50/50 yaweza kuwa jambo jema sana ili kuonesha usawa na sie tufanane na dunia.
Nadhani akina mama safari hii wamepata mtetezi wa kweli mwenye mamlaka makubwa ya uteuzi. Either mwenda zake alijaribu kuwa maingizo mapya mawili kwenye mifumo ambao huko nyuma nafasi hizo zilikuwa za wanaume.
VP Samia S. Hassan 2015-2021 (Ambae kwa sasa ndie C in C)
Commissioner Gen. wa Uhamiaji Dr. Anna Makakala.
Nataka kuamini hao wawili niliowataja walifika pale kwa meritocracy na ika-happen pia kuwa ni wanawake.
USA ambao wamepata uhuru na wana idadi kubwa ya wanawake waliosoma ila mpaka sasa ni nchi ya 70 kwa kiwango cha uwakilishi wa akina mama bungeni.
America lags far behind other countries on women representation in government. It ranks 75th out of 193 countries according to the Inter-Parliamentary Union.
Tunawatakia kila la heri akina mama ambao baadhi yao ni mama zetu, shangazi zetu, dada zetu, wake zetu, wanetu kwenye majukumu ya kuteuliwa na mamlaka kutumikia Watanzania.
Rai yangu kwa mamlaka ya uteuzi ni namna gani akina mama kama ambavyo wanaume au vijana wanatakiwa kuteuliwa washike nafasi by merits na sio kubebwa.
Na kwa muktadha wa sasa asiwe mtu kwa sababu ya CV (educational achievement) ila mtu mwenye uwezo wa ku-push the bounds na kufanya mambo yatokee.
Tanzania inapakana na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Zambia, Malawi na Mozambique; Baharini tuna nchi kama Comoro, Madagascar, Seychelles na Mauritius.
Tuna muono gani kulifikia hilo soko kwa mahitaji ya msingi kama chai, kahawa, korosho, cocoa, nyama, samaki, maziwa, nguo za kuvaa au vitambaa?
Tumezungukwa na nchi zenye watu wengi sana, nadhani wateule wa Mhe. Rais waje na akili zenye kuleta suluhisho linalowezekana, ni namna gani tukiamua kuuza hata biscuits nchini Comoro toka Tanzania zifike kwa haraka kwa bei nafuu kuliko Dubai?
Juzi nimenunua cornflakes, kuchungulia nikaona made in Libya; yaani linchi looote hili yet tuna import cornflakes?
It high time akina mama, wanaume, vijana wa kike kwa kiume ambao mtateuliwa na mamlaka za uteuzi mje na solutions zenye kuzalisha ajira, kuongeza exports, kuongeza tax base, kupunguza imports.
Kila la kheri tena Mama Samia Suhuhu Hassan Rais wa JMT kwenye kulijenga Taifa na kutekeleza kwa vitendo 50/50.