101.4 FM BBC World Service Dar es Salaam

101.4 FM BBC World Service Dar es Salaam

BBC World Service ni bonge la shule kaka.

Mtu yeyote anayeniambia anasikiliza BBC World Service naona kama naweza kuongea naye mambo mengi sana.
 
Hivi tunaanza vipi kuhakikisha hii station inarudi. Mimi siwezi kabisa kusikiliza hizi radio za Bongo. Leo nimejaribu kusikiliza Clouds asubuhi, ni vile vile ilikuwa four years ago mara Bonge sijui nani michosho. Nikafungua moja wanaongea kiingereza nilitambua sauti ya Jimmy Kabwe nikaona wanajadili habari ya kujamba......basi nikazima radio. Bring back BBC english service
 
Tatizo kwetu radio hakuna in taarabu,bongo flavor au spiritual,sisi wengine tunapata taabu tuliozoea kupata world news 24 hrs,sijui itakuaje jamani

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
uko sahihi sana. shida inaanzia hapo. kuna kipindi hadi niliwaza 'hivi niongeze decoder na dish jingine nini?' maana nilinunua tv ya pili niwe naangalia mwenyewe room huku nikiwaacha wao sebuleni na tamthlia zao lakini wapi. decoder ni hiyohiyo moja kinachowekwa sebuleni na we2we huko chumbani ndo hichohicho uangalie. sasa watoto wanataka katuni zao na vipindi vyao vya ajabuajabu. mama anataka tamthlia. wakati huohuo arsenal na liverpool zinacheza baba ninataka hapo au nataka kuangalia dunia inakwendaje kupitia sky news inakua shida kubwa sana. unaamua kuwaacha unatoka unakwenda bar kuangalia mpira huku home umelipia full ili uwezage kuangalia mpira. hapo umeongea suala linalonikwazaga sana yani. lakini sasa solution yake ni expensive sana. utakuaje na dstv mbili kwenye nyumba moja.
Yaani ni shiida! Kuna kitu wanaita Dstv Etra View kama sikosei unaongezea 45,000 lkn kwa usawa huu hiyo sio hela ndogo!
 
Binafsi pia nimesikitishwa sana na kuchukuliwa kwa masafa ya 103.3 FM ambayo yamekuwa yakitumiwa na BBC World Service masaa 24 kila siku kwa muda mrefu hapa Dar.

Kuwepo kwa radio ya muziki tu masaa 24 si wazo baya, ishu ni kwa nini iwe hayo masafa ya 103.3 FM katika listi ya redio zaidi ya 20! Very disappointing!

Tangu 2014 BBC idhaa ya Kiswahili wamekuwa na ofisi hapa Dar na wao BBC World Service wamo karibu miji mikubwa yote Afrika achilia mbali duniani kote.

Sikutegemea kwa kweli 103.3 FM ichukuliwe na broadcaster mwingine (Kusaga & Co.) isipokuwa kama BBC World Service wana mpango wa kuamia mawimbi mengine tofauti - I hope so!
 
Hivi tunaanza vipi kuhakikisha hii station inarudi. Mimi siwezi kabisa kusikiliza hizi radio za Bongo. Leo nimejaribu kusikiliza Clouds asubuhi, ni vile vile ilikuwa four years ago mara Bonge sijui nani michosho. Nikafungua moja wanaongea kiingereza nilitambua sauti ya Jimmy Kabwe nikaona wanajadili habari ya kujamba......basi nikazima radio. Bring back BBC english service
Hivi kuna mtu alishajaribu kuwasiliana nao (BBC) wakalitolea majibu? Nafkiri tuanzie hapo
 
Duh kumbe wadau wa BBC tupo wengi!! Mawazo yangu yote nmekosea frequency kumbe ishachukuliwa na classic FM!! dah yaani mara kumi redio zote zingezimwa ila sio BBC ntakosa mengi sana
 
Wakuu nimepata solution hapa ni kutumia app yao ya BBC radio inakuwa na radio za BBC zote zipo kama 20 hivi na haili MB sana kma nilivyofikiri huwa nasikiliza usiku kucha najikuta mpka naamka inaongea tu ila MB zilizokwenda hazifiki hata 100 kwa masaa yote hayo so ni bora muipakue hiyo app at least mnakuwa updated na habari za dunia 24/7 kuliko hizi radio zetu zenye uswahili mwingi
Screenshot_2018-05-27-14-29-36.png
Screenshot_2018-05-27-14-29-19.png
 
Back
Top Bottom