10,000 vs 200,000 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

10,000 vs 200,000

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by oba, Dec 4, 2011.

 1. oba

  oba JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huwezi amini, yule dokta bingwa wa mifupa pale MOI, KCMC, BUGANDO, MBEYA na kwingineko anapokuwa zamu for 24 hours posho yake ni 10000 na mbunge anapokuwa bungeni for tha day hours anazokuwa mjengoni posho yake ni 200000. Dokta huyu aweza kushinda amesimama theta kwenye operation, wakati mwingine huutumia usiku pia kuwatibu wagonjwa wa dharura.
  Huu uwiano wa 1:20 unavunja moyo wa kazi na sidhani kwamba hawa watumishi wa afya watafanya kazi kwa moyo huku keki ya taifa ikigawanywa kihuni namna hii.
  Nawasilisha!
   
 2. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ndio maana wataalamu wetu wengi wanakimbilia siasa maana ndio inayolipa
   
 3. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  huyo dokta anaitwa nani maana ana bidii sana yaani anaweza akawa MOI, KCMC, BUGANDO na MBEYA halafu anakula buku 10 tu... weka na namba yake ya sim...
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  job true true bongo tabu kweli mwanasiasa yupo juu kuliko mtaalamu..:shock:
   
 5. King2

  King2 JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Watanzania si Mazuzu!! acha tu muibiwe!
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Dah, kweli huo uwiano unatisha.
  Yani bongo anaejishughulisha zaidi anapata chini ya asiyejishughulisha. No wonder watu wanaona bora kubeba mabox ulaya kuliko kuja bongo sehemu ambayo haithamini taaluma na kujituma kwa watu.
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  Ma specialist wengi kuwaona tunalipia sh 10 000 hembu fikiri atibu wagonjwa 20 ndipo amfikie mbunge!wito dr.shafiq,masawe,ekenywa,prof matuja,mbise,ndosi,kaushik hamieni kwenye siasa mtuache wagonjwa tufe
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,689
  Likes Received: 82,553
  Trophy Points: 280
  Kuna daktari mzuri sana wa magonjwa ya moyo. Huyu alikuwa anasoma US na baada ya kumaliza alipata kazi nzuri sana US lakini akaamua kurudi nyumbani ili kusaidia Wagonjwa wa moyo kwa bei poa kabisa ukilinganisha na bei ya kuwapeleka India kwa matibabu. Akajinyima na pesa zake kununua vifaa muhimu alivyohitaji kama Daktari wa magonjwa ya moyo na wengi walimpa misaada baada ya kuwafahamisha alichokusudia kukifanya.

  Aliporudi nyumbani kutaka kuanzisha hospitali yake alipigwa vita sana na wengine Wizara ya afya kumuomba hata rushwa eti wamsaidie kufungua hospitali yake, hatimaye alishindwa kufanikisha lengo lake, sijui aliishia wapi yuke Dr. Wacha watu watafute kazi nchi za nje ambapo wanafanya kazi kwa raha zao, kulipwa ujira unaoendana na taaluma zao na pia kupewa vitenda kazi muhimu vinavyohitajika katika taaluma zao.

  Mwaka jana nilipata bahati ya kupita mahala ambapo yule Dr alikuwa afungue hiyo hospitali ya wagonjwa wa moyo (Dar) ikiwemo kuwafanyia upasuaji wale ambao walihitaji huduma hiyo. Hapakuwa na dalili ya uhai maana jengo lilikuwa limezungukwa na pori si la kawaida. Sijui kama aliamua kurudi US au kwenda nchi nyingine au alifungua mahali pengine nchini.

   
 9. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #9
  Dec 4, 2011
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa hapo dr. Akipasua kichwa badala ya mguu atalaumiwa?
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Bongo hovyo sana,sijui lini tutabadilika.
   
Loading...