Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,227
Mkuu Tujitegemee
Huko nyuma tumeeleza kwa uchache jinsi Da'Amina alivyopenya hadi 3 .
Hilo ni moja ya tatizo linalotukabili nchini. Hatuchagui viongozi kwa merits, bali kuongozwa na eneo au jinsia.
CCM wanaongozwa na hofu ya kukutana na KANU na UNIP kama watu wataamua kubadilika.
Karata inayochezwa ni jinsia
Mkuu, kuelimika ni zaidi ya vyeti mtu anavyopata. Hatunad hamira ya ku criticize elimu yake, tunachosema ni kuwa elimu ni pamoja naweledi na exposure
Inaonekana Da, amepata nafasi nyingi za kumwezesha kuwa na weledi na exposure.
Swali, je alitumia fursa hizo kupata maarifa zaidi?
Nafasi aliyokuwa anawania inahitaji weledi, hatudhani yeye kama yeye alikuwa tayari kwa ‘prime time'.
Kilichotokea aliandikiwa hotuba na washauri wake kwa lengo la kupata nafasi.
Ndio maana alimshirikisha Edo bila kutambua alikuwa anatia nyongo katika kitumbua.
Hakujua kuwa hadi wakati ule kambi ya Edo ilikuwa namaruwe ruwe 'Delirium'
Waliomwandikia hatujui uelewa wao katika mambo ya siasa.
Siasa za siku hizi ni za kisayansi si za kukota wapiga debe.
Nadhani washauri wake walikuwa dhaifu, ukichanganya na udhaifu wake, unaishia kupata suala la middle class kuelekea first world
Ilikuwa ni rahisi kubaini. Wiki iliyopita UN imetangaza nchi zilizoingia uchumi wa kati.
Jirani zetu kenya walikuwa kundi moja vi nchi masikini sana. Hatujui kama alioma habari hizo
Tuna tatizo, sasa huyo ndiye alikuwa awe mgombea!
Mkuu kwanza shukran sana kwa mchango wako na nadhani watu hawafahamu ya kwamba URAIS ni mpango wa muda mrefu kwa vyama haswa kwa nchi za Kiafrika (maskini) kwa sababu bado ni mataifa tegemezi. Kwa hiyo hotuba ya Bi. Amina haikuwa na malengo ya kupotosha bali kuwapa wajumbe na wananchi tumaini zaidi ya kwamba UCHUMI wetu ulikuwa katika hali nzuri kulingana na malengo yalotakiwa kufikiwa. Ukati wake unategemea na ujazo wa chupa tulobeba...Naufatilia kwa karibu mjadala huu, na ahsanteni nyote kwa michango yenu.
Haikuwa nia yangu kusimamisha muendelezo wa mjadala huu na kuwarudisha nyuma juu ya sifa za watia nia kugombea urais kupitia CCM ambao walifika tatu bora (nadhani twaweza kusema bora tatu). Lakini nimelazimika kuwarudisha nyuma ili niweze kupata maoni yenu juu ya jambo hili ambalo kila ninavyojaribu kulipuuzia kutolileta jamvini linazidi kunikereketa kichwani.
Jambo lenyewe ni kuhusu hotuba walizozitoa watia nia hao wa 'bora tatu' wakati wakiomba kura kwenye mkutano mkuu wa CCM. Niliwasikiliza wote watatu (John, Amina na Asha-Rose) kupitia redio. Amina na Asha-Rose inaonekana walijiandaa, kutokana na namna walivyojieleza lakini John kwa jinsi alivyoomba kura ni dhahiri shairi hakujiandaa kwa tukio lile. Alishtukizwa. Hotuba iliyonistua ni ile ya Amina Salum Ali; hasa aliposema kuwa " ...sasa Tanzania ipo kwenye uchumi wa kati na inaelekea uchumi wa kwanza/juu..." hivyo atasaidia Tanzania kuingiiza kwenye uchumi wa juu akiwa rais wa nchi hii. Nimejaribu kulifuatilia hili kuona kama mimi ndiye 'niliyepitwa na wakati' kiasi kwamba sijui hata uchumi wa nchi yangu uko kiwango gani (kwani nilikuwa najua Tanzania uchumi wetu ni wa kiwango cha chini-low income economy country).
Nilivyotembelea tovuti ya Benki ya Dunia nikakuta kumbe bado Tanzania ni nchi yenye uchumi wa chini ( Tanzania | Data ). Nilivyododosa zaidi juu ya Mama Amina S.A nikagundua alisomoea masuala hayo ya biashara, masoko na uchumi huko India na kwingineko. Na masuala hayo ya Uchumi, masoko na biashara ni masuala ambayo yanahusisha sana takwimu sahihi ili kufikia maamuzi. Pia nikagundua Mama A.S.A ni:
" Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika (AU) Marekani (United States) akiwa kama ni Muwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika. (i) Mshauri wa Kamisheni Umoja wa Afrika kuhusiana mambo ya Afrika huko Marekani. (ii) Kufuatilia mambo ya Maendeleo ya Afrika huko Marekani kwa kuwajuilisha kuhusu sera mbali mbali za bara la Afrika zinazoendelea na mpya. (iii). Kuwashajiisha wawekezaji wa Marekani na pia Diaspora wa jamii ya Kiafrika huko Marekani kuwekeza Afrika. (iv) Kuimarisha uhusiano baina ya Marekani na vyombo vya Serikali, Mabunge na Taasisi za kijamii za Afrika . (v) Kusaidia kupatikana kwa Fedha za Maendeleo ya Afrika kwa kuzieleza Sera za Maendeleo za Afrika, na kuwashawishi waziunge mkono. (vi) Kushirikiana na vyombo vya fedha vya Bretton Woods (World Bank na IMF) kwa Maendeleo ya Afrika.
......................... . (Rejea>>>https://www.jamiiforums.com/uchaguz...tegemewa-kuwa-makamu-wa-rais-kupitia-ccm.html)
Sasa ninajiuliza kama huyu Mwakilishi wetu wa waafrika huko US mwenye majukumu mazito namna hiyo anashindwa kujua nchi ipo kiwango gani kiuchumi (kama takwimu za world bank zitakuwa sahihi):
1. Je. Kamati ya usalama na maadili ya CCM, baraza la ushauri la Wazee wa CCM, Kamati kuu ya CCM (CC), na halmashauri kuu ya CCM (NEC) hawaoni kuwa sasa ni muda muafaka kuwaomba radhi wanachama wa CCM kwa kushindwa kutekeleza jukumu lao sawa sawa kiasi cha kumpitisha mtia nia ambaye hajui anataka kuongoza nchi ya namna ki-uchumi ?
2. Je. hivi kwa kiwango chake (hadhi na kitaaluma) huyu Mama Amina S.A tunaweza kusema 'aliteleza kutoa kauli ile' hivyo tumuache aendelee kutuwakilisha huko US bila bughudha?
Tusemezane juu ya hili kisha tuendelea na mada.
Mkuu Mkandara
Ni tofautiane nawe kuhusu kuwalaumu wananchi kwa yanayotokea. Ninaamini kabisa, badala ya kuwalaumu wanasiasa na vyama vya upinzani, wananachi wanapaswa kuchukua lawama hizo.
Hakuna mahali katika dunia hii nguvu ya dola iliwahi kushinda umma. Dola ni zao la nguvu ya umma na si kinyume chake
Kwa dunia ya wenzetu, wanasiasa huwatumikia wananchi na si wananchi kuwatumikia wao.
Mambo yekienda kombo, jukumu la kuweka sawa ni la wananchi si la vyama vya siasa.
Vyama vya siasa hubeba agenda ya wananchi kwavile wana platform. Hufanya hivyo wakijua agenda ya wananchi ndio muongozo na si kinyume chake
Kama tutakubaliana wananchi hawana sababu ya kubeba lawama, tukubaliane hawana sababu za kulaumu wanasiasa
Muhimbili wananchi wakilala sakafuni, akina mama wakipanga foleni ya kwenda kwenye chumba cha kujifungulia hilo si tatizo la wanasiasa wanaotibiwa chunusi Appolo au Joberg. Na wala hakuna mwanasiasa atakayesimama kuzungumzia matatizo hayo kwasababu hayamhusu.
Kwa nchi za wenzetu, wananchi wanachukua jukumu mikononi mwao, iwe kwa njia ya sanduku la kura au nyingine
Ni makosa kuwapumbuza wananchi tukitumaini kuwa ipo siku malaika watataremka kulinusuru taifa. Tumejaribu miaka 50, je tusubiri hadi karne nyingine? Wale wenzetu wanaochukua hatua dhidi ya 'malaika' wamepungukiwa nini ?
Ni wananchi wa Tanzania peke yao wanaosubiri miujiza na si wao kuchukua hatma ya taifa lao
Wanasiasa wamefikia mahali wanadhani wao ndio nchi. Sababu kubwa ni wananchi walioshindwa kuwaambia wao ni waajiriwa. Mwajiri anaposhindwa kuchukua hatua dhidi ya mwajiriwa hilo ni tatizo lake, si la mtu au taasisi nyingine
Mkuu hakuna nchi iliyofanikiwa kupigana na rushwa kama hizi za chaguzi bila kuwashirikisha wadau a.k.a wananchiNguruvi3:
Kwa sababu ulianzishwa mradi wa demokrasia ya vyama vingi, basi tunaweza kuwalaumu wananchi kwa matatizo yanayotokea Tanzania. Lakini ukichunguza kwa makini demokrasia yenyewe haikuja kumpa mtanzania nafasi ya kuchagua viongozi bora. Ilikuja hili kuonyesha wahisani kuwa Tanzania nayo ina mfumo wa vyama vingi. Hivyo kuwalaumu wananchi wa kawaida ni kutowatendea haki.
Ni kweli wananchi wanatakiwa kuwa chachu ya maendeleo yao. Lakini tusisahau kuwa kundi la intelligensia ndio kioo cha jamii. Na hili kundi ndilo lingeweza kutoa mabadiliko ya kweli ya kijamii. Kwa Tanzania kundi hili bado halijakuwa chachu za maendeleo. Leo hii madaktari, maprofessa, wanafunzi vyuo vikuu na wafanya kazi wa idara za kiserikani wakigoma kudai mabadiliko, mabadiliko hayo yatatokea. Kwanini sasa anasubiriwa mwanakijiji ambaye hana uwezo kufanya uchambuzi.
Nimerudi kutoka Tanzania, wasomi wengi wanaotaka kugombea viti mbalimbali kupitia CCM wanatoa rushwa hili wapate nafasi ya kugombea kupitia chama. Hawa watu ni vioo kwa jamii zao. Kama wao wanaweza kufanya hivyo, kwanini mwananchi wa kawaida asifanye hivyo?
Dr.Slaa pengine ndiye mwanasiasa wa upinzani anaeheshimika na kusikilizwa zaidi Tanzania.
Yote hii ni sababu ya misimamo yake kupinga ufisadi, kusimamia na kutetea maslai ya Taifa bila kuogopa.
Amewahi kutaja hadharani listi ya mafisadi 11 Lowasa akiwa namba tisa na Kikwete akiwa namba kumi na moja.
Alienda kule Arumeru alimtuhumu Lowasa waziwazi kwa ufisadi na kukwepesha miradi ya Arumeru na kuipeleka Monduli.
Lakini leo tunaambiwa kuwa Lowasa anakaribishwa ndani ya Chadema na kuungama dhambi na atasamehewa.
Sina tatizo na ujio wa Lowassa ndani ya chama tatizo langu ni heshima na taswira ya Dr. Slaa aliyojijengea kwa muda mrefu kwa kuukemea ufisadi.
Je leo yupo tayari kutangaza hadharani kuwa Lowasa amekuwa msafi sio fisadi tena, yupo tayari kupunguza ile list of shame ya Mwembeyanga kutoka kumi na moja na kubaki kumi.?
Japo siasa hazina adui wa kudumu wala urafiki wa kudumu, kwa hili naona heshima ya Dr.Slaa na Chadema kwa ujumla ikiporomoka.
Maana heshima ya Dr Slaa na Chadema imejengwa kwa kuukemea ufisadi, lakini tunakoelea Hali itabadilika na kuwa Chadema ni chama cha kuwasafisha Mafisadi.
Kuelekea Uchaguzi Mkuu Tutasikia mengi sana Leo hii Chadema wanamlilia Lowassa.
Tusemezane.
Mkuu wangu tuendelee kutokubaliana katika hoja hizi maana mitazamo ipo mingi na tutafikia mahala tutaelewana kwa kutokubaliana..Mkuu Mkandara
Ni tofautiane nawe kuhusu kuwalaumu wananchi kwa yanayotokea. Ninaamini kabisa, badala ya kuwalaumu wanasiasa na vyama vya upinzani, wananachi wanapaswa kuchukua lawama hizo.
Hakuna mahali katika dunia hii nguvu ya dola iliwahi kushinda umma. Dola ni zao la nguvu ya umma na si kinyume chake
Kwa dunia ya wenzetu, wanasiasa huwatumikia wananchi na si wananchi kuwatumikia wao.
Mambo yekienda kombo, jukumu la kuweka sawa ni la wananchi si la vyama vya siasa.
Vyama vya siasa hubeba agenda ya wananchi kwavile wana platform. Hufanya hivyo wakijua agenda ya wananchi ndio muongozo na si kinyume chake
Kama tutakubaliana wananchi hawana sababu ya kubeba lawama, tukubaliane hawana sababu za kulaumu wanasiasa
Muhimbili wananchi wakilala sakafuni, akina mama wakipanga foleni ya kwenda kwenye chumba cha kujifungulia hilo si tatizo la wanasiasa wanaotibiwa chunusi Appolo au Joberg. Na wala hakuna mwanasiasa atakayesimama kuzungumzia matatizo hayo kwasababu hayamhusu.
Kwa nchi za wenzetu, wananchi wanachukua jukumu mikononi mwao, iwe kwa njia ya sanduku la kura au nyingine
Ni makosa kuwapumbuza wananchi tukitumaini kuwa ipo siku malaika watataremka kulinusuru taifa. Tumejaribu miaka 50, je tusubiri hadi karne nyingine? Wale wenzetu wanaochukua hatua dhidi ya 'malaika' wamepungukiwa nini ?
Ni wananchi wa Tanzania peke yao wanaosubiri miujiza na si wao kuchukua hatma ya taifa lao
Wanasiasa wamefikia mahali wanadhani wao ndio nchi. Sababu kubwa ni wananchi walioshindwa kuwaambia wao ni waajiriwa. Mwajiri anaposhindwa kuchukua hatua dhidi ya mwajiriwa hilo ni tatizo lake, si la mtu au taasisi nyingine
Wanasiasa wamefikia mahali wanadhani wao ndio nchi. Sababu kubwa ni wananchi walioshindwa kuwaambia wao ni waajiriwa. Mwajiri anaposhindwa kuchukua hatua dhidi ya mwajiriwa hilo ni tatizo lake, si la mtu au taasisi nyingine
Wananchi hawawezi fanya lolote ikiwa mfumo wenyewe ni mbaya kiasi kwamba tuna Ushabiki wa vyama na sio Upinzani. Hili ni tatizo kubwa Kidemokrasia nchini na hivyo itachukua miaka pengine 20 mbele kabla ya mageuzi ya fikra ifikie watu kuvitazama vyama kiitikadi badala ya WATU waliomo.Mkandara.nimekusoma vizuri wewe pamoja na Nguruvi3. hoja zenu.
Ni kipi wananchi wanatakiwa kukifanya kwa sasa maaana walikuwa wanategemea upinzani kama kimbilio lao upinzani nao kimbilio lao kwa hawa mafisadi ambao kila siku wamekuwa wakiwambia wananchi ndiyo wanaoliangamiza taifa letu kwa ufisadi.
Kwa mtazamo huu wananchi wanaotaka mabadiliko wamebakia njia panda hawajui wapi wakimbilie.