Ushauri gani ulipewa na mzazi, iwe ni baba au mama, ukaufuata na umekusaidia kufika mpaka hapo ulipo?
Naanza:
“Atayekulisha ni mwema, ila utampa pia uwezo wa kukulaza njaa wakati wowote atakapoamua - jishughulishe na hakikisha hauwi tegemezi”. Ushauri kutoka kwa baba yangu (Mungu amrehemu)...