2016 US Election Results: Donald Trump has won the presidency

2016 US Election Results: Donald Trump has won the presidency

Mkuu, ina maana wewe una uchungu na nchi ya Amerika kuliko Waamerika wenyewe, naona kama ungekuwa wewe ungetoa matokeo yako ambayo si ya Waamerika, ndo tayari wameisha amua iwe hivyo.

Wapi nimeandika kuwa nina uchungu? Nimeonesha ukweli ulijidhihirisha katika matokeo haya ya uchaguzi wa USA. Na bahati nzuri kwa nchi yetu tuna Rais asiye jipendekeza.

Na washawasha!
 
Ujumbe bora Raisi wetu John Magufuli angeandika kwa kiswahili
 
Hadi sasa sielewi nini kimetokea Marekani hadi Trump kushinda, kipindi cha kampeni hata uelekeo wa ''upepo'' ilikuwa ni wazi Mama Clinton anaingia ikulu, hebu mwenye uelewa wa haya mambo nisaidieni kidogo, au jinsia yake ndo imemwangusha??
 
629ba1a4ecfcdf744b947c3d78d1a87d.jpg
Hamna namna, warudi tu manake hata Babu zao walishasema; ndama akivunjika mguu urudi zizini!

Karibu nyumbani Jumanne Zuberi!
 
Saiv mwarabu kuingia marekani itakua ishu
Trump atabadilika. Na kampeni ni kitu -ingine kabisa.Na maisha baada ya kampeni ni kitu -ingine. Ni sawa na CCM wakisema maisha bora kwa kila mtanzania kwenye kampeni na machungu ya maisha kwa kila mtanzania baada ya uchaguzi.

Umeshamsikia Trump anasema" we owe her a major debt of gratitude for her service to our country,” . Siasa ni mchezo mbaya sana kwa utu wa binadamu.

“Hillary has worked very long and very hard over a long period of time, and we owe her a major debt of gratitude for her service to our country,” Trump said. “I pledge to every citizen of our land that I will be president for all Americans and this is so important to me.”

Link Donald Trump Has Defeated Hillary Clinton in a Stunning End to the Presidential Race

Link Trump: US owes Clinton 'debt of gratitude' for her service - Vanguard News
 
SIO HIVYO TU MKUU.
TRUMP KAONGEZEA NA KUSEMA KAMPENI ZIMEISHA NI WAKATI WA KUJENGA USA.
Fuatilia mwisho wa hotuba yake.
Speech nitaifuatilia baadae mkuu wacha na mimi nijenge Tanzania kwanza Uchaguzi ushaisha Nimefurahi sana... Asiyependwa ndio kaja
 
Binafsi kama walivyowengi sikutegemea kabisa Trump kushinda. Vyombo vyote vya habari vikikuunga mkono kama vilivyofanya kwa mama Hillary uwezekano wa kushinda ni mkubwa. Tunakumbuka hapa kwetu CCM waliwahi siku ya mwisho karibu media zote, Kuna media kama Star TV walikuwa hawamuachi mamvi apumue, kwa Trump CNN, WSJ, NBC, Dailymail UK, Sky etc wote walikuwa kinyume na huyu mheshimiwa lkn matokeo yameamuliwa na Silent Majority.
Wapenzi wa hbr Za Trump tuliishia kwenye mitandao ya kirusi kama RT angalau tuangalie mashambulizi ya Wikilieaks na matumaini kidogo kwa Trump.

Mara ya kwanza kumjua mtu anaitwa Trump ni mwaka 2011 baada ya kupewa kitabu kiitwacho WHY WE WANT YOU TO BE RICH. By R. Kiyosaki na D. Trump kama nilivyomjua mwanasiasa mwingine Ben Carson mwaka 2002 Kupitia kitabu chake THINK BIG.

Miaka mitatu baadae nikakutana na softcopy niliyoitoa humu JF nadhani kwenye Ule uzi uliopo JF stores "Kuna kitabu chochote unatafuta" kitabu kinaitwa MIDAS TOUCH (Uwezo wa kubadili chochote kuwa dhahabu). kikiandikwa na hao hao Trump na mwenzake. Humo ndio nilijifunza somo la akili alililielezea Trump mwenyewe kuwa Kuna aina Saba ya akili hii ya darasani ni tawi tu Kati ya hizo Saba. Baadae katika group moja la kwenye mtandao la kusoma vitabu nikakutana na kitabu kingine Cha Trump mwenyewe kinaitwa Don't Give up nilipitia kwa juujuu lkn Kuna madini mazuri pia.

Ukisoma vitabu vyake utamuona Trump kama mtu mwenye Uwezo mkubwa, mwenye ushawishi kwa wasionacho kuwa siku moja mambo yatakuwa mazuri, kwa ufupi anauwezo mkubwa, Cha ajabu alipojitokeza kwenye campeni alionekana mkorofi, asiyetaka mapatano, mkali etc nikabaki mdomo wazi mbona yule jamaa wa kwenye vitabu huwa mstaarabu mwenye hekima na akili? Ya wezekana alikuwa ameshawekeza kwenye maisha ya wamarekani alijua wanataka nini.

Ninaamini wamarekani wamepata mtu mwenye Uwezo mkubwa, Ninamkubali 100%.
Ulimuelewa vipi Trump kabla ya kupambana kwenye siasa na kuwa Rais Leo?
 
Back
Top Bottom