Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,698
- 4,693
UKweli ni kwamba kama ni kuhongwa madaraka, wakati wa Kikwete walihongwa. Wako wapi? Nani aliyeweza kuonesha umahili wake? Bungeni nilimuona Anna Makinda akionesha ukomavu Wengine ni hoi tu wakaanza hata kupigana vijembe; Mara Ghasia anasema hivi, Mhagama anasema vile! Hooovyo!Katika vitu ambavyo mhe. Rais Samia ameanza vibaya mno ni hiyo ya 50/50. Atakuja kusimulia jinsi ambavyo alikosea atakapoacha urais. Anatenda kana kwamba bado ni mwanaharakati katika NGO enzi ziilee!!! akiwa bado hajavaa mkitandio akiwa kwenye makongamano, warsha nk. Juzi nimeshangaa mhe . Mulamula hawezi kusoma figure za bajeti za wizara yake, sasa mtu hata figure za trilioni na bilioni na mama ya mamilioni hawezi kuyasoma huyu I doubt ni shoga yake aliwahi kumkarimu huko majuu N. York kwenye harakati za kusave per diem alipoenda kwenye mikutano nadhani. Practically katika viongozi bora wa miaka ya 1980's kule uingereza alitokea mama Margaret Thatcher ambaye alikuwa waziri mkuu aliyeongoza kwa miaka 12 mfululizo na hamna mwenye rekodi hiyo siku za karibuni nchi ile. Thatcher hakuteua mwanamke hata mmoja kwenye baraza la mawaziri. Waandishi walimtania kuwa baraza lake lina mwanaume mmoja na wanawake waliobakki(vice versa). Sikuelewa mantiki yake lakini mwanamke mpaka awe efficient lazima jukumu la maumbile (kuzaa) lazima asacrifice. Hata mama Samia kama usingekuwa ushabiki wa gender balance urais wa kupambania kama JMKkikwete angeusikia kwenye bomba. Sasa kama amefika pale halafu anataka awainue kina mama wote ni Kazi hatoiseza. Kea kipindi chake atawawezesha hatukatai lakini bass yake maji yatafind it's own level. Hivi anataka ashindane na Kagame kwa hilo ,wakati mwenzie kule anakwepa influence ya wanaume kwenye jamii. Hatukatai wanaweza wakawa hata 41 kwa 59 , lakini kumlazimisha 50/50 hapana mhe Samia hiyo crusade ni false start. Katika vitu ambavyo anavipigania na vitaleta athari(legacy) mbaya kwake ni viwili(1)gender balance(2)usawa wa Tanganyika na Zanzibar. Haya ajiandae watu kudai serikali ya Tanganyika chini ya utawala wake. Fikiria mtu kama Warioba aliwahi kutamka wazi kuwa muungano hauna faida yoyote ila kwa wakubwa juu kugawana vyeo. Hii ilfanya Nyerere asimuunge mkono Warioba kuwania urais 1995, akamwambia asubiri serikali ya Tanganyika ndio anaweza kuwa Rais. Kwa hiyo muungano na usawa kijinsia ni mambo sensitive sana yanatakiwa handling ya tahadhari mno sio kea sweeping statement za sasa. Mengine anatenda vizuri tu hadi leo.Rais Samia anaweza kuwa Rais bora tangu tupate uhuru kwani ni kudra za Mungu kaipata ile nafasi ,hana deni na mtu kufika pale. Afanye maamuzi sahihi tu basi. Biasness aache kwa kundi lolote atafanikiwa.
Ukiwasikia wazoefu akina Mongela ambao nao walibebwa kwa miaka mingi, sasa wanazungumzia minyoo na kufundisha watu kutongoza! Hawa!