Mm napenda ball
sio shabiki wa mtu
Argentina alibebwa tukio gani
Okay twende taratibu.
Nataka hapa tufanye reasoning huku tukirejea baadhi ya sheria za mpira ili tuone kama hoja ya kwamba Argentina alibebwa ina mashiko au la.
Kuna sheria inaitwa "Denying a goal or an obvious goal-scoring opportunity (DOGSO)"
Sheria hii inazungumzia faulo iliyochezwa dhidi ya mpinzani aliyekuwa katika nafasi ya kufunga goli. Sheria hii mara nyingi huwa inapimwa zaidi pale ambapo beki anakuwa ni mtu wa mwisho.
Adhabu ya kosa hili ni kadi nyekundu.
Na reference ya karibu, ni kwenye mechi ya Mexico Vs South Africa.
Sithole anatolewa nje kwa kadi nyekundu.
Sio tukio hilo peke yake lililoamuliwa kwa red card.
Mechi kati ya Iraq na Senegal, mchezaji wa Iraq anayeitwa Rebin Sulaka alitolewa kwa kadi nyekundu kwa kosa hilo hilo nililoweka kifungu chake hapo juu.
Mechi kati ya Belgium Vs Iran, mchezaji wa ubelgiji Nathan Ngoy alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Sasa kwanini nimekuonesha hizo clips zinazozungumzia faulo moja?
World Cup ya 2022 kwenye final kulikuwa na tukio kama hili.
Hapa ni mchezaji wa Argentina Nicolaus Otamend akimchezea faulo Kolo Muani kwenye penalty box
Unaweza kuangalia hii clip kwa kujiridhisha zaidi
Hiyo ni faulo ambayo iliamuliwa kwa mkwaju wa penati lakini hakuna kadi nyekundu iliyotolewa kwa Otamend licha ya kwamba yeye ndio alikuwa mtu wa mwisho na hakugusa mpira alimgonga Kolo Muani na goti lake.
Argentina wangekuwa down kwa 10 against 11 hii ilikuwa ni advantage wa France na pengine ingeweza kabisa kubadilisha momentum ya mechi.
Hiyo ni incident moja tu, ila zipo nyingi na references zake zipo. Nataka unipe maoni yako wewe unayesema huna mapenzi na timu yeyote ila unapenda mpira kama maamuzi yaliyotolewa hapo yalikuwa ni sahihi kutompa Otamend kadi nyekundu au hayakuwa sahihi.