wakati akiwepo akuweke kundini badala ya kuacha kuabudu ilihali hujui lolote na siku ya mwisho hata km hayupo hautakuwa umepoteza kitu.
kama ni muislamu maneno haya yanaashiria udhaifu wa imani ya msemaji wa haya maneno, maana waumini wanapaswa kuwa na yaqini kabisa juu ya kile wanachokiamini na sio kuwa na imani ya shaka kuwa ukimkuta haya usipomkuta haya hii sio sawa.
 
Back
Top Bottom