50/50 Ni Majanga kwa Wanaume

50/50 Ni Majanga kwa Wanaume

MZIMU

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
4,058
Reaction score
1,377
Jamani hili suala la 50/50 ni Majanga kwa Wanaume. Huku Makazini hatakama kazi sio ya kutumia nguvu, lakini ukipangwa na Mwanamke basi utajuta. Kila kazi utafanya wewe. Anakuegemea kwa kila kitu. Yaani wao sio kama hawataki kujisumbua miili yao katika kutumia nguvu peke yake bali hata katika kutumia akili.

Watu wengi waliopangiwa kazi pamoja na Wanawake hua wanalazimika kufanya kazi hizo peke yao, sio kuanzia Vyuoni hadi katika research n.k.

Hawa Binadamu wenzetu, Mama Zetu, Dada zetu, Shangazi zetu, Wake zetu, Wenetu na Nyumba ndogo pia, kazi ambayo nadhani inawafaa tena zaidi ya 50/50 let say 75/25, ni kupiga Domo kamakule Mjengoni basi. Huku kwengine ni balaa.

Haya ni Maoni yangu tu kutokana na Sehemu Mbali mbali nilizopitia katika kulijenga Taifa hili Changa.

Unajua hiyo 50/50 ipo ilikuwafumba macho wanawake wengi ili wapige kura ya ndio kwa katiba ilopendekwa! Dats y wakiwa katika kampeni za kura ya ndio kwa katiba mpya hicho kipngele kinatumika sana! Lakini kwa kuwa muwazi n vgum kutekelezeka

Hii comment ya ndugu Bilulu II, nimeipenda ndio maana nimeichukua na kuiweka hapa front page.

Wakubwa wenyewe washafanya yao, iyo 50/50 ina malengo tofauti na nyie mnavyofikiri hata hao wanawake wenyewe hawaelewi zaidi ya kufuata mkumbo tu.
Hili janga si Tanzania tu bali duniani kote,Jiulize Marekani wamepita marais wangapi na hakuna hata rais mmoja mwanamke!je huko marekani hakuna 50/50?

Mkuu UHURU JR hapa umesema ukweli kwa wenye akili peke yao.

Mleta mada ametaja baadhi ya kazi ambazo wanawake wanakuwa tegemezi zaidi. Tena shukrani yao kubwa kwa anayemsaidia ni kumlisha "sambusa". Kazi nyingi za kutumia akili kidogo na nguvu kidogo-wanawake wanaweza. Lakini zile za kutumia akili nyingi au mitulinga-wanawake wanageuka wanakuwa parasite.

Anko Sam, Huo nao ni ukweli Mwengine ambao watu wanajifanya hawaujui.
 
Hivi 50/50, mwanamke atapewa kazi kwasababu tu ana K bila kuzingatia sifa, uwezo na mashariti ya kazi husika? Kama ndivyo, basi taifa letu litaendelea kuwa changa!
 
acheni dharau,wawezesheni wanawake wanaweza.Uko vyuoni SI kujipendekeza Tu nahuwa wanaume mnakuwa kimaslahi zaidi
 
Jamani hili suala la 50/50 ni Majanga kwa Wanaume. Huku Makazini hatakama kazi sio ya kutumia nguvu, lakini ukipangwa na Mwanamke basi utajuta. Kila kazi utafanya wewe. Anakuegemea kwa kila kitu. Yaani wao sio kama hawataki kujisumbua miili yao katika kutumia nguvu peke yake bali hata katika kutumia akili.

Watu wengi waliopangiwa kazi pamoja na Wanawake hua wanalazimika kufanya kazi hizo peke yao, sio kuanzia Vyuoni hadi katika research n.k.

Hawa Binadamu wenzetu, Mama Zetu, Dada zetu, Shangazi zetu, Wake zetu, Wenetu na Nyumba ndogo pia, kazi ambayo nadhani inawafaa tena zaidi ya 50/50 let say 75/25, ni kupiga Domo kamakule Mjengoni basi. Huku kwengine ni balaa.

Haya ni Maoni yangu tu kutokana na Sehemu Mbali mbali nilizopitia katika kulijenga Taifa hili Changa.

Kwa akili hizi, hata Kadhi ni manyanyaso kwa akina mama no wonder tafiti zinaonesha wengi wao hawataki kusikia huo upuuzi. Mkuu MZIMU, kwa maandiko yako humu JF yumkini wewe ni Kadhi mtarajiwa; hivi kweli kwa utumbo ulio-post hapa wanawake wa Kiislamu watapata haki kwa mashauri utayoamua wewe!?

Kila jinsia ina mapungufu yake na pia sikubaliani na issue ya 50/50 iwe ni mwanamke au mwanaume anapendelewa ila kwa lugha uliyoitumia dhidi ya akina mama inaonekana una dharau sana wewe. Hebu kuwa na staha au ndio lugha za makadhi mnaotaka walipwe mishahara hadi na makafiri?
 
Last edited by a moderator:
Ndani ya 50/50 kuna uwezekano baadae wanawake wakawa na nafasi ya kutoa mahari na wakaweza kuoa kama mme na kuacha pia.

Huu ni ujinga kufuata sheria za Nchi za magharibi dini gani inayosema mwanamke lazima awe sawa na mwanamme? Kitabu gani kimesema hivo?

Kwetu sisi waislamu ikiwa mke atakuwa sawa na mme ni kuwa hakutakiwi tena kuwe na mahakama ya kadhi maana yake sheria zote ziko wazi za wazungu
 
Kwa hiyo unataka mwanamke asiwe sawa na mwanamme ili kuwe na mahakama ya kadhi? Hivi mahakama zipo kwa ajili ya wanadamu au wanadamu kwa ajili ya mahakama?
 
Acha dharau, Mimi mke wangu namuona anawasha laptop hadi Jumapili anapiga kazi na siku nyingine akitoka kazini baada ya kumaliza kuandaa chakula usiku anawasha laptop kuandika taarifa au kumalizia ripoti inatakiwa asubuhi kazini kwao. Kwa hiyo siamini kama ni mtegemezi ofisini kwao. Pia nawajua baadhi ya wanaume wanaenda kazini wanakaa dk chache wanachomoka kwenda BAR ya jirani kupiga masanga. Vipi kuhusu wale akina Dada wa benki hasa Tellers, kuanzia saa tatu asubuhi hadi jioni wanapiga kazi tu, sijawahi kuona mwanaume pembeni akiwafanyia kazi kama unavyotaka tuamini. Wewe lazima utakuwa Mkurya unaamini wanaume tu ndio wanaweza kufanya kazi wanawake hamna kitu, hutaki kuachana na imani potofu. Vipi kuhusu Halima Mdee, juzi napiga kazi ya maana Sana pale Furahisha Mwanza
 
acheni dharau,wawezesheni wanawake wanaweza.Uko vyuoni SI kujipendekeza Tu nahuwa wanaume mnakuwa kimaslahi zaidi

Hii kauli uwa siielew vzuri... wakiwezeshwa wanaweza!!??
 
Hii kauli uwa siielew vzuri... wakiwezeshwa wanaweza!!??

Huelewi nini hapo? Jamii zetu nyingi zimekuwa na desturi ya kutomjali au kutomwendeleza mtoto wa kike na ndicho chanzo cha wao kuwa myuma kimaendeleo kulinganisha na jinsia ya kiume. Ni suala lililo wazi kwamba ndani ya familia zinazoendekeza ukale (conservatism) mtoto wa kiume ndio hupewa elimu pamoja na kurithishwa mali, ardhi, n.k.

Kuwezeshwa kunakoongelewa hapa ni kuwapa watoto wa kike haki sawa ya elimu, haki sawa ya mirathi, haki sawa ya kumiliki ardhi, n.k. Kwa upande wa elimu baada ya kampeni ya muda hata wewe ni shahidi jinsi akina dada wanavyowatoa kamasi vijana wa kiume kwenye elimu kuanzia elimu ya awali hadi PhD's hata Mamndenyi na FaizaFoxy ni mashahidi labda kama waliozeshwa ndoa za utotoni kutimiza sunna.
 
Huelewi nini hapo? Jamii zetu nyingi zimekuwa na desturi ya kutomjali au kutomwendeleza mtoto wa kike na ndicho chanzo cha wao kuwa myuma kimaendeleo kulinganisha na jinsia ya kiume. Ni suala lililo wazi kwamba ndani ya familia zinazoendekeza ukale (conservatism) mtoto wa kiume ndio hupewa elimu pamoja na kurithishwa mali, ardhi, n.k.

Kuwezeshwa kunakoongelewa hapa ni kuwapa watoto wa kike haki sawa ya elimu, haki sawa ya mirathi, haki sawa ya kumiliki ardhi, n.k. Kwa upande wa elimu baada ya kampeni ya muda hata wewe ni shahidi jinsi akina dada wanavyowatoa kamasi vijana wa kiume kwenye elimu kuanzia elimu ya awali hadi PhD's.

Kwa sababu kwene interview pia wanawezeshwa sana.. maofisin hali kadharika mavyuon wanawezeshwa kwa namna tofautitofauti
 
Mie binafsi sitaki 50/50. Ila ninacho taka ni uwezo wa mtu ndio ufanye kazi basi.
Kama sehemu husika wanawake watakua 70 na wanaume 30 sawa ili mradi wanafanya kazi inavyotakiwa.
Hivyo hivyo hata kwa wanaume.
Na hata ikifika mahali hakuna mwanaume au mwanamke na kazi inaenda inavyotakiwa ni sawa.
Lakini hii ya 50/50 kuna wengine wataingia kwenye majukumu hana uwezo na wengine wataachwa wenye uwezo ili kukidhi tu 50/50.
Tanzania ni nchi ya ajabu sana.
 
kwakuwa na 50/50 basi yawapasa nao kucompite ile kaul ya mwanamke kwanza ndo mwsho wake. Wote tutakuwa sawa hivyo ni wakat wao kuingia kwenye ushindan wakifanikiwa basi hata nafas zote washike. Na wakishindwa basi ndo iwe hivyo mambo ya ladies first hakuna wote 50/50.

Mtazamo tuu.
 
wanawake wa kitanzania ni bado sana kuwakabidhi uongozi, ili kuamini kama bado angalia ulipokua unasoma nao
 
Unajua hiyo 50/50 ipo ilikuwafumba macho wanawake wengi ili wapige kura ya ndio kwa katiba ilopendekwa! Dats y wakiwa katika kampeni za kura ya ndio kwa katiba mpya hicho kipngele kinatumika sana! Lakini kwa kuwa muwazi n vgum kutekelezeka
 
Kwa kawaida wana usemi wao wanasema "ukimwezesha anaweza" kiasili ni kwamba hawezi
Mpaka umpige stata tuache dharau
Ila wanatakiwa kupigwa stata ila
Ikumbukwe anaepigwa stata si
sawa na anayempiga stata
Hamuwezi mpaka muwezeshwe huo ndio ukweli na utaendelea kubaki hivyo hiyo
 
Hii kauli uwa siielew vzuri... wakiwezeshwa wanaweza!!??

Katika matangazo ya kazi huwa kuna statement hata mimi huwa siielewi

Women are encouraged to apply!

Kwa wale manaofahamu maana yake nini?
 
Kwa akili hizi, hata Kadhi ni manyanyaso kwa akina mama no wonder tafiti zinaonesha wengi wao hawataki kusikia huo upuuzi. Mkuu MZIMU, kwa maandiko yako humu JF yumkini wewe ni Kadhi mtarajiwa; hivi kweli kwa utumbo ulio-post hapa wanawake wa Kiislamu watapata haki kwa mashauri utayoamua wewe!?

Kila jinsia ina mapungufu yake na pia sikubaliani na issue ya 50/50 iwe ni mwanamke au mwanaume anapendelewa ila kwa lugha uliyoitumia dhidi ya akina mama inaonekana una dharau sana wewe. Hebu kuwa na staha au ndio lugha za makadhi mnaotaka walipwe mishahara hadi na makafiri?

Kwa hiyo unataka mwanamke asiwe sawa na mwanamme ili kuwe na mahakama ya kadhi? Hivi mahakama zipo kwa ajili ya wanadamu au wanadamu kwa ajili ya mahakama?

Hii sio mada ya Mahakama ya Kadhi. Tusime ukweli. Wanawake wengi ni Mizigo Makazini. Halafu ni watu wa Majungu sana ili waendelee kuwepo kazini. Maranyingi sana hua wanashindana kutoka na Mabosi wao ili kuwakoga wengine na kuzembea kazi.
 
Hiyo 50/50 ni gia ya mwisho ya CCM kufanya katiba yao ipite sababu wanajua ni rahisi mno kuzilamba kura za wanawake wakati wa kupigia kura rasimu yao.

Kiuhalisia wanachodai wanawake si hiyo 50/50 - bali yapo mambo ya msingi kabisa ambayo wanakandamizwa hasa kuanzia ngazi ya familia.

Hata Mwenyezi Mungu hajatuumba kwa kutumia hiyo ratio.
 
Ndo 50/50
 
Attachments

  • 1413810168969.jpg
    1413810168969.jpg
    10.1 KB · Views: 615
Back
Top Bottom