12th August Each year

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,324
2,238
Ni siku ya watu wanao tumia mkono wa kushoto (mashoto or left handed).

Nakumbuka nirafiki yangu alikua akipigwa sana na mwalimu pale
alipokua anaandika kwa kutumia mkono wa kushoto,au akinyoosha mkono
wa kushoto kujibu swali.

Pia ilinitokea majuzi tu,mtoto wa rafki yangu alipokua anapokea kitu kwa mkono
wa kushoto nilikataa na nikamlazimisha atumie wa kulia,....

Swali ni je:-
1.ni kwanini tunathamini sana kutumia mkono wa kulia (right handed) ?

obama
bill clinton

wote ni left handed people

inaaaminika watu wa kushoto wanakuwaga na bahati saana,akilli sana...
na baadhi yao wanakuwaga na magonjwa ya akili

Hata mie nimejiuliza, ina connection gani, sie binadamu kuona mkono wa kushoto sio wa heshima?

obama
bill clinton

wote ni left handed people

inaaaminika watu wa kushoto wanakuwaga na bahati saana,akilli sana...
na baadhi yao wanakuwaga na magonjwa ya akili

So,yawezekana kabisa kwamba wale watoto wanavochapwa
kulazimishwa kutumia mkono wa kulia kunasababisha kuwapunguzia confidence

Kiutamaduni tu na mazoea katika kupata picha ya kwamba "shoto" ndio mkono wa kunawishia maeneo yetu yalee
Baada ya haja kuuu..
Tokea hapo unahusishwa sana na uchafu, hii moja.
Pili ambayo hata mimi nashindwa kuelewa (nadhani Genekai atoe muongozo)... kwenye maandishi ya dini!
Mkono wa kuume(kulia, kwa tafsiri iliyozoeleka) ndo upande ambao wapendwa wote wa JEHOVA, kinyume chake mkono wa kushoto yake watakaa wale waliopewa laana...... Kwa upande huu wa kibiblia (samahani sijui kitu kuhusu Quran), nadhani pia nahitaji msaada!

So,yawezekana kabisa kwamba wale watoto wanavochapwa
kulazimishwa kutumia mkono wa kulia kunasababisha kuwapunguzia confidence

hupaswi kumlazimisha mtu kwa hilo
wapo watu wamezaliwa moyo upo kulia pia

Moyo wa binadamu upo upande wa kushoto! Kama tunavyojua, moyo unafanya kazi kubwa sana kwenye mwili wa binadamu!
Kwa watu wengi huu upande huwa weak. Tunashauriwa tusi uoverload upande moyo ulipo!

Moyo wa binadamu upo upande wa kushoto! Kama tunavyojua, moyo unafanya kazi kubwa sana kwenye mwili wa binadamu!
Kwa watu wengi huu upande huwa weak. Tunashauriwa tusi uoverload upande moyo ulipo!

Hahaha,asante sana Rejao,...
nimegundua jukwaa la siasa linafanya tu-define vingine watu lakini kumbe
ni vichwa balaa,...safi sana mkuu

Hata mimi ni left handed, nimeteswa sana utotoni! Halafu ni upuuzi tu, hakuna lolote. Nimeteswa na kunyimwa uhuru utotoni, sasahivi mi najiachia nnavyotaka. Mkono wangu navutia hata bei!

Ni siku ya watu wanao tumia mkono wa kushoto (mashoto or left handed).

Nakumbuka nirafiki yangu alikua akipigwa sana na mwalimu pale

alipokua anaandika kwa kutumia mkono wa kushoto,au akinyoosha mkono

wa kushoto kujibu swali.

Pia ilinitokea majuzi tu,mtoto wa rafki yangu alipokua anapokea kitu kwa mkono

wa kushoto nilikataa na nikamlazimisha atumie wa kulia,....

Swali ni je:-

1.ni kwanini tunathamini sana kutumia mkono wa kulia (right handed) ?

kwa sababu hamuelewi chochote!

kwa sababu hamuelewi chochote!

mm natumia kushoto na ninaelewa vzuri tu! Hizo ni fikra mgando tu na mapokeo ya hovyo kabisa tulizorithishwa na wazee wetu. Kwa kifupi hizo ni fikra za kizee!

First Born; kwa sababu hamuelewi chochote

Si kweli, nadhani na mazingira tuliyolelewa nayo yanachangia. Tulivyokuwa wadogo ukitumia mkono wa kushoto tulikuwa tunachapwa tunalazimishwa tutumie mkono wa kulia. Nikiwa kwa Obama classmates watano niliokuwa nao close wakawa wanatumia mashoto. Ofisi niliyokuwa nafanya 3 akiwemo na CFO wa kampuni walikuwa wanatumia mashoto. Kwa hiyo nadhani ni makuzi tu.

Moyo wa binadamu upo upande wa kushoto! Kama tunavyojua, moyo unafanya kazi kubwa sana kwenye mwili wa binadamu!
Kwa watu wengi huu upande huwa weak. Tunashauriwa tusi uoverload upande moyo ulipo!
Mimi nilikuwa natumia kushoto kufanya kila kitu alkini kwa muda sasa umepungua nguvu na pia nahisi ganzi kwa mbali,nimeshauriwa kutumia mkono wa kulia zaidi na kufanya mazoezi ya uzito kuweka mambo sawa.

mimi ni left hand,sister wangu ni left hand,hupata tabu nikitumia mkasi kukata kitu,inanibidi nitumie right hand.

Mkuu hili ni tatizo kubwa! Vitu vingi vimetengenezwa kwa fikra kwamba wote tunatumia mkono wa kulia. Ni kweli kwamba wengi ni right handed lakini ku generalize ni kuwanyima haki wale wachache. Ninashauri hata mouse za left hand user zitengenezwe pa1 bidhaa zote zinazotulazimisha kutumia mkono wa kulia!

Similar Discussions

Back
Top Bottom