50kms kwenye Highway: Tuanze kufikia suluhisho ambalo ni kuweka vivuko vya juu au chini vya waenda kwa miguu

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,586
4,274
Mimi nashauri badala ya kuongeza vibao ya 50kms/ kwenye barabara kuu

Tuanze kufikia suluhisho ambalo ni kuweka vivuko vya juu au chini vya waenda kwa miguu

Mfano: Barabara ya Arusha kwenda Dar; kutokea Arusha hadi Same miji inaunganika kwa kasi sana, sasa bila kuanza kufikiria suluhisho itafika wakati mtu anaendesha km 50 kwa zaidi umbali ya km 300 na itakuwa ni kudumaza uchumi kwa kupunguza uzalishaji
 
Ng'ombe na mbuzi nao watapita juu ya vivuko? Ukiachana na Binadamu kuna wanyama hayo maeneo na wafugaji ni wengi. Safiri usiku tu.
 
Ng'ombe na mbuzi nao watapita juu ya vivuko? Ukiachana na Binadamu kuna wanyama hayo maeneo na wafugaji ni wengi. Safiri usiku tu.
Kiongozi, zaidi ya robo tatu ya maeneo ya barabarani hayana wafugaji wenye ulazima wa kuvusha mifugo barabarani lakini pia sijasema zitolewe kwa asilimia 100%. Nakujulisha tu kuwa nimefanyia utafiti kabla ya kuandika
 
Sheria za makazi Tanzania zimekaa kienyeji sana.

Hata upeleke barabara porini kesho yake unakuta watu wameshaanza kujenga nyumba pembeni wakiamini fursa zitakuja.

Tanzania kulitakiwa kuwe na super hughway ya kuunganisha maeneo ya mbali.
 
Sema ukweli vibao vya 50 vinazungua. Sasa unakuta highway nayo trafiki wanategea uzidi 50 wakulambe mzigo. Suluhu ni kujenga daraja za budget ndogo wavukaji wapite juu hasa maeneo ya watu wengi.
 
Wenzetu kama South Africa wameweza. Ni swala la kukaa chini na kufanya upembuzi tu. Inawezekana kabisa kuwa na highway isiyokuwa na matuta. Kweli speed ya 50km/hr na kuongezea matuta vinaleta shida barabarani.
 
Ng'ombe na mbuzi nao watapita juu ya vivuko? Ukiachana na Binadamu kuna wanyama hayo maeneo na wafugaji ni wengi. Safiri usiku tu.
Hii ya usiku nayo imekaa vizuri kama ni mzoefu na hauna usingizi, maana changamoto ya usiku huwa ni kumulikana tu,hivyo usipokuwa mzoefu na njia unaweza kukuta gari iko juu ya mti.
 
Back
Top Bottom