2019 Africa Cup of Nations Special Thread

Observer

Senior Member
Oct 18, 2006
188
290
1130345


1130346


Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika inatazamiwa kuanza kutimua vumbi ijumaa tarehe 21/06/2019 kwa mechi kati ya wenyeji Egypt dhidi ya Zimbabwe

Michuano hiyo itahusisha mataifa 24 ambayo yamegawanywa katika makundi 6, kila kundi likiwa na timu 4

Tanzania imefanikiwa kufuzu kwenye mashindano hayo kwa mara ya pili katika historia yake, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1980 na imepangwa katika kundi C

Mara ya mwisho mashindano haya yalifanyika 2017 nchini Gabon ambapo Cameroon walifanikiwa kuchukua kombe baada ya kuifunga Egypt kwa magoli 2 -1 katika mechi ya fainali

Je nchi gani unaipa nafasi ya kuchukua kombe hilo?

Nini matumaini ya Tanzania kwenye mashindano hayo?

Tutakuwa tunatumia mada hii kuhabarishana tukielekea kwenye ufunguzi wa mashindano hayo, yanayojiri wakati wa mechi, matokeo na matukio yote yanayohusiana na mashindano hayo

UPDATES

Ratiba 21/06/2019: Egypt vs Zimbabwe

Matokeo: Egypt 1 - 0 Zimbabwe

Ratiba 22/06/2019: Congo vs Uganda | Nigeria vs Burundi | Guinea vs Madagascar

Matokeo: Congo 0 - 2 Uganda | Nigeria 1 - 0 Burundi | Guinea 2 - 2 Madagascar

Ratiba 23/06/2019: Morocco vs Namibia | Tanzania vs Senegal | Kenya vs Algeria

Matokeo: Morocco 1 - 0 Namibia | Tanzania 0 - 2 Senegal | Kenya 0 - 2 Algeria

Ratiba 24/06/2019: Ivory Coast vs South Africa | Tunisia vs Angola | Mali vs Mauritania

Matokeo: Ivory Coast 1 - 0 South Africa | Tunisia 1 - 1 Angola | Mali 4 - 1 Mauritania

Ratiba 25/06/2019: Cameroon vs Guinea Bissau | Ghana vs Benin

Matokeo: Cameroon 2 - 0 Guinea Bissau | Ghana 2 - 2 Benin

Ratiba 26/06/2019: Nigeria vs Guinea | Uganda vs Zimbabwe | Egypt vs Congo

Matokeo: Nigeria 1 - 0 Guinea | Uganda 1 - 1 Zimbabwe | Egypt 2 - 0 Congo

Ratiba 27/06/2019: Madagascar vs Burundi | Senegal vs Algeria | Tanzania vs Kenya

Matokeo: Madagascar 1 - 0 Burundi | Senegal 0 - 1 Algeria | Tanzania 2 - 3 Kenya

Ratiba 28/06/2019: Tunisia vs Mali | Morocco vs Ivory Coast | South Africa vs Namibia

Matokeo: Tunisia 1 -1 Mali | Morocco 1 - 0 Ivory Coast | South Africa 1 - 0 Namibia

Ratiba 29/06/2019: Cameroon vs Ghana | Benin vs Guinea Bissau | Burundi vs Guinea

Matokeo: Cameroon 0 - 0 Ghana | Benin 0 - 0 Guinea Bissau | Burundi 0 - 2 Guinea

Ratiba 30/06/2019: Madagascar vs Nigeria | Uganda vs Egypt | Zimbabwe vs Congo

Matokeo: Madagascar 2 - 0 Nigeria | Uganda 0 - 2 Egypt | Zimbabwe 0 - 4 Congo

Ratiba 01/07/2019: South Africa vs Morocco | Namibia vs Ivory Coast | Tanzania vs Algeria | Kenya vs Senegal

Matokeo: South Africa 0 - 1 Morocco | Namibia 1 - 4 Ivory Coast | Tanzania 0 - 3 Algeria | Kenya 0 - 3 Senegal

Ratiba 02/07/2019: Benin vs Cameroon | Guinea Bissau vs Ghana | Angola vs Mali | Mauritania vs Tunisia

Matokeo: Benin 0 - 0 Cameroon | Guinea Bissau 0 - 2 Ghana | Angola 0 - 1 Mali | Mauritania 0 - 0 Tunisia

UPDATES 2

Baada ya mechi za makundi nchi zilizofaulu kuingia raundi ya mtoano ni: Morocco, Benin, Uganda, Senegal, Nigeria, Cameroon, Egypt, South Africa, Madagascar, Congo, Algeria, Guinea, Mali, Ivory Coast, Ghana, Tunisia

Baada ya mechi za makundi nchi zilizotolewa ni: Tanzania, Kenya, Namibia, Burundi, Zimbabwe, Mauritania, Angola, Guinea Bissau

Round of 16

Ratiba 05/07/2019: Morocco vs Benin | Uganda vs Senegal

Matokeo: Morocco 1 - 4 Benin (Kwa mikwaju ya penalti); Dakika 90 ziliisha kwa kila timu kufunga goli 1 -1, zikaongezwa dakika 30 nazo hazikuwa na mshindi {Benin imeingia robo fainali}

Matokeo: Uganda 0 - 1 Senegal {Senegal yaingia robo fainali}

Ratiba 06/07/2019: Nigeria vs Cameroon | Egypt vs South Africa

Matokeo: Nigeria 3 - 2 Cameroon {Nigeria imeingia robo fainali} | Egypt 0 - 1 South Africa {South Africa imeingia robo fainali}

Ratiba 07/07/2019: Madagascar vs Congo | Algeria vs Guinea

Matokeo: Madagascar 4 - 2 Congo (Kwa mikwaju ya penalti); Dakika 90 ziliisha kwa kila timu kufunga magoli 2 - 2, zikaongezwa dakika 30 nazo hazikuwa na mshindi {Madagascar imeingia robo fainali}

Matokeo: Algeria 3 - 0 Guinea {Algeria imeingia robo fainali}

Ratiba 08/07/2019: Mali vs Ivory Coast | Ghana vs Tunisia

Matokeo: Mali 0 - 1 Ivory Coast {Ivory Coast Imeingia robo fainali}

Matokeo: Ghana 4 - 5 Tunisia (Kwa mikwaju ya penalti) Dakika 90 ziliisha kwa kila timu kufunga goli 1 - 1, zikaongezwa dakika 30 nazo hazikuwa na mshindi {Tunisia imeingia robo fainali}

UPDATES 3

Nchi zilizofanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ni: Nigeria, South Africa, Senegal, Benin, Ivory Coast, Algeria, Madagascar na Tunisia

Ratiba: Robo Fainali

10/07/2019: Senegal vs Benin | Nigeria vs South Africa

11/07/2019: Ivory Coast vs Algeria | Madagascar vs Tunisia

Matokeo 10/07/2019: Senegal 1 - 0 Benin {Senegal imeingia nusu fainali} | Nigeria 2 - 1 South Africa {Nigeria imeingia nusu fainali}

Matokeo 11/07/2019: Ivory Coast 3 - 4 Algeria (Kwa mikwaju ya penalti) Dakika 90 ziliisha kwa kila timu kufunga goli 1-1, zikaongezwa dakika 30 nazo hazikuwa na mshindi {Algeria imeingia nusu fainali}

Matokeo 11/07/2019: Madagascar 0 - 3 Tunisia {Tunisia imeingia nusu fainali}

UPDATES 4

Ratiba: Nusu Fainali


14/07/2019: Senegal vs Tunisia | Nigeria vs Algeria

Matokeo 14/07/2019: Senegal 1 - 0 Tunisia {Senegal imeingia fainali} | Nigeria 1 - 2 Algeria {Algeria imeingia fainali}

UPDATES 5

Ratiba: Kutafuta Mshindi wa Tatu


17/07/2019: Tunisia vs Nigeria

Matokeo 17/07/2019: Tunisia 0 - 1 Nigeria {Nigeria wamekuwa washindi wa tatu}


UPDATES 6

Mechi ya Fainali 19/07/2019: Algeria vs Senegal

Latest Scores

7" Algeria 1 - 0 Senegal

Halftime: Algeria 1 - 0 Senegal

60" Algeria 1 - 0 Senegal

70" Algeria 1 - 0 Senegal

80" Algeria 1 - 0 Senegal

85" Algeria 1 - 0 Senegal

90+ Algeria 1 -0 Senegal

Final Score: Algeria 1 - 0 Senegal

Algeria imefanikiwa kuchukuwa ubingwa wa Afcon 2019
 
Front seat booked tayari

Awali ya yote niipongeze taifa stars kwa kuwa mmoja wa washiriki wa michuano ya mwaka huu.

Angalau sasa hivi na sisi tutaona wimbo wetu wa taifa ukiimbwa huku na bendera yetu ikiwa kwa pembeni wakati huo tunangaliwa na bara zima.

Binafsi nilikuwa nimechoka kila mwaka kuangalia na kushabikia timu za watu tu, angalau sasa hivi pengine labda na sisi huu utakuwa ndio mwanzo wa kupata mashabiki wa timu yetu ya taifa nje ya taifa letu kama yalivyo mataifa mengine tuliozoea kuyashabikia.

Timu yangu ya kwanza kui-support ni Taifa stars na hisia zangu zinaniambia hatutoki bila point katika michuano hii.

Kuhusu timu itakayochukua ubingwa ni ngumu kutabiri, lakini naona kama vile hii fainali itachezwa na waarabu tupu kama ilivyokuwa kwenye CAF champs league.

Kwa hap Afrika mashariki nategemea Uganda ndio watatuwakilisha vizuri na si ajabu wakafika nusu fainali.

Mungu ibariki stars na kila anayeisapoti.
 
Back
Top Bottom