Well said Mwanakijiji….lakini iwe ni rais kijana au mzee; mwenye busara au asiye na busara bado hawezi kukukabiliana na changamoto zxa msingi za taifa hili ikiwa bado atakuwa anaongozwa na Katiba inayosimamia utawala bora wa kimagharibi! Nchi yetu ina matatizo makubwa; yasiyoweza kunyanyulika kwa folk lift wala kwa winch! Kabla ya huyo rais ambae wewe na wengine wote tungependa tuwe nae kwanza anapaswa kupewa nyenzo itakayobeba matakataka makubwa kuliko yote yaliyopo nchini kwetu na kwenda kuyatupilia mbali…ikibidi hata bahari ya Pacific ili yasirejee tena nchini mwetu! Matakata haya, ni maadili mabovu ya Watanzania; ingawaje tunataka kuaminishana kwamba ni maadili mabovu ya Viongozi wa CCM! Nyenzo pekee anayopaswa kupewa rais huyo chaguo la wote ni Katiba ya Kidikteta…..Sio Kiongozi wa Kidikteta; bali ni Katiba ya Kidikteta itayaoondowa makandokando yote yaliyogubika mioyo hasidi ya Watanzania walio wengi!
Vyovyote iwavyo, hata kama Rais ajae atoke mbinguni, bado hawezi kuondoa makandokando hayo chini ya katiba inayohubiri Utawala Bora; Utawala Bora wa Kimagharibi! Mfumo ambao, moja ya nguzo zake kuu ni Utawala wa Sheria!! Mfumo ambao unatuambia kwamba mtu atabaki kuwa mtuhumiwa hadi pale itakapothibitika; beyond reasonable doubt kwamba kosa analotuhumiwa nalo kwamba ni kweli amefanya!! Kwamba; leo hii ingawaje William Mhando anatuhumiwa kufanya ufisadi TANESCO lakini bado huwezi kuwa na grounds za kumpeleka korokoroni na kumtupa jela….huwezi kufanya hivyo kwa kuwa huna ushahidi; huo ndio Utawala wa Sheria; moja ya nguzo muhimu kabisa za Utawala Bora!!! Wengine nao wanadai Maswi (Katibu Mkuu wa Nishati) ndie fisadi na ananufaika na Puma Energy….huyo nae, huwezi kumpeleka mahakamani kwavile hakuna ushahidi…na hata ukimpeleka bado atashinda kesi; huo ndio Utawala wa Sheria, ambao ndio msingi mkuu wa Utawala Bora!
Hivyo basi, tatizo sio ni rais wa aina gani, bali ni katiba ya aina gani !! Tunahitaji kwanza katiba ya kidikteta itakayo-shape maadili ya Watanzania!Tunahitaji Katiba ya Kidikteta ambayo itamafanya rais yeyote ajae 2015 kufanya si kwa kutaka bali kwa kulazimishwa na Katiba Ya Kidikteta!! Katiba ambayo, itatamka wazi, ile kutuhumiwa peke yake inatosha kabisa kumpeleka mahakamani mtuhumiwa na badala ya kutaka upande wa mashitaka ndio uthibitishe beyond reasonable doubt tuhuma dhidi ya mtuhumiwa; basi ni mtuhumiwa ndie athibitishe beyond reasonable doubt kwamba tuhuma dhidi yake si sahihi…tuhuma ninazozungumza hapa ni zile ambazo ndizo kansa kuu ya nvchi hii; TUHUMA ZA UFISADI!! Katiba ya Kidikteta ambayo pia itatamka wazi kwamba; kumzushia mtu tuhuma ambazo si za kweli; hiyo nayo ni serious crime ili kuzuia watu kuwazushia wenzao kwavile tu wanafahamu wazi kwamba Katiba Yetu Mujarabu Ya Kidikteta itamwajibisha yule anayemzushia!
Anyway, nazani hili linahitaji thread inayojitegemea lakini nihitimishe tu kwamba kwa katiba yoyote itakayoendeleza Mfumo wa Utawala Bora ambao moja ya nguzo zake kuu ni Utawala wa Sheria basi haitakuwa na msaada wenye tija kwa rais awaye yote labda tu aamue kuvunja misingi ya katiba inayohubiri utawala bora!