Mnamo tarehe 06.03.2022 majira ya saa 02:00 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako huko Kata ya Chimala, Tarafa ya Ilongo Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya na katika msako huo alikamatwa mtuhumiwa EMANUEL MSIGALA [42] Mkazi wa Uyole – Mbeya akiwa amepakia na kusafirisha vipodozi...