21st to remember. Tarehe 21 ya kukumbukwa.. A count down!

21st to remember. Tarehe 21 ya kukumbukwa.. A count down!

mtu mzima mwenye heshima, familia na wajibu halali wa kujipatia kipata kamwe hawez kubebwa ufala wa kifikra na kupumbazwa na msukule mpotoshaji kama hamprhey polepole

hicho ni kiwango kibaya sana cha umaskini wa kifikra 🐒
Ww ni yule wa kuyamba yamba
 
Angalieni Linconmedia mda huu ashaanza kuongea tayari
slow slow kaingia mitini, hizo unazoziona sasa ni wadau wanarudia za zamani wanazirusha live.

huyu ni tapeli sijui atakuja na kisingizio gani
 
no, si mimi gentleman,
bali mimi ni alfa na omega, mwanzo na mwisho katika kuchambua, kufafanua na kutafiti masuala mballimbali ya kisiasa humu nchini 🐒
514d93c2-4a7a-49ad-b3da-c671ff860fd6.jpeg
 
Bwana Humphrey Polepole keshatuandaa vema kumsikiliza leo tar 21. O8. 2025.. Ni tangazo lenye hamasa kwamba litatokea jambo kubwa.. Kwa maneno yake ya siku za nyuma aliwahi kusema wasipomsikiliza basi ataongea ambayo hawatapenda kuyasikia

Kwa tafsiri ya haraka ni kwamba leo tarehe 21. O8.2025 ndio inaweza kuwa siku ya kuizika rasmi CCM ama kuimalizia kabisa kutokana na yale atakayo yaongea
Je ataongea nini? Kuweka ramli chonganishi pembeni ataongea yaleyale ambayo siku zote yaliongelewa chini ya zulia ama kwa sauti ya China
Ataongea yaleyale ambayo hakuna chombo cha habari kilithubutu kuyaandika
Ataongea yale ambayo ccm iliyafanya kushinda chaguzi
Ataongea kuhusu mtandao ndani ya ccm, ambao ndio unaamua nani awe nani kwenye nini
Naamini pia ataongea kuhusu utekaji na watekaji, nani alitekwa alipelekwa wapi na kama yuko hai ama mfu.. Na alikoenda kutupwa ama kuzikwa

Kwa kifupi ataongea mambo mabaya waliyofanyiwa watanganyika chini ya utawala wa ccm! Na kwa vyovyote hayatakuwa na afya kwa chama tawala
Kuna hofu na kuna kejeli pia.. Hofu kwamba nini kitatokea baada ya mazungumzo yake! Kwamba atasababisha mtikisiko mkubwa utakaomaliza enzi za wana mtandao
Kejeli kwamba hana jipya na hakuna kitakachotokea.. Na kwamba akishindwa leo atakuwa amepiga mweleka mkubwa sana na kulipa nguvu zaidi kundi la wana mtandao
Baada ya mazungumzo yake inaweza kujulikana sasa nguvu yake ama walio pamoja naye na nguvu yao.. Ameamua kujivika mabomu ambayo kama hayatalipuka.. Taifa litaingia kwenye ukiwa mkubwa lakini kaka yakilipuka na kukosa upinzani wa uharibifu ndio itakuwa mwanzo wa ukombozi wa Tanganyika!

Yamebaki masaa machache Polepole kutengeneza historia mpya ya shujaa wa Tanganyika!
Tar 21 inaweza kuwa siku kuu Tanganyika.. A day to remember..
Tar 21 August inaweza kuwa siku maarufu zaidi Tanganyika na ikapewa kila aina ya slogan ikiwemo ya A DAY WHEN EVERYTHING WENT WRONG!

Mwezi August ulitabiriwa na watabiri wengi kama mwezi wa mtikisiko mkubwa ndani ya ccm! Tuna utazamia kuuona ukitimia...

Ni leo saa 2 kamili usiku, muda ambao ni wa taarifa za habari macho na masikio yatakuwa kwa Polepole.. Je kuna uhusiano wa kiroho kuhusu hii tarehe na muda aliouchagua!? Wanajimu kwenye hesabu za namba watatuambia.. 21.08.2025 02:00

Kumbukeni Akimaliza Polepole leo tutakuwa na mapumziko ya siku mbili kisha atakuja Gwajima. Ambaye naye ameahidi kuongea mazito na makubwa
Tuupe muda wakati...


View: https://www.facebook.com/share/v/19cuV4g9Qc/

21st to forget. DJ katupeleka studio
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom