2013 Acha Ushamba Ushamba Wako!!!!! Take Control !!!!!!!!!!!!

2013 Acha Ushamba Ushamba Wako!!!!! Take Control !!!!!!!!!!!!

lara 1

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2012
Posts
15,700
Reaction score
29,190
Wakubwa zangu shikamooni!!!!!!!!!!!!

IGWEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! (Mwaka mpya na salamu jipya)


Kwanza kabisa guys LIKE JF FACEBOOK PAGE TO SUPPORT JF!!!!!!! M pesa imewashinda hata Like tu! Embu make shit happen kule FB banaa sio Kung'aa sharubu kama mmezipiga kiwi!!!!!!! Chama kubwa kama hili vilike vinahesabika, sponsors wakibwaga manyanga mtandao ukafungusha wengi tutakufa na stress ikichanganyika na pressure!!!!!!!!! People show some love jamani na gongea JF like FB (Hata guest mnaochungulia humu linawahusu hili) Hadi viblog mbuzi vinatushinda! Make shit happen people!!!!!!!!!

BACK TO TOPIC

Mwaka ndo unaanza huu mpyaaaaaaaa! Yale mambo yako ya mwaka jana ya kishamba kishamba ya kuwa lonely! Mwenye mawazo! Unhappy! Cha Unyonge! Stress zimekujaa! Unampenda mtu unashindwa kumwambia! Uko na mtu uliemchoka/usiempenda, Umepewa cha mbavu! Mumeo ana cheat! Mkeo huna imani nae! Mkeo ana gubu! Basi ndo mwaka wote huna rahaaa mto wa mwanamke mwenzangu!!!!!!!!! ACHA KABISAAAAA!!!!!! Utakufa mapema bureee!

Kauli mbiu ya mwaka huu ni TAFUTA FURAHA ILIPO!!!!!!!!!!! ITS NOT OKAY KUTOKUWA NA FURAHA!!!!!!!! Hatua ya kwanza tambua nini kinakunyima furahaaa! Then chukua hatua!!!!!!!!! Yafuatayo yatakusaidia kutpata furaha yako!

Kubali tatizo linalokukabili!!!!!!!
Kama umeachwa/ unachitiwa kwa tuhuma za umekuwa Bongisa usiendelee kujidanganya kuwa its okay! It might be okay kwa wenzio wanaume zao wanaopenda minyama bt wako hapendi so its not okay!!!! Anza mazoezi na ndimu hapo! Kama gubu ndo limemfanya arudi usiku wa manane kubali kuwa RAP zako zinamkeraaa! Acha, anza kumbembeleza, Kama mkeo anakusema bahili acha mara moja na pesa ionekane! Kama bia ndo zinaleta gogoro kubali taztizo anza kunywea nyumbani au nenda nae bar!

Regain your self esteem!!!!!
Mara nyingi baada ya kupata makavu live self esteem inakufa kabisaa! Sasa huwezi kurudisha furaha bila kurudisha self esteem! Ni ngumu ila inawezekana!!!!!! Anza kwanza kwa kuboresha muonekano wako! Repea kile kinachokunyima comfidence mwilini mwako! Kama kaka una michunusi tafuta dawa kwa gharama yoyote, kama ni bonge ndimu jamani, kama wembamba umekuzi chips yai isikauke sana! Kama mavazi yako ya kishamba nenda botique upate catalogue! Muonekano wako ni kiungo kikubwa sana cha furaha! People like/hate what they see! Uzuri wako wa ndani hakuna anaeuona!!! Ndo maana i say work on the exterior look! Ukivaa vizuri watu watakuwa wakarimu hata ukimuomba mdada namba anakupa kiurahisi! Na mdada ukifanya wadrobe restructure hata ukipita sehemu watu wakawa wanakusifia comfidence inarudi! Kama shule ndo inakunyima self esteem rudi skonga hujachelewa! (Japo nakubali kuna vitu unreparable kama Ufupi na urefu)

Look things in a positive way!!!!!!!
Smtms vitu vinatunyima raha sababu tuna focus on the negative side na kuignore the postive! "Life consists not in holding good cards but playing well the cards you hold"! by Steve Jobs. Jaribu kutafuta postivity ya jambo linalokunyima raha!! Mfano kazini! Learn to like n accept your job kuliko kukaa kisirani kama utahama kesho na huami wala nini! Labda mumeo kakuchoshaaaa, na hana kazi huna hamu nae kabisaaa! Waza japo hakufai kipesa ila kwa dushelele si haba! Au mkeo kafubaa hadi huna hamu nae, waza huyu tumetoka mbali na ni mama wa wanangu! Utagundua ukiangalia vitu ina a positive way ni rahisi kuvikubali na kuvifurahia tena!

Dare!!!!/Thubutuuuu!!!!!!
Acha woga woga wa kishambaa wa kushindwa kumake things happen!!!!!!! Unampenda mtu hata hujamwambia ushamba wako tu unaanza kujishusha huyu matawi ya juu! Mi mbaya bwana hawezi kunipenda, nina nini cha kumpa? Huyu wa kina flani bwana!!! Na humpati kweli si utani!!!!!! Nani kakuponza? USHAMBA WAKO!!!! Wewe kama una kipenda kitu thubutu kukifata!!! Mungu yupo atakusaidia! Kama mkaka umempenda msalimie, mtanie, atakunotice you never know sio kumchungulia mita 60 usawa wa ukanda wa bahari! Ataoteshwa uko ukumbini hapo? Kama mkaka you want something dare to get it! Kama ni mdada masalimu, make comversation to make your self visible!!!!!!!! Watu tunaowaona special there aint anything special about them just tu wamejitambua na kuelewa what they can do!

Ignore the Society!!!!!!
Jamii mostly ni negative!!!!!!! Kama unahitaji sababu ya kutofanikisha jambo iulize jamii! Ila kama unataka kulifanikisha kaza roho tekeleza! Ukisikiliza jamii utabaki kama jamii ilivo!!!!! Huto make the impossible happen kamwe! Watakupa million reasons usifanya kitu!!!!! Kama ni mwanamme watakwambia mambo laki na ushee kuwa hakufai kabisaaa! Mtaokeo yake mwengine nae hivo hivo! Mwishowe utakuwa huoi wakati wao wanaokushauri wameo siku nyingi!!!!! Hata wadada utaambiwa hana kitu kapuku huyooo! Hakufai unawahi wapi! Mala.ya, amekupendea pesaaa zako! Wao wanakwambia hivo wamo kwenye ndoa zaoooo! Najua jamii yako ni people that you trust but some time you shouldnt have!!! Ndo barrier yako kubwaaa!

HAPPY NEW YEAR !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
nice message lkn wafikiri haya tu yatosha?
 
Yapi mengine tichaaa? Tupe tupe!!!!!!
 
Bonge la insipirational message in an artistic way of presenting!

Hiyo ya society umemaliza, mimi maamuzi yangu makubwa yote huwa nayafanya mwenyewe na ndio maana sinaga wa kumlaumu. Kuna watu hawaendi msalani mpaka washauriwe.

Happy new year!
 
Umenipa ujasiri Lara, ngoja nikafunguke kwa mrembo mtaa wa pili hapa uswahilini. Ntakuja na feed back
 
Sasa nikilike jf page na watu wote hawajui kama mi naijua jf itakuwaje hehehe. Sema nna mpango wa kuuza mbuzi na mie nichangiemo.
Happy new year everyone.
(umbeyaaa, kile kikao cha mamndenyi umewachomokaje? Mi nimewaambia najenga orofa baharini, for the next 5yrs nisiulizwe kitu. Stule ya JK, tumejenga mashuleee (yasiyo na waalimu, maabara wala madawati na vitabu) na mabarabara(yanayobonyeaaa))
 
Sasa nikilike jf page na watu wote hawajui kama mi naijua jf itakuwaje hehehe. Sema nna mpango wa kuuza mbuzi na mie nichangiemo.
Happy new year everyone.
(umbeyaaa, kile kikao cha mamndenyi umewachomokaje? Mi nimewaambia najenga orofa baharini, for the next 5yrs nisiulizwe kitu. Stule ya JK, tumejenga mashuleee (yasiyo na waalimu, maabara wala madawati na vitabu) na mabarabara(yanayobonyeaaa))

Hahahaaaaaaaaaaaa! Kikao kesho! Chupi imenibanaje sasa!
 
mwaka huu nahamia kwenye mitumba hehehehe najua mtanishangaa........
 
Daaah! Ushauri mzuri sana!

Yote hayo ni kutafuta furaha!
Furaha ni kila kitu maishani!

Happy new year lara1
nkugambile?
 
Kijana upo wajameni, mbona unarudi kimyakimya au hutaki hizo gift za TA tugawane? Tunashukuru hata kwa kututakia kheri.
 
Mdau Lara 1 naona umefunguka na message za kutia moyo kwa wale wasiojitambua, nimependa hiyo paragraph ya mwisho maana watu wengi hupenda kufanya vitu kwa kuridhisha nafsi za watu wengine wakati moyoni ana mpango mwingine ambao kama akiamua atafanikiwa lakini anachojali ni jicho la tatu ambalo ni la jamii itamwonaje na mwisho wa siku atakuja kujuta. heri ya mwaka mdau
 
Heshima huu ni mwanzo mwema wa 2013@Lara 1
Kwa unavyojua kujitetea kesho mwenyekiti anapigwa siasa ataishia kukupa hadi nauli zote!
 
sometimes its not about being "mshamba", its about how things are supposed to be at that particular moment and for a specific purpose
 
IGWEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! (Mwaka mpya na salamu jipya)

Kauli mbiu ya mwaka huu ni TAFUTA FURAHA ILIPO!!!!!!!!!!!!!

IGWEEEEEEEEEE!!

Hapo kwenye kutafuta hiyo furaha nayo italeta stress zingine, nadhani itoshe tu watu tujue kuwa "Furaha yako ni wewe mwenyewe"

Ukifurahi na dunia itakufurahia!
 
Back
Top Bottom