50/50 inayotafutwa haina msingi zaidi ya kufahamiana na kujuana

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
1,998
2,000
Ulinganifu hauwezi kuletwa na rais. Samia anatakiwa aelewe amefikaje hapo na ajiulize je, angejaribu kuomba urais wa Z’bar angeupata? Sasa anaanza kulazimisha kabla ya kuondoa mfumo na vikwazo vilivyo mbele ya wanawake. Tunajua atawateua lakini watatuangusha. Tunawaona bado wakifundishwa uvaaji wa heshima, siyo kwamba hawajui, bali wanahangika kuwavutia wanaume.

Hatua iliyo bora ni hiyo ya kuanzisha shule za wasichana za boarding, siyo kila mkoa, iwe ni kila Wilaya. Haya mengine unayoita 50/50 yataishia kuwachagua marafiki zako wa huko kwenye NGO tu na watakuja na mavazi yao ya kuiga u-zungu u-zungu wakiamini ndo maendelao.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,269
2,000
Kuteua mtu kwasababu ya Jinsia, dini, mkoa, kanda, pande za Muungano haijawahi kuwa suluhisho kwa matatizo yoyote.

Mfano mimi Mama yangu yuko kijijini, hata Rais Samia akisema ateue wanawake tupu hilo litamsaidia nini ?

Hata akisema ateue mtu wa dini atamsaidia nini ?

Matatizo makubwa ya nchi hii siyo teuzi. Teuzi ni njia tu za kugawana keki ya taifa kitu ambacho hakina faida kwa wengi.

Anyway, Mwisho wa siku watu watakuja kuangalia matokeo ya utawala wako tu bila kujali uliteua kina nani.

Wakati huo watu watakuwa wanaongelea matatizo ya MAJI, AJIRA, BIASHARA, MIUNDOMBINU, SHULE, AFYA, MALAZI, HAKI, USALAMA. Hakuna atayekumbuka kuwa uliteua watu fulani.
 
robinson crusoe

JF-Expert Member
Oct 22, 2020
484
1,000
Niliwasikiliza wakati akiongea nao hapo Dodoma. Ni kama walikwenda ili kuwazomea wanaume. Wengine walipohojiwa baada ya mkutano, ilikuwa ni mashindano ya kuzungumza kama mwingereza, na kupinda ulimi saaana!

Bungeni viti maalumu/upendeleo havijawahi msaidia mwanamke wa kijijini, badala yake vinawasaidia walioteuliwa tu na wanajiunga na kundi la wanaume kufanya mambo yao. Samia, mama! Elimisha wanawake; Jenga shule nzuri za boarding kwa kila wilaya. Achana na 50/50 ambayo haina msingi. Lakini kama unataka marafiki zako nao wale pesa za taifa hili endelea na ahadi hizo. wateue na baada ya miaka mitano utathibitisha wanawake mzigo uliowabeba.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,119
2,000
Ulinganifu hauwezi kuletwa na rais. Samia anatakiwa aelewe amefikaje hapo na ajiulize je, angejaribu kuomba urais wa Z’bar angeupata? Sasa anaanza kulazimisha kabla ya kuondoa mfumo na vikwazo vilivyo mbele ya wanawake. Tunajua atawateua lakini watatuangusha. Tunawaona bado wakifundishwa uvaaji wa heshima, siyo kwamba hawajui, bali wanahangika kuwavutia wanaume.

Hatua iliyo bora ni hiyo ya kuanzisha shule za wasichana za boarding, siyo kila mkoa, iwe ni kila Wilaya. Haya mengine unayoita 50/50 yataishia kuwachagua marafiki zako wa huko kwenye NGO tu na watakuja na mavazi yao ya kuiga u-zungu u-zungu wakiamini ndo maendelao.
Huyu maza amefeli mapema sn kuliko Rais yoyote baada ya kuanza mambo ya ajabu ajabu
 
Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,158
2,000
50/50 yaweza kuwa jambo jema sana ili kuonesha usawa na sie tufanane na dunia.

Nadhani akina mama safari hii wamepata mtetezi wa kweli mwenye mamlaka makubwa ya uteuzi. Either mwenda zake alijaribu kuwa maingizo mapya mawili kwenye mifumo ambao huko nyuma nafasi hizo zilikuwa za wanaume.
VP Samia S. Hassan 2015-2021 (Ambae kwa sasa ndie C in C)
Commissioner Gen. wa Uhamiaji Dr. Anna Makakala.

Nataka kuamini hao wawili niliowataja walifika pale kwa meritocracy na ika-happen pia kuwa ni wanawake.

USA ambao wamepata uhuru na wana idadi kubwa ya wanawake waliosoma ila mpaka sasa ni nchi ya 70 kwa kiwango cha uwakilishi wa akina mama bungeni.

Tunawatakia kila la heri akina mama ambao baadhi yao ni mama zetu, shangazi zetu, dada zetu, wake zetu, wanetu kwenye majukumu ya kuteuliwa na mamlaka kutumikia Watanzania.

Rai yangu kwa mamlaka ya uteuzi ni namna gani akina mama kama ambavyo wanaume au vijana wanatakiwa kuteuliwa washike nafasi by merits na sio kubebwa.
Na kwa muktadha wa sasa asiwe mtu kwa sababu ya CV (educational achievement) ila mtu mwenye uwezo wa ku-push the bounds na kufanya mambo yatokee.

Tanzania inapakana na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Zambia, Malawi na Mozambique; Baharini tuna nchi kama Comoro, Madagascar, Seychelles na Mauritius.
Tuna muono gani kulifikia hilo soko kwa mahitaji ya msingi kama chai, kahawa, korosho, cocoa, nyama, samaki, maziwa, nguo za kuvaa au vitambaa?

Tumezungukwa na nchi zenye watu wengi sana, nadhani wateule wa Mhe. Rais waje na akili zenye kuleta suluhisho linalowezekana, ni namna gani tukiamua kuuza hata biscuits nchini Comoro toka Tanzania zifike kwa haraka kwa bei nafuu kuliko Dubai?

Juzi nimenunua cornflakes, kuchungulia nikaona made in Libya; yaani linchi looote hili yet tuna import cornflakes?

It high time akina mama, wanaume, vijana wa kike kwa kiume ambao mtateuliwa na mamlaka za uteuzi mje na solutions zenye kuzalisha ajira, kuongeza exports, kuongeza tax base, kupunguza imports.

Kila la kheri tena Mama Samia Suhuhu Hassan Rais wa JMT kwenye kulijenga Taifa na kutekeleza kwa vitendo 50/50.
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,448
2,000
Kuteua mtu kwasababu ya Jinsia, dini, mkoa, kanda, pande za Muungano haijawahi kuwa suluhisho kwa matatizo yoyote.

Mfano mimi Mama yangu yuko kijijini, hata Rais Samia akisema ateue wanawake tupu hilo litamsaidia nini ?

Hata akisema ateue mtu wa dini atamsaidia nini ?

Matatizo makubwa ya nchi hii siyo teuzi. Teuzi ni njia tu za kugawana keki ya taifa kitu ambacho hakina faida kwa wengi.

Anyway, Mwisho wa siku watu watakuja kuangalia matokeo ya utawala wako tu bila kujali uliteua kina nani.

Wakati huo watu watakuwa wanaongelea matatizo ya MAJI, AJIRA, BIASHARA, MIUNDOMBINU, SHULE, AFYA, MALAZI, HAKI, USALAMA. Hakuna atayekumbuka kuwa uliteua watu fulani.
Huyu rais wetu ananifanya nimkumbuke yule mama aliyekuwa anaitwa Ananilea Nkya. Kila kitu alitaka kibadilike kesho yake. Nimekumbuka na kulazimishwa kuukubali ushoga kunakofanywa na nchi za magharibi. Rais naye anataka kuibadilisha society mechanically.

Hata kama unachopambana nacho ni kibaya sana, lakini socially hujaweza wageuza watu, itakuwa vigumu sana kufanikiwa. Rais kaja na hadithi za NGO na UN. Huko huko na walioendelea kama US bado hilo ni tatizo ingawa wanasema nasi tukubali mashoga. Muacheni awapendelee wanawake wenzake aliofanya nao kazi maana nina hakika hakuna mama wa kijijini atakayefaidika na mfumo wake.
 
GEMBESON

JF-Expert Member
Apr 15, 2012
1,167
2,000
Hii staili ya 50/50 mimi naiona ni zao la kutengeneza mfumo wa ubaguzi tu kwa watoto wa kiume.

Kwenye masuala ya uongozi wangefanya uteuzi kwa kuangalia Taaluma, uwezo na sifa za mlengwa hata kama wanawake ni 80% ni sawa tu ila sio kuinadi hii kaulimbiu ya kibaguzi
 
WALOLA VUNZYA

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
663
1,000
Ulinganifu hauwezi kuletwa na rais. Samia anatakiwa aelewe amefikaje hapo na ajiulize je, angejaribu kuomba urais wa Z’bar angeupata? Sasa anaanza kulazimisha kabla ya kuondoa mfumo na vikwazo vilivyo mbele ya wanawake. Tunajua atawateua lakini watatuangusha. Tunawaona bado wakifundishwa uvaaji wa heshima, siyo kwamba hawajui, bali wanahangika kuwavutia wanaume.

Hatua iliyo bora ni hiyo ya kuanzisha shule za wasichana za boarding, siyo kila mkoa, iwe ni kila Wilaya. Haya mengine unayoita 50/50 yataishia kuwachagua marafiki zako wa huko kwenye NGO tu na watakuja na mavazi yao ya kuiga u-zungu u-zungu wakiamini ndo maendelao.
Hiyo hamsini hamsini ni jipu kwa ustawi wa nchi.
 
balibabambonahi

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
9,952
2,000
Ulinganifu hauwezi kuletwa na rais. Samia anatakiwa aelewe amefikaje hapo na ajiulize je, angejaribu kuomba urais wa Z’bar angeupata? Sasa anaanza kulazimisha kabla ya kuondoa mfumo na vikwazo vilivyo mbele ya wanawake. Tunajua atawateua lakini watatuangusha. Tunawaona bado wakifundishwa uvaaji wa heshima, siyo kwamba hawajui, bali wanahangika kuwavutia wanaume.

Hatua iliyo bora ni hiyo ya kuanzisha shule za wasichana za boarding, siyo kila mkoa, iwe ni kila Wilaya. Haya mengine unayoita 50/50 yataishia kuwachagua marafiki zako wa huko kwenye NGO tu na watakuja na mavazi yao ya kuiga u-zungu u-zungu wakiamini ndo maendelao.
Angetafuta namna ya kubadili mindset ya walio wengi ambao wako kwenye kupiga picha na kutingisha makalio mitandaoni.
 
muyovozi

JF-Expert Member
Dec 28, 2017
468
1,000
Katika vitu ambavyo mhe. Rais Samia ameanza vibaya mno ni hiyo ya 50/50. Atakuja kusimulia jinsi ambavyo alikosea atakapoacha urais. Anatenda kana kwamba bado ni mwanaharakati katika NGO enzi ziilee!!! akiwa bado hajavaa mkitandio akiwa kwenye makongamano, warsha nk. Juzi nimeshangaa mhe . Mulamula hawezi kusoma figure za bajeti za wizara yake, sasa mtu hata figure za trilioni na bilioni na mama ya mamilioni hawezi kuyasoma huyu I doubt ni shoga yake aliwahi kumkarimu huko majuu N. York kwenye harakati za kusave per diem alipoenda kwenye mikutano nadhani. Practically katika viongozi bora wa miaka ya 1980's kule uingereza alitokea mama Margaret Thatcher ambaye alikuwa waziri mkuu aliyeongoza kwa miaka 12 mfululizo na hamna mwenye rekodi hiyo siku za karibuni nchi ile. Thatcher hakuteua mwanamke hata mmoja kwenye baraza la mawaziri. Waandishi walimtania kuwa baraza lake lina mwanaume mmoja na wanawake waliobakki(vice versa). Sikuelewa mantiki yake lakini mwanamke mpaka awe efficient lazima jukumu la maumbile (kuzaa) lazima asacrifice. Hata mama Samia kama usingekuwa ushabiki wa gender balance urais wa kupambania kama JMKkikwete angeusikia kwenye bomba. Sasa kama amefika pale halafu anataka awainue kina mama wote ni Kazi hatoiseza. Kea kipindi chake atawawezesha hatukatai lakini bass yake maji yatafind it's own level. Hivi anataka ashindane na Kagame kwa hilo ,wakati mwenzie kule anakwepa influence ya wanaume kwenye jamii. Hatukatai wanaweza wakawa hata 41 kwa 59 , lakini kumlazimisha 50/50 hapana mhe Samia hiyo crusade ni false start. Katika vitu ambavyo anavipigania na vitaleta athari(legacy) mbaya kwake ni viwili(1)gender balance(2)usawa wa Tanganyika na Zanzibar. Haya ajiandae watu kudai serikali ya Tanganyika chini ya utawala wake. Fikiria mtu kama Warioba aliwahi kutamka wazi kuwa muungano hauna faida yoyote ila kwa wakubwa juu kugawana vyeo. Hii ilfanya Nyerere asimuunge mkono Warioba kuwania urais 1995, akamwambia asubiri serikali ya Tanganyika ndio anaweza kuwa Rais. Kwa hiyo muungano na usawa kijinsia ni mambo sensitive sana yanatakiwa handling ya tahadhari mno sio kea sweeping statement za sasa. Mengine anatenda vizuri tu hadi leo.Rais Samia anaweza kuwa Rais bora tangu tupate uhuru kwani ni kudra za Mungu kaipata ile nafasi ,hana deni na mtu kufika pale. Afanye maamuzi sahihi tu basi. Biasness aache kwa kundi lolote atafanikiwa.
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,448
2,000
Niliwasikiliza wakati akiongea nao hapo Dodoma. Ni kama walikwenda ili kuwazomea wanaume. Wengine walipohojiwa baada ya mkutano, ilikuwa ni mashindano ya kuzungumza kama mwingereza, na kupinda ulimi saaana!

Bungeni viti maalumu/upendeleo havijawahi msaidia mwanamke wa kijijini, badala yake vinawasaidia walioteuliwa tu na wanajiunga na kundi la wanaume kufanya mambo yao. Samia, mama! Elimisha wanawake; Jenga shule nzuri za boarding kwa kila wilaya. Achana na 50/50 ambayo haina msingi. Lakini kama unataka marafiki zako nao wale pesa za taifa hili endelea na ahadi hizo. wateue na baada ya miaka mitano utathibitisha wanawake mzigo uliowabeba.
Yes! Hilo ndo tatizo. Wanashangilia kabla hata hawajaona mafanikio ya uongozi bora. Kwa kuwa tu ni wanawake, wanashangilia. Kama ulivyoeleza hakuna kilicho hovyo kama aina ya wananwake walioalikwa. Kweli mtu anahojiwa, majawabu yanakuwa ni maringo ya kuchanganya kiingereza kingi, na maneno ya kiswahili yaliyoharibiwa, yakitamkwa utadhani ni mwingereza!

Maigizo kama hayo yanatufanya tuwaone hawako serious na maisha yao. Na hao ndo waliopelekwa Dodoma kwamba wanaweza. Nchi ya majaribio na kuwagawia pesa za serikali kwa kisingizio cha empowerment!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom