2015 Mlihubiri Mabadiliko, 2020 Mtahubiri Nini?

2015 Mlihubiri Mabadiliko, 2020 Mtahubiri Nini?

Tanzania. hatuna kitu kinachoitwa "Election" bali tunafanyiwa "Selection" na wenye makali. Huwaga sio matakwa ya wananchi. Kwa style hii watashinda to infinity.
Kwa hiyo wamaanisha hata MAJIMBO ama KATA walizoshinda UPINZANI haikuwa ELECTION ni hiyo hiyo SELECTION usemayo?
 
Zaidi sana utaambulia matusi kutoka kwa wafuasi wao

On mnachojua chana kina wanachama hakuna wafuasi.

Anyway muda utakapofika mtajua mpaka sasa hakuna mabadiliko labda kujaza chuki na Visasi kwenye Taifa ndilo mliloliweza kwa asilimia 100
 
Wagumu sana kuelewa very simple concepts

The easiest way ni kuweka fair play kwenye kiwanja cha siasa halafu ndipo utawajua kama kuna wapinzani au lah.Katika mazingira ya kumiminiwa risasi 40 na taasisi za Umma halafu unasema hakuna upinzani basi una tatizo mahali.

Kama Mkullu wameshindwa kuishi kama Taasisi usitegemee Mabadiliko.Pamoja na kuongolea mabadiliko Chadema walionhelea mabadiliko ya taasisi,uchumi na maendeleo.

Leo tulipiga pushup tumeishia kuua wapinzani wanaoyukosoa.
 
Mabadiliko yenyewe ni ya akina mch. Msigwa na Lema? Hakuna cha m4c wala nini. Hata wakizungusha mikono hadi wapate kizunguzungu hawapati kitu.
2015 kamanda siro alipoka computer za watu pale haki za binadamu ! Kama kweli chama kilishinda kihalali kwanini alipoka! Jpm alipata kura 54000 tu dar nzima kama ile mikono ilikuwa haina maana mbona hasijafika hata laki
 
Badala ya kudai hakina upinzani mwambieni huyo anauejiita mzalendo arihusu mikutano ya vyama vya siasa . Yeye afanye jangwani na lowasa afanye popote dar tuone wapi kutajaa. Mnalinganisha aliyekaa na anayekimbia? Yan mtu ametunyima kuona bunge live kisha ndo awe shujaa huyo
 
We jamaa bado sana una mtazamo finyu sana unaosababishwa na elimu duni ya kuwa na uwezo wa kuchanganua mambo kwa kina. Huyu yupo ndani ya CCM lakini anajua fika uchaguzi ukiwa huru na wa haki CCM hawana chao ila wewe unatokwa povu zito kutokana na kutokuwa na uwezo wa kutafakari nini kinachoendelea nchini.



Tanzania bado hapajakuwa na chama cha upinzani ambacho kina reputation ya maana . Mbaya zaidi tukijaribu kuwashauri wafanye nini ili wawe na comparative advantage ni kama wameziba masikio.
 


Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kimfumo ambayo yatapelekea mabadiliko chanya ya kiuchumi, leo hii Magufuli anaongoza nchi kwa mfumo wa One Man Show ambao hatari yake ni kubwa mno maana mihimili yote mitatu inakuwa haitimizi wajibu wake kikatiba na badala yake inafanya kazi kwa maelekezo toka juu (mamlaka ya rais) rejea kauli ya rais Magufuli kwenda kwa mkuu wa mhimili wa Bunge Mh spika Ndugai kuwa wale wabunge wa upinzani ambao ni wakosoaji wakubwa wa serikali awatoe huko ndani ya bunge ili na yeye wakija huku nje ya bunge awashughulikie maana watakuwa hawana kinga ya bunge, rais katika hotuba zake ameenda mbali zaidi kwa kusema wale wakosoaji wakubwa wa serikali (aliowabatiza jina la wasaliti) hawastahili kuendelea kuishi, hivyo tafsiri yake wauliwe. Nchi hii tunahitaji Uhuru wa utendaji kazi katika mihimili ya dola na siyo kuwa na mmoja uliojichimbia ndani ambao uko tayari kuua wale against na Serikali kwa maslahi ya kumtetea mkuu wa nchi. Rais, uchumi wa nchi umemshinda unazidi kudorora kila kukicha, leo mapato ya serikali kupitia TRA ni hoi bin taabani ambayo ni bilioni 600 tu kutoka trioni moja tuliyokuwa tukitangaziwa kila baada ya mwezi mmoja mara baada tu ya utawala wa awamu hii kuingia madarakani, serikali imeamua kuanzisha TRA nyingine kwa jina la Polisi ambao nao wamekuwa wakusanyaji wa mapato na kila mwezi wanatangazia makusanyo yao. Toka kuingia madarakani kwa rais huyu hakuna miradi mikubwa ya maendeleo iliyoanzishwa tofauti na iliyoachwa na rais Kikwete, hivyo rais badala ya kutuletea mabadiliko chanya anatuletea mabadiliko hasi ya kiuchumi, neno mabadiliko Magufuli alilikariri tu kinywani kwenye majukwaa ya kisiasa kipindi cha kampeni kutokana na upepo wa kisiasa ulivyokuwa mgumu kwa ccm pasipo kuwa na mipango mikakati yake, leo hii ukiwauliza hata hao mawaziri kuhusu 'vision 2025' kwa usawia na ufasaha hawaijui.
 
2020 sitataka kujua upinzani upoje, hilo halinihusu. Linalonihusu ni kuona simpigii kura uchwara hata kwa mijeledi baaas!
Bahati nzuri, wendawazimu kama nyinyi mpo wachache nchi hii.
No effect
 
Kama ccm ingekua imefanikiwa kufanya siasa kusingezuiliwa, ukosoaji usingepingwa kwa mtutu wa bunduki na umwagaji damu, vile vile uhuru wa vyombo vya habari usingeminywa.Serikali ambayo haijibu hoja ni serikali iliyojichokea kuhudumia wananchi wake.Kwa hali inavyokwenda sasa hata upinzani hauna haja ya kuweka nguvu kubwa maana nchi imerudi nyuma mno na kila mtu mwenye ubongo kichwani mwake anaona.
 
Tanzania bado hapajakuwa na chama cha upinzani ambacho kina reputation ya maana . Mbaya zaidi tukijaribu kuwashauri wafanye nini ili wawe na comparative advantage ni kama wameziba masikio.
Kilichopo madarakani je kina reputition nzuri? au ndio uma puliza?
Kuna kitu cha maana zaidi ulipaswa kukiandika.
Je ni vyama vya upinzani vinavyochochea utengano, udini na ukabila? Je mikataba mibovu, uuzwaji mashirika ya umma, ukosefu wa ajira, ukosefu wa weledi, upotevu wa uzalendo na kadhalika vyote vinasababishwa na upinzani kukosa nguvu?
Hapo zamani za kale enzi za ujima wa chama kimoja palikuwa na mzee anaitwa Mzindakaya akiitwa mzee wa mabomu! Hakupata hata kunyooshewa kidole wala kuitwa majina ya ajabu baada ya kuibua kashfa ama kupingana na serikali bungeni. Leo hii hatujikumbushi hayo wakati wanaoitwa wapinzani wanapoibua kashfa au kukosoa madudu kwa nia njema... Je imechukua miaka mingapi Wizara ya Nishati na Madini kutenganishwa? Baada ya kugundulika nini? Kwanini waliotoa ushauri ule hawajapongezwa.... Acha tusubiri hati za dharula kwa wazee wa ndiyooooooo.... kwa kwa kwaaa.
sihitaji kuandika zaidi ya hapo.
 
Habari za leo Wanajamvi?

Leo najaribu kuvuta picha ya uchaguzi wa 2020. Nakumbuka kwa umri wangu, na kwa chaguzi nilizoshiriki so far uchaguzi wa 2015 ulikuwa mgumu sana, pengine hata mara kadhaa zaidi ya ugumu wa uchaguzi wa mwaka 1995. Yawezekana ukawa ni uchaguzi wa kwanza mgumu ambao CCM iliona kuna kila dalili za kuondolewa madarakani na kuwa kambi ya upinzani.

Uchaguzi wa 2015 ulihubiri mabadiliko. Ilikuwa ni mabadiliko katika mfumo mzima wa serikali na sekta/idara zake, na katika mfumo wa uchumi ambao ungeleta mabadiliko hata kwa sekta binafsi. Kiufupi yalihubiriwa mabadiliko katika mfumo mzima wa maisha ya wananchi. UKAWA na upinzani wengine nje ya UKAWA walihubiri mabadiliko. CCM baada ya kuona haja hiyo ya wananchi, waliahidi kwamba mabadiliko yaliyotarajiwa na wananchi hao yangeweza kupatikana ndani yake pia. Ilikuwa ni ngumu kuwaamini pengine na kile kilichodaiwa kuwa ni ahadi zisizotekelezeka, lakini mgombea wa CCM Mh. JPM aliwahakikishia wananchi kwamba angewaletea mabadiliko waliyokuwa wakiyatarajia.

Tangu Rais JPM aingie madarakani tumeona mapinduzi makubwa katika maeneo mbalimbali, kuanzia katika nidhamu kwa watumishi wa umma hadi katika mfumo wa uchumi. Tumeona elimu ya msingi ikitolewa bure, uwezo ndani wa ndani wa kugharamia miradi ukiongezeka, rasilimali zikilindwa kwa nguvu zote, na sekta ya uchumi kwa ujumla ikiboreshwa (umeme wa uhakika, usafiri wa reli, barabara, maboresho bandarini, airport, ukusanyaji kodi nk).

JPM anajitahidi sana kwenda beyond expectation, hali inayonifanya nione kwamba wapinzani watakuwa na kibarua kizito cha kuhubiri aina ya “mabadiliko” watakayoyataka, iwapo wataendelea na kauli mbiu hiyo hapo 2020; kwani mabadiliko yamekwisha patikana na yanaendelea kupatikana chini ya serikali ya awamu ya tano.

Iwapo upinzani watahubiri mabadiliko, Je ni mabadiliko gani hayo?

Benmpo
Tunampima kiongozi wa nchi kwa kuangalia hali halisi ya Uchumi wa nchi.
 
2015 kamanda siro alipoka computer za watu pale haki za binadamu ! Kama kweli chama kilishinda kihalali kwanini alipoka! Jpm alipata kura 54000 tu dar nzima kama ile mikono ilikuwa haina maana mbona hasijafika hata laki
Haya sawa, mtashinda kwa kishindo.
 
Itahubiriwa AMANI tu. Maana tuendako Amani inazidi kutoweka.
 
Mabadiliko yaliohubiriwa na kutakwa na wananchi sio yalofanyika......tulihitaji mazingira mazur kwa vijana wengi waweze kujiajir na hii ingetokea pale tu pangekuwa na sera nzur za kiuchumi hususan kuwekeza katka sekta zenye kuajir watu wengi kama kilimo, matokeo yake yamekuwa kinyume.....uchumi unaporomoka, mzunguko wa fedha umeondoka mtaan......Foreign investors hawana amani....kampun nyingi znafanya retrenchment......weny pesa wanaogopa kuinvest.......mdororo wa demokrasia .....siasa za chuki na walio wachache kujiona wafalme hata wasikosolewe hivi vyote n ishara ya mabadiliko yalofanyika n mabadiliko mfu!! Licha ya ukongwe wa CCM Barani Afrika lakn bado ni chama ambacho hakijabalehe kisiasa......2020....Hoja ni mbili tu....ANGUKO LA WATU KIUCHUMI NA MBINYO WA DEMOKRASIA!!
 
Back
Top Bottom