Ndiyo matatizo ya kuwa na madudu chungu nzima halafu unataka kugombea kuingia WH, lazima madudu ya miaka chungu nzima yaibuliwe. Angejikalia pembeni kula bata zake haya yote yangebaki chini ya carpet.
Precisely my sentiments.
Lakini huu uchaguzi GOP wasiuchukulie vibaya [naamini watashindwa tu hiyo Novemba 8].
Wauchukulie kama 'teachable moment'. Baada ya uchaguzi itabidi wakae chini wajifanyie tathmini na tafakuri ya wapi walipokosea hadi wakapata mgombea mbovu kiasi hivi.
Ni muda muafaka sasa wa kuangalia upya vigezo na masharti ya kupata mgombea.
Ni vyema kabla ya mtu hata kuchukua nomination forms kufanyiwa vetting kali sana ili kuepusha majanga mbeleni.
Waweke vigezo fulani vikali ambavyo watangaza nia itabidi wavikidhi kabla ya kukubaliwa rasmi.
Hata Dems nao wana la kujifunza kutokana na hii kashfa ya Trump ili nao siku mmoja wasije kujikuta wamepata mgombea kichaa.
Kwa mfano, kama mtu hayuko tayari kuonyesha tax returns zake kabla hata primaries hazijaanza, hiyo iwe disqualification.
Kama mtu ana mi sexual allegations kibao nayo iwe ni disqualification.
Ni lazima vyama viwe na vetting process kali sana ili walau kujipa fursa ya kutokuja kupata mtu kichaa kama Trump.
Minong'ono ya Trump kugombea ilianza zamani. Lakini mimi sikuwa naamini hata kidogo kwamba angeweza kufika mbali namna hii kwa sababu sijawahi kabisa kumwona akiwa serious.
Ila ndo hivyo tena, keshafika hapo alipo na bado anayo nafasi ya kushinda [ingawa binafsi sidhani kama atashinda...ila anything can happen].