2015 Mlihubiri Mabadiliko, 2020 Mtahubiri Nini?

Benmpo

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2015
Posts
450
Reaction score
423
Habari za leo Wanajamvi?

Leo najaribu kuvuta picha ya uchaguzi wa 2020. Nakumbuka kwa umri wangu, na kwa chaguzi nilizoshiriki so far uchaguzi wa 2015 ulikuwa mgumu sana, pengine hata mara kadhaa zaidi ya ugumu wa uchaguzi wa mwaka 1995. Yawezekana ukawa ni uchaguzi wa kwanza mgumu ambao CCM iliona kuna kila dalili za kuondolewa madarakani na kuwa kambi ya upinzani.

Uchaguzi wa 2015 ulihubiri mabadiliko. Ilikuwa ni mabadiliko katika mfumo mzima wa serikali na sekta/idara zake, na katika mfumo wa uchumi ambao ungeleta mabadiliko hata kwa sekta binafsi. Kiufupi yalihubiriwa mabadiliko katika mfumo mzima wa maisha ya wananchi. UKAWA na upinzani wengine nje ya UKAWA walihubiri mabadiliko. CCM baada ya kuona haja hiyo ya wananchi, waliahidi kwamba mabadiliko yaliyotarajiwa na wananchi hao yangeweza kupatikana ndani yake pia. Ilikuwa ni ngumu kuwaamini pengine na kile kilichodaiwa kuwa ni ahadi zisizotekelezeka, lakini mgombea wa CCM Mh. JPM aliwahakikishia wananchi kwamba angewaletea mabadiliko waliyokuwa wakiyatarajia.

Tangu Rais JPM aingie madarakani tumeona mapinduzi makubwa katika maeneo mbalimbali, kuanzia katika nidhamu kwa watumishi wa umma hadi katika mfumo wa uchumi. Tumeona elimu ya msingi ikitolewa bure, uwezo ndani wa ndani wa kugharamia miradi ukiongezeka, rasilimali zikilindwa kwa nguvu zote, na sekta ya uchumi kwa ujumla ikiboreshwa (umeme wa uhakika, usafiri wa reli, barabara, maboresho bandarini, airport, ukusanyaji kodi nk).

JPM anajitahidi sana kwenda beyond expectation, hali inayonifanya nione kwamba wapinzani watakuwa na kibarua kizito cha kuhubiri aina ya “mabadiliko” watakayoyataka, iwapo wataendelea na kauli mbiu hiyo hapo 2020; kwani mabadiliko yamekwisha patikana na yanaendelea kupatikana chini ya serikali ya awamu ya tano.

Iwapo upinzani watahubiri mabadiliko, Je ni mabadiliko gani hayo?

Benmpo
 
FB_IMG_1507150289722.jpg
 
Watasema tulinunua [HASHTAG]#BOMBERDIER[/HASHTAG] lakini zilikamatwa.....
 
Tanzania bado hapajakuwa na chama cha upinzani ambacho kina reputation ya maana . Mbaya zaidi tukijaribu kuwashauri wafanye nini ili wawe na comparative advantage ni kama wameziba masikio.

Zaidi sana utaambulia matusi kutoka kwa wafuasi wao
 
democracy

mauaji ya risasi na kuua watu kuwaweka kwa sandarusi

kutetea wasio na elimu

maamuzi ya kijinga

upuuzi wa kugawa madalaka

bado niendeleeeee.............
 
Tanzania. hatuna kitu kinachoitwa "Election" bali tunafanyiwa "Selection" na wenye makali. Huwaga sio matakwa ya wananchi. Kwa style hii watashinda to infinity.
 
Kuna uliyo ya sahau mkuu kubomoa nyumba za watu nje ya sheria kukiuka katiba ya nchi watu kupotelea kusikojulikana IGP kukamata wanao kwepa kulipa kodi ya mapato badara ya TRA madiwani kununuliwa watu wasio julikana kupiga risasi wanaojulikana shughuri za jeshi kuwa za chama tawala mkuu wa mkoa ajue kkk ila dereva wake awe kidato cha nne n.k & n.k ni kweli mabadiliko tayari yameonekana mkuu
 
Habari za leo Wanajamvi?

Leo najaribu kuvuta picha ya uchaguzi wa 2020. Nakumbuka kwa umri wangu, na kwa chaguzi nilizoshiriki so far uchaguzi wa 2015 ulikuwa mgumu sana, pengine hata mara kadhaa zaidi ya ugumu wa uchaguzi wa mwaka 1995. Yawezekana ukawa ni uchaguzi wa kwanza mgumu ambao CCM iliona kuna kila dalili za kuondolewa madarakani na kuwa kambi ya upinzani.

Uchaguzi wa 2015 ulihubiri mabadiliko. Ilikuwa ni mabadiliko katika mfumo mzima wa serikali na sekta/idara zake, na katika mfumo wa uchumi ambao ungeleta mabadiliko hata kwa sekta binafsi. Kiufupi yalihubiriwa mabadiliko katika mfumo mzima wa maisha ya wananchi. UKAWA na upinzani wengine nje ya UKAWA walihubiri mabadiliko. CCM baada ya kuona haja hiyo ya wananchi, waliahidi kwamba mabadiliko yaliyotarajiwa na wananchi hao yangeweza kupatikana ndani yake pia. Ilikuwa ni ngumu kuwaamini pengine na kile kilichodaiwa kuwa ni ahadi zisizotekelezeka, lakini mgombea wa CCM Mh. JPM aliwahakikishia wananchi kwamba angewaletea mabadiliko waliyokuwa wakiyatarajia.

Tangu Rais JPM aingie madarakani tumeona mapinduzi makubwa katika maeneo mbalimbali, kuanzia katika nidhamu kwa watumishi wa umma hadi katika mfumo wa uchumi. Tumeona elimu ya msingi ikitolewa bure, uwezo ndani wa ndani wa kugharamia miradi ukiongezeka, rasilimali zikilindwa kwa nguvu zote, na sekta ya uchumi kwa ujumla ikiboreshwa (umeme wa uhakika, usafiri wa reli, barabara, maboresho bandarini, airport, ukusanyaji kodi nk).

JPM anajitahidi sana kwenda beyond expectation, hali inayonifanya nione kwamba wapinzani watakuwa na kibarua kizito cha kuhubiri aina ya “mabadiliko” watakayoyataka, iwapo wataendelea na kauli mbiu hiyo hapo 2020; kwani mabadiliko yamekwisha patikana na yanaendelea kupatikana chini ya serikali ya awamu ya tano.

Iwapo upinzani watahubiri mabadiliko, Je ni mabadiliko gani hayo?

Benmpo
Usisahau vílevile mapato yameshuka mpaka billion 600.
 
Kuna uliyo ya sahau mkuu kubomoa nyumba za watu nje ya sheria kukiuka katiba ya nchi watu kupotelea kusikojulikana IGP kukamata wanao kwepa kulipa kodi ya mapato badara ya TRA madiwani kununuliwa watu wasio julikana kupiga risasi wanaojulikana shughuri za jeshi kuwa za chama tawala mkuu wa mkoa ajue kkk ila dereva wake awe kidato cha nne n.k & n.k ni kweli mabadiliko tayari yameonekana mkuu

Umekurupuka mkuu, kapangilie vizuri hoja zako na ziwe na ukweli. Toka lini TRA wakawa na power ya ku-arrest?
 
Hukusikiliza habari za IGP leo akiwa mby ITV huwa wanarudia asubuhi ya kesho saa 1:00 itarudiwa tafadhari iangalie ulete mrejesho
 
Msifanye upuuzi umu maisha magumu kipind hiki mnaleta maneno ya matawini hapa, eti mwaka 2020 uyo mungu tuna mipango nae, kama kiama kitakuwa kimesimama je? hebu tafta la kufanya uendeshe maisha yk maneno ya uongo na kweli peleka kwa wakaa maskani wenzako mnokosa la kufanya, OVYOOO, MAWAZO YA KAMPENI KAMA TUNA AHADI NA MUNGU.
 
Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kimfumo ambayo yatapelekea mabadiliko chanya ya kiuchumi, leo hii Magufuli anaongoza nchi kwa mfumo wa One Man Show ambao hatari yake ni kubwa mno maana mihimili yote mitatu inakuwa haitimizi wajibu wake kikatiba na badala yake inafanya kazi kwa maelekezo toka juu (mamlaka ya rais) rejea kauli ya rais Magufuli kwenda kwa mkuu wa mhimili wa Bunge Mh spika Ndugai kuwa wale wabunge wa upinzani ambao ni wakosoaji wakubwa wa serikali awatoe huko ndani ya bunge ili na yeye wakija huku nje ya bunge awashughulikie maana watakuwa hawana kinga ya bunge, rais katika hotuba zake ameenda mbali zaidi kwa kusema wale wakosoaji wakubwa wa serikali (aliowabatiza jina la wasaliti) hawastahili kuendelea kuishi, hivyo tafsiri yake wauliwe. Nchi hii tunahitaji Uhuru wa utendaji kazi katika mihimili ya dola na siyo kuwa na mmoja uliojichimbia ndani ambao uko tayari kuua wale against na Serikali kwa maslahi ya kumtetea mkuu wa nchi. Rais, uchumi wa nchi umemshinda unazidi kudorora kila kukicha, leo mapato ya serikali kupitia TRA ni hoi bin taabani ambayo ni bilioni 600 tu kutoka trioni moja tuliyokuwa tukitangaziwa kila baada ya mwezi mmoja mara baada tu ya utawala wa awamu hii kuingia madarakani, serikali imeamua kuanzisha TRA nyingine kwa jina la Polisi ambao nao wamekuwa wakusanyaji wa mapato na kila mwezi wanatangazia makusanyo yao. Toka kuingia madarakani kwa rais huyu hakuna miradi mikubwa ya maendeleo iliyoanzishwa tofauti na iliyoachwa na rais Kikwete, hivyo rais badala ya kutuletea mabadiliko chanya anatuletea mabadiliko hasi ya kiuchumi, neno mabadiliko Magufuli alilikariri tu kinywani kwenye majukwaa ya kisiasa kipindi cha kampeni kutokana na upepo wa kisiasa ulivyokuwa mgumu kwa ccm pasipo kuwa na mipango mikakati yake, leo hii ukiwauliza hata hao mawaziri kuhusu 'vision 2025' kwa usawia na ufasaha hawaijui.
 
Tanzania bado hapajakuwa na chama cha upinzani ambacho kina reputation ya maana . Mbaya zaidi tukijaribu kuwashauri wafanye nini ili wawe na comparative advantage ni kama wameziba masikio.
Hoja kichekesho hata kwa watoto wa chekechea. Ushauri kutoka lumumba toka lini?
 
Back
Top Bottom