2015 ndio ilikuwa mara ya mwisho Tanzania kuwa na uchaguzi, tusichanganyikiwe

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
57,239
Reaction score
90,296
Tutaongea yote ila mara ya mwisho Tanzania kuwa na uchaguzi mkuu au serikali za mitaa ni mwaka 2015.

Kumuhusudu na kumkubali aliyesababisha hali hii yote ya sasa huku unamlaani na kumkosoa mrithi na mwanafunzi wake ni sawa na kuchanganyikiwa na kuwa bumunda.
 
Tunaweza hata tusije kupata tena uchaguzi kama ule, ikawa mfumo wa uchaguzi wa 2020 na 2025 ndio tutakaoendelea nao milele.
Ni kweli..kipindi kile hata wapinzani waliungana na walimsumbua sana ccm. Nadhani baada ya pale ccm alipata somo kuwa anatakiwa kuhakikisha anawagawa wapinzani kwanza wasiwe kitu kimoja halafu ndo tunaenda kwenye uchaguzi.
 
CCM Haijawagawa upinzani bali imeua mfumo wa uchaguzi ndani ya CCM yenyewe na katika taifa.
 
Wewe ndo unachanganyikiwa bosi. Ni lini kuliwahi kuwa na uchaguzi hapa Tanzania ama labda huko nyuma ulikuwa hujazaliwa. Kama tuliwahi kuwa na uchaguzi kabla ya 2015, ya wapi matokeo ya uchaguzi mwaka 2010?. Maana ya uchaguzi ni pale taratibu zinapohitimishwa na matokeo ya wazi, Sasa tukuulize wewe hapo utusaidie. Matokeo ya 2010 Yako wapi na majumuisho yake Yako wapi?
 
Kumuhusudu na kumkubali aliyesababisha hali hii yote ya sasa huku unamlaani na kumkosoa mrithi na mwanafunzi wake ni sawa na kuchanganyikiwa na kuwa bumunda.
Mkuu kwani kwenye siasa kanuni ya "KILA MTU ATABEBA MZIGO WAKE" huwa haifanyi kazi?

Maana tokea uchaguzi umeanza kwenye Nchi hii, kila uchaguzi una vituko vyake.
 
Ni kweli..kipindi kile hata wapinzani waliungana na walimsumbua sana ccm. Nadhani baada ya pale ccm alipata somo kuwa anatakiwa kuhakikisha anawagawa wapinzani kwanza wasiwe kitu kimoja halafu ndo tunaenda kwenye uchaguzi.
Hakujawahi kuwa na free and fair elections Tanzania. Hata hizo chaguzi za 2015 kurudi nyuma wizi, udanganifu na nguvu za vyombo vya dola zilitumika kuhakikisha CCM inabaki madarakani, 2020 & 2025 hakukuwa na uchaguzi kabisa.
 
Tutaongea yote ila mara ya mwisho Tanzania kuwa na uchaguzi mkuu au serikali za mitaa ni mwaka 2015.

Kumuhusudu na kumkubali aliyesababisha hali hii yote ya sasa huku unamlaani na kumkosoa mrithi na mwanafunzi wake ni sawa na kuchanganyikiwa na kuwa bumunda.

Ungekuwa na uwezo wa kufikiria walau kidogo,ungejiuliza maswali kama haya

Kwanini hakurithi kutokusafiri safari hovyo kama mwalimu wake

Kwanini hakurithi kugomea chanjo za uviko na mikopo yake ili awe mwanafunzi bora

Kwanini hakurithi kutokufuja rasisilimali za Taifa kama mwalimu wake

Kwanini hakurithi kujaribu kujenga Taifa lenye kujitegemea

Na mengine mengi tu ya namna hiyo,ila kwasabu umeshasema kwamba wewe ni BUMUNDA,basi TUFANYE upo SAHIHI
 
Kwa sababu anajua Kingereza kidogo na yeye ni wa mjini tofauti na mwalimu wake aliyetokea Bush kwa hiyo yeye yuko polished.
Mwalimu wake alifuja rasilimali za Taifa pia ila kwa namna nyingine, huoni alijenga Airport ya kimataifa kijijini kwake na kuifanya nchi kuwa Ikulu mbili.
Mwalimu wake alikuwa mtu wa propaganda ndio maana hamjui alichukua mikopo kwa Matrilioni kutoka kwa mabeberu.
 
Back
Top Bottom