45% ya Wanawake wenye Ajira wametoa Rushwa ya Ngono! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

45% ya Wanawake wenye Ajira wametoa Rushwa ya Ngono!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by fangfangjt, Mar 17, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  ?45% wanawake, wasichana wamepata kazi kwa ngono?


  Wednesday, 16 March 2011 20:36


  Nora Damian
  ZAIDI ya asilimia 45 ya wanawake na wasichana walioajiriwa kwenye ofisi mbalimbali nchini, zikiwamo za serikali walipata ajira hizo baada ya kutoa rushwa ya ngono, imeelezwa.

  Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Asasi ya Ushauri Nasaha na Maisha ya Familia (CAFLO), Mariam Mlugu, kwenye mafunzo kwa viongozi wa serikali za mitaa kuhusu unyanyasaji wanawake na wasichana katika familia.

  Mlugu alisema hali ya unyanyasaji wa mwanamke imekuwa ikiongezeka kila siku, hasa ngazi ya familia na kaya, kazini na maofisini.“Wengi wa wanawake na wasichana, wamekuwa wakinyanyasika kingono ikiwamo kubakwa, kupigwa na kunyimwa haki ya kurithi mali na hata kuuawa,” alisema Mlugu.

  Alisema zipo sababu mbalimbali zinazowafanya wanawake kunyanyasika, kama kutofahamu haki za binadamu, mfumo dume, mawazo mgando, mila, desturi na wanawake kutotambua nafasi na majukumu yao kwenye familia.

  Pia, Mlugu alisema unyanyasaji wanawake na wasichana haupo Tanzania peke yake, kwani ni tatizo ambalo limeenea sehemu nyingi duniani na kutolea mfano Afrika Kusini kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, wastani wa wanawake watatu walikuwa wakibakwa kila baada ya dakika 90.

  Mwenyekiti huyo alisema unyanyasaji mwanamke unaleta madhara makubwa kwenye familia na jamii, kama kushuka kwa kasi ya maendeleo, kuongezeka kwa umaskini, kupotea kwa hadhi na thamani ya utu wa mwanamke.
  Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, madhara mengine ni kusambaratika kwa familia, kuongezeka kwa matatizo kama Ukimwi, vifo na watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.

  Nao viongozi wa serikali za mitaa walioshiriki mafunzo hayo, ambao wanatoka kata za Buguruni na Vingunguti, waliaswa kuwa na mikakati mahsusi ya kutokomeza unyanyasaji huo, kwani wao ni wadau wakubwa wa mapambano hayo.

  Pia, viongozi hao walitakiwa kuimarisha mabaraza ya usuluhishi kwa kuwawezesha wadau, kupata mbinu sahihi na utaalamu wa kutatua kesi mbalimbali zinazoletwa kwenye mabaraza yao.Mlugo aliwataka wanaume kutumia nafasi zao kuleta maendeleo ndani ya familia, bila kubagua wanawake kwani wakipewa fursa wanaweza kuleta mabadiliko ya familia na taifa.
   
 2. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wametumia kiungo chao, wewe inakuuma nini? Tumia na wewe cha kwako upate ajira nzuri zaidi ya hizo walizopata wao.
   
 3. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli hii ni changamoto kwa dada zetu wanaotoka vyuoni. Na ukilitizama hili suala kwa mapana huu unyanyasaji utendelea kwa muda mrefu kwa kuzingatia huu ufinyu wa utengenezwaji wa ajira katika nchi yetu na utaratibu mbovu wa
  kupata wafanyakazi kwa kujuana kutozingatia vigevyo, lakini nina mifano michache hai ya dada zetu nao kuwa na hii kasumba ya kujilahisisha ili apate ajira.wito kwa dada zangu jitahidini kusimama ili muweze kupata kazi kihalali ni sawa tunajua maisha magumu ila mikiendelea na nyie kujirahisi mnategemea nini?
   
 4. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  mkuu kweli are you great thinker i ?au ndo huu mtazamo tu.mhhhh
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hivi hakuna wanaume waliopata kazi kwa ngono??
   
 6. F

  FUSO JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,339
  Trophy Points: 280
  I hope my wife to be is not among those...
   
 7. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Suala hili lina pande mbili. Mara nyingi tunapozungumzia rushwa, tunaangalia mla rushwa peke yake. Hatuangalii mto rushwa naye.

  Upande wa kwanza ndo huo wa unyanyasaji na mfumo dume unaowafanya wanaume walioko kwenye position of power wajione kuwa wana haki ya kufanya chochote dhidi ya watu wanaotafuta favour zao. Hii ina maana kuwa hata wanaume wengi walioko makazini (hasa serikalini) walilazimika kutoa rushwa ingawa wao rushwa yao ni ya kifedha hapa unyanyasaji hausemwi sana.

  Upande wa pili ni wa baadhi ya wanawake kuamini kuwa miili yao inawapa "negotiation power" na kuwa wanaweza kuitumia miili yao kupata wanachokitaka. Hawa wanapoona wameshindwa kwa njia ya kawaida "kujiachia" ndo inakuwa njia yao nyingine. Kama vile vile wanaume wanavyotumia ushawishi wa kutoa rushwa wanapoona kuwa hawawezi kupata kwa njia ya kawaida.

  Kwa hiyo tatizo kubwa hapa ni ufisadi au corruption. Ukiondoa ufisadi umetibu magonjwa mengi ambayo kusema kweli ni magonjwa nyemelezi tu. Ukimwi wenyewe ni ufisadi.
   
 8. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Tatizo wanawake wenyewe wengi wao hawalioni hilo kama ni unyanyasaji! Ukiwauliza wanakwambia 'its all about positioning yourself strategically'
   
 9. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  mkuu hili nalo neno dada zetu wanatia sana hasira kwenye hili. Hizi haki wanazozitaka kwanini wasiwe wa kwanza kujitendea haki kwa kutojidhalilisha
   
 10. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kulingana na matokeo ya utafiti uliofanywa na shirika moja la kujitegemea hapa nchini, unaonyesha asilimia takriban arobain (40%) ya wanawake walio na ajira rasmi wamezipata kazi hizo kwa kutoa au kulazimishwa Rushwa ya ngono.
  Ndugu wanaJF kwangu hizi habari nimezipokea kwa masikitiko, nawashangaa dada zangu kwa kujirahisisha kiasi icho ukizingatia kuwa wengi wao wanavigezo na ni wasomi wa viwango vya juu kielimu, nawalaumu kwa kushindwa kujithamin kiasi cha kutoa mapenz kwa nia ya kupata kazi, huku ni kujishushia thamani ya utu wao.
  Kwa upande mwingine napenda washauri wanasheria pamoja na maafisa utumishi wote kuja na mbinu au mkakati utakaowezesha kuwabaini maafisa kazi wote waombao rushwa hizi za ngono, pia wawachukulie hatua kali za kinidhamu. PCCB PIA WANAHUSIKA KTK UFUMBUZI WA TATIZO HILI.
  Ndugu wanaJF nawasilisha!
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  imebidi nicheke sana......
   
 12. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wanawake wengine anatumia hiyo kama chombo cha kufaulu kwenye interview kwani hata huko vyuoni walifaulu kwa kugawa ngono.
   
 13. s

  salisalum JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Nilidhani hili jambo ni serious na halina utani. Mbona unajibu hivo ndugu yangu? Maana yake kila wanawake 10 walio na ajira karibu watano walipata hizo ajiri kwa kutoa mwili wao kama rushwa. Hii inaweza kuhusisha dada yako, mke wako, shemeji yako, au mchumba wako ambaye unataraji kumuuoa hivi karibuni atakapokuwa confirmed pale kazini kwao.

  Huu ni udhaifu wa wanaume, tukiri tu wazi. Mzaha unaoufanya kwenye jambo nyeti kijamii linaonyesha kwa namna fulani au unafurahishwa na vitendo hivyo au ni mdau. Tuwalinde wanaweke, kama tukitaka ngono tusitumie advantage zetu na shida zao. Hii imezidi na inaudhi sana wanaume kujidai wana nguvu kumbe ni dhaifu wa kutupwa.
   
 14. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #14
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  suala hili limeanzia kwenye ngazi ya chuo kwani kuna degree cha chupi.wasichana wanajirahisi kwa wahadhiri ili kufanikisha masomo.
  huu utafiti umeangalia matawi badala ya mzizi wa tatizo.naomba kujua baada ya utafiti huu hiyo taasisi inajiandaa kufanya nini? au ndio kazi imeishia hapo.
  na nafasi ya wasichana i wapi ktk hili kwani wao hata hawashangai na wanakebehi wavulana waliokosa ajira kuwa watakoma kuzaliwa wanaume.
  nashauri wakafanye tafiti ziwezazo leta tija kwa maendeleo ya wananchi kwani hapo wanazungumzia walio na ajira badala ya kuangalia wasio kuwa nazo na njia ya kuwasaidia
   
 15. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  sophia simba naye alitoa uroda kupata kazi,iam sure,atleast from her stupid errotic statements
   
 16. c

  carefree JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  wako wengi hata hapa ofisini kwetu yupo alimdo HR akaletwa tuko naye hana ajualo na wala hataki kujifunza
   
 17. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  eeh hatari hapa mkuu wa bunge letu kapona kweli? na hawa wakuu wa wilaya inamaana na wenyewe wapo wanaovua nguo!
   
 18. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Kwa upande mwingine hii takwimu ya kuwa 'karibu' nusu ya waajiriwa wanawake wametoa rushwa ya ngono naona kama inawaeleza wanawake wasioajiriwa au walio vyuoni kuwa 'ajira' kwa kiasi kikubwa zinapatikana baada ya kuhonga ngono...na hivyo kuwaandaa 'kiasikolojia' kutoa hongo hiyo!

  Ni mtazamo wangu tu...
   
 19. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama Degree uliipata kwa kutoa ngono basi na kazi itakuwa hivyo hivyo matokeo yyake unapata kazi lakini kazi yenyewe hujui.

  Aibu kubwa
   
 20. K

  Kamongo JF-Expert Member

  #20
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  idara za serikali kwenye tabia hizo ni polisi,mahakama ....etc kumeoza
   
Loading...