4X4=18, Taarifa ya habari ITv

4X4=18, Taarifa ya habari ITv

Je haya ndiyo matokeo ya elimu aliyosema Mbatia.
Usiku huu kwenye taarifa ha habari ITV kuna dada mmoja alikuwa anaongelea kuhusu gazeti la the gurdian na Nipashe kuzindua huduma ya yaarifa kwa njia ya sms kupitia tigo kasema mteja atakuwa anapokea msg nne kwa mpigo mara nne akakazia kwamba nne mara nne ni kumi na nane.

Huyo atakua alisoma elimu ya MEMKWA kama sio UPE!!
 
Je haya ndiyo matokeo ya elimu aliyosema Mbatia.
Usiku huu kwenye taarifa ha habari ITV kuna dada mmoja alikuwa anaongelea kuhusu gazeti la the gurdian na Nipashe kuzindua huduma ya yaarifa kwa njia ya sms kupitia tigo kasema mteja atakuwa anapokea msg nne kwa mpigo mara nne akakazia kwamba nne mara nne ni kumi na nane.
Mmh kwani jamani 4x4 sio 18? Au na mimi sijui hesabu? MAGAZIJUTO!
 
nimependa sana...unajua sisi watanzania ni wabunifu sana ni kitu cha kujivunia mno
 
Watangazaji wengi wa redio na TV zetu wanafanya silly mistakes. Sijui huwa hawaoni TV kama Sky, CNN, BBC au hata CITIZEN! Wanashindwa hata kuiga Dira ya Dunia ya kina Kikeke dakika 30 tu lakini unapata maelfu ya habari za kukufanya usikose kipindi.
 
Kuna misemo mingi sana inayotuasa au kutuonya tusifanye jambo kabla ya kutafakari. Ni nani aliye mkamilifu kati ya wanadamu? Hakuna! Msemo "Learning Through Mistakes" au kujifunza kutokana na makosa unatoa picha kamili ya kuwa mwanadamu kama mwanafunzi,hujifunza kutokana na makosa yanayomkabili katika maisha yake ya kila siku!

Wa Kusoma,hata wewe uzi wako una makosa katika baadhi ya maneno uliyoandika! Kwa mfano badala ya kuandika taarifa umeandika yaarifa, badala ya kuandika taarifa ya umeandika taarifa ha! Panapotakiwa kuwekwa herufi kubwa umeweka herufi ndogo! Nafikiri ulitakiwa kuandika The Guardian na siyo the guardian,kitu ambacho ni kosa japo maana ni ile ile!

Hata wadau wengine waliochangia uzi huu wamefanya makosa yale yale yanayotokea na kufanywa na watu mara nyingi tu katika uandishi! Kuna maneno ambayo yakikosewa kidogo tu wakati wa kuyaandika huleta maana mbaya kwa msomaji au wasomaji. Hivyo basi ni vyema na haki tukaelimishana na siyo kukashifiana.
 
Acheni udhaifu kutafuta kasoro kwa wenzenu,mwengine anapokosea chukua hilo kwa manufaa yako, si ajabu wewe unafanya makosa zaidi ya huyo aliyekosea pengine kwa bahati mbaya. We are bound to do mistake.
Tatizo siku hizi watu wengi wanasomewa, wao kuchabo tuuu ndio haya yanatokea kazini.mtangazaji mwingine leo huko Morogoro kasema;MWANZO WA NGOMA NI LELEMAMA!!! mashaka, tunako elekea balaa.
 
haya ni maoni yako na huzuiwi kua na uivu wa kijinga, maana ndio wangine wakiwezacho. Lakini wene weledi wanafahamu kua si ajabu mwanadamu kukosea. Pia kukosea kwa kurudia si dalili ya kutojua hesabu.
siyo maoni yangu bali hiyo ni fact kama hutaki sikushikii fimbo, werevu wamenielewa, nimefikisha ujumbe nimetimiza wajibu wangu.
 
Back
Top Bottom