2026 FIFA World Cup - Special Thread

Kuna watu ambao hawataki Argentina ichukue ubingwa.

Lionel Scaloni avunja ukimya kuhusu mjadala mzito unaoendelea kufuatia Argentina kushinda mechi yake dhidi ya Egypt.

Akizungumzia madai ya refarii kuwapendelea, Lionel amezidi kusisitiza kwamba kuna ajenda dhidi ya bingwa mtetezi imeundwa.

"Kuna kampeni imeundwa baadhi ya watu wamekuwa wakisema tunapata upendeleo wa muda mrefu. Labda hawataki kuona tunashinda kwasababu tumeshinda kombe lililopita.

Kuliko kuacha hizi kelele ziwatoe kwenye mchezo, Scaloni amesema watazitumia hizo kelele kama hamasa ya silaha ya

"Tutatumia ukosoaji na maoni ya watu kama motivation. Tutageuza hizo criticism kuwa nishati ya kuwafanya wachezaji wetu wapambane zaidi

Pia alipinga hizo nadharia kwa kuonesha ni kwa namna gani mfumo wa sasa wa refarii unavyofanya kazi.


🗣️"Siku hizi kuna VAR, ni ngumu kwa mtu yeyote kukubeba. Kila kitu kinakuzwa kwenye mitandao ya kijamii lakini katika uhalisia hakuna favouritism.🙅‍♂️📺
 
Romain Molina ametangaza kufanya uchunguzi mkubwa wa kile alichokiita "umafia wa mpira wa Argentina"

Sehemu ambayo nioo interested nayo ni hapo alipoitaja FIFA.

Huyu jamaa aliwahi ku expose mambo mengi ikiwemo sexual abuse kwenye shirikisho la mpira wa Hait na Gabon pamoja na corruption ambayo baadaye ili switch kwenda kwenye mahakama za judicial.

Moja ya reputation ya huyu mwamba aliyojijengea ni kufichua ukweli ambao watu wenye nguvu wanataka kuuzika.

Na wakati huo ukumbuke FBI bado nao wanamfanyia investigation Claudia Tapia raisi wa shirikisho la soka la Argentina kwa kashfa za utakatishaji pesa wa zaidi ya $57M.

Sijui Romain ana ushahidi gani ila najua hajakurupuka ukicheki kawa mention FIFA directly, hiyo ni defamation tayari kama hana ushahidi.

Let's see
 
Wameamua kucheza nje ya uwanja hao maana dimbani La Pulga anapiga utosini tu....
 
Yaani huwa nashangaa haters kwa kusema Messi anabebwa. Yaani wanafikiri uwezo alionao ni mdogo.

Wanaabudu uwezo mkubwa wa CR7.Alafu angalia Ronaldo kamzidi nini Messi zaidi ya umri,mechi nyingi,na magoli 57 kwenye tofauti ya mechi 130+
Na UEFA 1

Yaani ubebwe na FIFA kwenye career yako na FIFA wakupe magoli 920+, Huna uwezo hata kidogo, Ballon D'or 8 bila kuonyesha chochote uwanjani. Uongoze tuzo za ufungaji bora Bara la ulaya na haujui lolote.

World cup under 20 na World cup 2022 zote upewe wewe tu bila kuwa na uwezo wowote.

Wivu ukizidi unakuwa uchawi. Kam hizo data zote ni za kuoewa na FIFA naamini Messi ana uwezo mdogo sana na CR7 ni bora zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…