85% ya gamba la Lowassa halina ukurutu. Halihitaji kuoshwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

85% ya gamba la Lowassa halina ukurutu. Halihitaji kuoshwa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Nov 25, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Nov 25, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  EL kaamua kuchukua maamuzi magumu kwa kuuanika ukweli wa mambo hadharani. Hata hivyo naona kama kachelewa sana kuonyesha juhudi zake za kujisafisha. Hata hivyo kwa kuonyesha kuwa gamba lake halina ukurutu nampa zawadi ya ushindi kwa 85% Namkata 15% kwa kosa la kuujua ukweli na kukaa kimya. Kazi kwako gamba mkuu wa magamba!
   
 2. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Ushindi upi na ukweli gani anaujua?...hamna kitu hapa huyu jamaa ni fisadi tena papa_hii ni picha ambayo yeye(EL)na swaiba wake (******_JK)wanataka kuicheza ili wapokezane vijiti vya uongozi wa nchi.......pumbafuuuuuuuuuuu
   
 3. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  soma hii!

  Sikuamini macha yangu, nikasoma magazeti mpaka matatu ili nijiaminishe, sasa nimeamini kuwa JK ni msanii wa kutupwa.
  Baada ya Lowasa kujitetea kuhusu Richmond na kufanikiwa kumhusisha JK na Richmond, pia alimtuhumu Nape kwa kumchafua yeye ( Lowasa) bila ushahidi, alifuatia waziri mkuu mstaafu Sumaye ambaye pamoja na maelezo mengine ya kumtetea Lowasa alihoji, tuwafanyeje Nape na Chiligati ikiwa kamati ya maadili itamsafisha Lowasa? aliuliza Sumaye. Hii ni kutokana na kwamba hawa akina Nape wameshazunguka nchi nzima kumchafua Lowasa kama bw Lowasa alivyotuambia. Kitu ambacho sikutegemea,
  JK alikadakia kauli ya Sumaye na kusema, watachukuliwa hatua za kinidhamu.
  Sakata hili ni baada ya NEC kukubaliana na pendekezo la CC ya NEC lilisomwa na Pius Msekwa la kuomba suala kujivua gamba lirudishwe ktk kamati ya maadili, hoja ambayo ilipita.

  My take,
  Mbele ya macho yangu, ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee mwaka 2011, JK akiwa mgeni Rasmi ktk tamasha Nyimbo za Injili alituambia, Nape anayoyazungumza kuhusu gamba siyo maneno yake mwenyewe bali ya ccm - ndiyo kazi tuliyomtuma.
  Jana alisema kama ikidhihirika ktk kamati ya maadili kuwa Nape alimtuhumu Lowasa Bila kufuata utaratibu wa chama basi atachukuliwa hatua za kinidhamu.

  Ikumbukwe kwamba;
  Hoja mojawapo ya Lowasa na Sumaye ni kwamba, kwa nini suala la Lowasa halikupelekwa ktk kamati ya maadili kama ilivyotaratibu za Chama na badala yake Nape akalikimbiza ktk vyombo vya habari?
  Pili, Ikimbukwe kuwa ktk maelezo ya Lowasa alisema, Mkiti unakumbuka ukiwa nje ya nchi, nilikupigia kukushauri kuwa tuvunje mkataba wa Richmond, wewe ukasema ngoja tusikie ushauri wa kamati ya makatibu wakuu ambao ndo waliosababisha mkataba usivunjwe?
  Tatu, mkiti unafahamu kuwa hakuna jambo nililofanya ambalo sijakushirikisha, kila kitu unajua.
  Nne, Lowasa akiwa ameshika hansard ya Bunge aliuliza ripoti ya Richmond haijasema nimehusika, ilisema ninapaswa kuwajibishwa kutokana na makosa ya watendaji walioko chini yangu.

  My take 2
  Nini hatma ya Nape Ndani ya CCM?
  Je, tukisema kuwa ccm imefika mwisho huu utakuwa ni ushabiki wa kisiasa?
  Je, Lowasa kufanikiwa kumhusisha JK na Richmond moja kwa moja, JK atapata wapi ujasiri wa kuendeleza zoezi la kuwavua wengine gamba au kupambana na ufisadi.
  Je, kama zoezi la uvuaji wa gamba likihitimishwa kwa staili hii, nini kitawafanya watz wasiichague Chadema 2015?
  je, hoja ya Chadema ya Ufisadi ambayo waliiparamia sasa si itawabakiza magamba kweli.
   
 4. c

  chegreyson JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 735
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 60
  Kasema aliachia ngazi kulinda heshima ya serikali na chama chake.Kigumu kuelewa hapo ni nini?
   
 5. d

  davidie JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama issue ilikua kukilinda chama chake na serikali yake kwa nini bado anataka kurudi tena kwenye chama na serikali ile ile yenye uozo? Ana lipi jipya? Au nae anataka kulipa lkisasi?
   
 6. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,260
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  Nape watch out the movie is not finished yet! Actually you are the one in sniper mind to be removed from scene!
   
 7. Dogo Tundu

  Dogo Tundu JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 441
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  duu, EL kweli anaweza kuchukua japo maamuzi mazito! jamaa kafanikiwa kumlipua mwenye kaya.... EL for 2015. hakuna wa kumzuia.
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,565
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kuliona hili...this is great post my friend! in other words msalaba atakaoubebea Kikwete kwa sasa ni mdogo mno ukilinganisha na alioubeba Kikwete..........mpaka ziishe episode zote Lowasa yuko Ikulu
   
Loading...