4X4=18, Taarifa ya habari ITv

Sishangai hata kidogo!kwa vitabu alivyotolea mfano Mh.Mbatia ambavyo ndivyo nadhani kavisoma huyu kisura,unatarajia asemeje?Tena kajitahidi sana kwani jawabu linakaribiana na ukweli yaani tofauti ya 2 tu siyo issue!Je angesema 4X4=44?Tuwashangae wale waliotoa ithibati ya vitabu alivyovitolea mf Mh.Mbatia kwani wanawapoteza watoto wetu.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Ah!!!! Yuko sawa . Hiyo Ni mbinu mojawapo ya kukufanya ukumbuke Na kuzingatia zaidi.
 
Kitu cha ukwee. Huyo ukikutana naye kwenye interview, kidume lazma upigwe chini.
 
kwa kweli hata taarifa hizo siangalii tena
nshajichokea mie.
 
Tutofautishe facebook na JF ,sisi ni muhimu sana kwa taifa.

Sent from cm ya wife using JamiiForums
 
Halafu ni taarifa aliyokuwa ameiandaa na alikuwa anaisoma......Inaonesha hali halisi ya mambo yanavyokwenda nchi hii...UKANJANJA TUUU
 

mkuu, hata wewe sentensi ya kwanza ya uzi huu mwishoni ulitakiwa kuweka alama ya kuuliza (?) badala ya nukta. makosa ni kawaida na ndo maana huwa tuna edit pengine hata yeye angeweka kauli yake kimaandishi angeona hilo kosa.
 
Hata mi nilimwona, labda kama angepata nafasi ya kujitetea angesema ulimi uliteleza kama Mulugo maana hauna mfupa!
 

co kila lisemwalo ni kweli,tafakari na ulinganishe na mazingira husika yaliyotumika
 
ahsante meneja muajiri (mtoa ajira) katika kampuni hiyo ametudhihirishia wazi kuwa watumishi wake hawana sifa za kitaaluma ila kuna somthing behind the pazia. Hahahahaha, 4x4 = 18 sijui ni hesabu za nchi gani hizi.

Halafu mdada huyo alikuwa anaongea kwa mapozi utadhani ndio anajifunza kiswahili. La professerrrrrrrrrr
 
Huu ndio umbea, kuna binadamu asiekosea? Uivu wa kijinga/

Hapo hakuna wivu, ile taarifa aliihariri kabla ya kuisoma na hakugundua tatizo na kama ni typing error kwa herufi inakubalika na siyo kwenye hesabu, kama unajuwa hesabu utakaporudia nafsi itakataa tu kwamba hili siyo jibu lake mwandishi alikosea, utasahihisha, anyway nyie si mnasema hata ukipata alama F ya hesabu haina madhara kwa kuwa anaenda kusoma HGL aendelee tu, matokeo yake ndiyo hayo, hamjuwi kuwa hesabu ni cross cutting.
 
haya ni maoni yako na huzuiwi kua na uivu wa kijinga, maana ndio wangine wakiwezacho. Lakini wene weledi wanafahamu kua si ajabu mwanadamu kukosea. Pia kukosea kwa kurudia si dalili ya kutojua hesabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…