2026 FIFA World Cup - Special Thread




Adidas Trionda.
Mpira utakaotumika World Cup.


Sifa kuu 4 za huu mpira.

1. Una Paneli 4 Tu: Ndio mpira wa kwanza wa Kombe la Dunia kuwa na paneli nne tu zilizounganishwa kwa joto. Hii inaufanya uwe duara kamili, upae vizuri hewani, na usinyonye maji yakivuja uwanjani.

2. Una Sensor ya Ndani (Chip): Una kifaa kidogo cha kiteknolojia ndani yake kinachotuma taarifa mara 500 kwa kila sekunde. Hii inasaidia marefa wa VAR kutambua offside na magoli kwa usahihi mkubwa.

3. Una Betri Inayochajiwa: Tofauti na mipira ya zamani, mpira huu una betri ndogo inayoweza kuchajiwa kabla ya mechi na inadumu kwa saa 6 uwanjani ili kuwasha sensor ya ndani.

4. Una Ngozi ya Grip (Mabonde): Juu ya ngozi yake kuna vishimo na michirizi midogo inayomsaidia mchezaji kuwahi kuudhibiti (control) na kipa kuudaka kwa urahisi hata kukiwa na mvua.
 
Technology imekuwa sana!!
 
Inatukumbusha Jabulani
 
Kiwanja kiko katikati ya mji.
 

Kwangu naona kama ni miongoni mwa viwanja vyenye mechi ngumu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…