Ccm itapata wakati mgumu kuliko vipind vyote 2020 na kuna uwezekano mkubwa mno wa kuwa ndilo anguko la ccm
Kilimo hoi,njaa kila mkoa,
Kauli za Rais tunazikumbuka sana,
"Mkoa wa kagera kwa nini nyie tu,UKIMWI nyie tu,Mara katerero,Mara tetemeko," huyo ndo rais chief of comfort
Mikopo ya vyuo vikuu danadana,watoto wa maskini sasa hivi ni kawaida kukosa mikopo
Elimu bure,shule haziendi,mfano shule ina wanafunzi 1200,capitation unaletewa laki 3, sasa hivi mitihani ya ndani haifanyiki,na kama wamejitahidi wanaandikiwa ubaon,wakati Kenya wanasambaza laptop mashuleni
Milioni 5o,kila kijiji sasa hivi ni ndoto tena,ccm na serikali yake haitaki hata igusie
Viwanda ,hii Sera ipo kwenye makaratasi na midomoni lakn utekelezaji zero,hii ni sambamba na kilimo kipo hoi
Maji,afya ni shida,nashindwa kuelewa ccm mtakuja na sera ipi,maana mambo yanayowagusa wananchi kwa asilimia kubwa hayaguswi,wamekalia bombardier
Hali uchumi mmoja mmoja duh ,sasa hivi huulizi,ingia tu mtaani na vijijini watakwambia hali ilivyo
Ajira,sasa hivi hakuna ajira,pia watu wengi wanapoteza ajira kwenye sekta binafsi,hii linajieleza
Watumishi wa umma,rais amewakatisha mori wa kufanya kazi, hakuna nyongeza za mishahara ,hata ile kisheria,madaraja hamna
2020 ccm ijiandae kisaikolojia kukabidhi nchi,kizazi kilichopo si kama kilichokuwepo mwaka 1990, hatuli maneno tunataka maisha mazuri,serikali itengeneze mazingira ya vijana kupata ajira au kujiajiri