OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 419
- 670
Nisiwe mchoyo wa takwimu na data mzee wenu niliyejizika kwenye takwimu. Ndugu zangu 2.6% ya ndoa huvunjika kwa amri ya ndugu. Hizi ni takwimu za NBS ndugu zangu 'The 2021 Social Institutions and Gender Index (SIGI) - Tanzania Survey Report'
Aidha wengi sana wanaachana kwa ugomvi badala ya kukubaliana. Takwimu zinaonesha ni 9.3% ya wenye mahusiano huachana kwa kubaliana kuachana. Wengine huwa ni mawazo ya upande mmoja, yaani aidha mwanamke au mwanaume anaamua kumuacha mpenzi wake. Kimsingi wanaume ndio wanaongoza kwa kuwaacha wanawake bila kusikiliza 45.8% huku wanawake 42.3 ndio huwaacha wanaume bila kuwa na makubaliano.
Wazee sipingi talaka, lakini nadhani ili kuwa na kuachana kwenye maslahi kwa watu wote ni heri kuachana kwa kukubaliana, na isiwe kuacha. Aidha, ndugu wasipewe nafasi kwenye suala la talaka.