2026 FIFA World Cup - Special Thread

Messi katolewa lakini ukweli utabaki kwamba Ronaldo Hana world cup
Messi ingawa amekosa Kombe kwenye fainali hizi na hata kama atastaafu Anastahili sifa nyingi.
Ameufanyia mambo mengi mchezo wa soka.
Katika wachezaji wa zama hizo anastahili pongezi na sifa nyingi.
Sasa ni zamu ya akina Yamal, Pau Cubarsi nk
 
Messi hastahili kulia ukweli ni kuwa kwa fainali ya jana ilikuwa zaidi ya upande mmoja zaidi hawakustahili kushinda na ndo ilivyotokea, moja kati ya fainali mbaya za kombe la dunia za hivi karibuni, Argentina walikuwa hopeless at least zile 5 minutes za mwisho walionyesha uhai kidogo
 
Mbappe ameshinda Golden Boot na kumaliza akiwa mfungaji bora kwenye World Cup history.

Olise amemaliza kwa kuwa na rekodi ya mchezaji anayeongoza kwa assist nyingi kwenye historia ya kombe la dunia.

Rodri won the Golden Ball. What about your so called Goat ?

What's your GOAT achieved so far?

Argentina imekuwa timu ya kwanza kwenye historia ya miaka 96 ya World Cup kufika semi final bila kukutana na top 10 ranked team.

Argentina imemaliza kwa kufunga rekodi ya kupiga Penalty nyingi, kukosa penalti nyingi na kuwa mchezaji wa kwanza kukosa penalti mbili kwenye World Cup moja.

Rekodi nyingine pia aliwahi kuwa top scorer wa World Cup history kwa muda wa wiki moja.

 
Mimi ni shabiki halisi wa mpira japokua namkubali sana Messi, kwanza sikutarajia kwamba watafika fainal mana kikosi ndio kilekile cha 2022 kilichobeba kombe wameshachoka.

Ufaransa na Argentina tuzipe heshima yake tuache ushabiki

Ufaransa kabeba 2018 halafu karudi tena fainali 2022

Argentina kabeba 2022 karudi tena fainali 2026

Sio rahisi Mzee, Kuna timu hazijawahi kucheza hata fainali
 
Kbabakee goaaaaaaalllllqaaa hatimae messi anasawqzisha bao 1-1 [emoji91]
 
Hata Infantino hakutarajia ndio maana aliwaandalia njia nyepesi.

Wewe unafikiri ni kwa bahati mbaya Argentina iwe timu pekee kwenye miaka 96 ya World Cup kufika semi final bila kukutana na top 10 ranked?

Hivi unadhani yale ambayo tumekuwa tukiyalalamikia humu kuhusu favouritism ambayo Argentina na Messi wamekuwa wakiipata, ilikuwa ni maneno matupu yasiyokuwa na hoja?

Unadhani ni kwanini Laporta ambaye ni raisi wa Club ya Barcelona kabla ya mechi alisema Spain wana timu nzuri ya kushinda kuliko Argentina ila ikiwa tu mwamuzi atachezesha fair?

Hivi unafikiri ni bahati mbaya kwenye miaka 96 ya World Cup (kasoro minne iwe karne ) Messi kuwa na Penalty nyingi kuliko mchezaji yeyote na huku penati 4 akizipata kwenye single tournament??

Uliyemuona jana, yule ndio Messi ambaye sisi tumekuwa tukimjua siku zote na tukiwaambia mnakaza fuvu.

Stats za Messi jana ni sawa tu na zangu ambaye nilikuwa naangalia hiyo game maana sina on target, sina off target, sina dribbles, sina goli.

Kitu pekee kinacho nitofautisha nayeye ni kwamba, mwenzangu alikuwa hana hivyo vyote akiwa yupo uwanjani wakati mimi nikiwa kwenye kitanda.
 
Mbusi ya watu kiroporopo
View attachment 3633454
Alitaka kumchomea kwa refa Cocurella.

Kuna narrative ya kishamba ambayo mashabiki wake wamekuwa wakim praise Messi dhidi ya Ronaldo eti Messi ni humble.

I still don't get it, I mean how could a so called humble man be a snitch?
Your browser is not able to display this video.
 
Vijana WC imeeisha, hii wiki ikiisha turudi kwenye majukumu ya kujijenga kimaisha na taifa kwa ujumla. Hata aliyeanzisha huu uzi alilenga watu wafurahie kwa wakati huu mfupi maisha mengine yaendelee. Tusitumie muda mrefu kujadili mambo yaliyopita na yasiyo tuongezea pesa.
Tafuteni pesa muishi maisha ya raha bila stress.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…