1408 bonge la Movie

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,539
3,833
Image may contain: 1 person..Aliujua ubora wake kwenye uandishi..akatengeneza mashabiki wanaopenda kalamu yake..visa vya kutisha ndo vilimuhusudu sana..na ye akalijua hilo..akaliishi..

..Mtindo wake wa uandishi ni wa matukio ya kustaajabisha tu..hata majina ya vitabu vyake ni ya kufikirika kutoka kuzimu..

..Ila si kila watu wana wakipendacho..basi mashabiki walimnyima usingizi kutaka kuonana nae..waandishi wa habari walipenda kujua siri ya mafanikio ya vitabu vyake..

na heshima ikaongezeka na jina likakua..ni Mike Enslin..mwandishi wa Ten Nights in Ten Haunted Houses..

..Alichezea maneno kama Laura Pettie kwenye kiroba cheusi,kuna waliomsifu kwa kupenda utani kuliko Abdul Dunia..

wasomaji waliziona taharuki zilizoendana na mikono ya Hussein Issa Tuwa..na utundu wa lugha kama wamekutana na Maundu Mwingizi kwenye kitanda cha kuwadi

historia pia haikukaa mbali na vitabu vyake...ni kama unamsoma Nihzrath Ntani Jnr akiwa kwenye ubora wake..

..Wasifu wake ulikuwa unampamba kisomi kama Msalaba Bernard..hakuandika sana mapenzi kama Green Osward..japo watu walimwambia ana ucheshi wa Hanifa Kafashe..

...Akasoma gazeti moja na kuona kuwa kuna hotel ambayo inasemekana ina chumba cha ajabu na watu hawakitumii kwa sababu hiyo..

Mike enslin mwandishi anaependa kuchunguza kabla ya kuandika..mtu asieamini katika uchawi wala mizimu japo vitabu vyake vinahusu hivo..akataka kujua siri ya hotel hiyo..

akaandaa jina la kitabu chake kipya..akaenda kutaka kuyaishi mazingira ya kitabu chake hotelini..hakujua..hakujua..

..Aliingia hotelini akaomba chumba alichohitaji..akakataliwa..akauliza kama ye hajulikani pale..akajibiwa we ni maarufu ila hiki chumba hakikujui..

akawaambia nataka niandike kitabu ambacho hata nyie mtakipenda na kinatokana na niliyoyasoma ndani ya chumba hiki..akaonywa..akaonywa tena..

...Akaruhusiwa kwa umaarufu wake..akaingia kuandika kitabu ndani ya Dolphin Hotel on 61st Street in New York City..chumba namba 1408..

..Mwandishi huyu fundi alikialika kifo chake mwenyewe..milango pia ilimruhusu kuingia na sio kutoka..

alilia alipoamini kuwa sasa kitabu kinamponza..aliamua kukubaliana na ukweli na kujuta kwa kutosikiliza na kuweka umaarufu mbele..

..Unataka kujua kama alitoka hai!!..hapana sikwambii..

..waandishi wa vitabu wanapitia mengi sana,kwa wale ambao wanafanya uchunguzi kabla ya kuandika..its a good movie..and inspiration..

#bonge la movie
#1408..
sio lazima kuiangalia kama una ugonjwa wa woga..
credit: Kaisal Ally
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom