uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. M

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 ACT Wazalendo: Mchakato wa uchaguzi uliharibiwa na tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC). Tutakwenda mahakamani

    Chama cha ACT Wazalendo kimesema kimejipanga kuchukua hatua za Kisheria kwa kile wanachodai kuwa ni kudai haki ya ushindi walioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Kauli hiyo imetolewa na Mnadhimu wa Kambi rasmi ya Upinzani katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Profesa Omar Fakih, wakati...
  2. JamiiForums Tanzania PostGE2025 Ijengwe minara kuwaenzi waliouawa kipindi cha uchaguzi mkuu 2025

    Hakuna namna nyingine sahihi sana ya kuwaenzi hawa zaidi ya kuwajengea minara katika mikoa husika. Mnara mkuu utawekwa Dar Es salaam. Utaitwa mnara wa pili wa mashujaa. Kisha kila mkoa ambao.palitokea mauaji ya halaiki pajengwe mnara kisha majina yote ya waliouawa yawekwe hapo. Kadhalika picha...
  3. JamiiForums Tanzania Kufanya maridhiano na wauwaji na wezi ni kuutunuku mauwaji na wizi wa uchaguzi uliofanyika

    Kufanya maridhiano na wauwaji na wezi ni kuutunuku mauwaji na wizi wa uchaguzi uliofanyika . point ni zile zile, uchaguzi bandia ufutwe, mateka wote waachiliwe, katiba mpya tukutane tarehe 9/12
  4. R

    JamiiForums Tanzania Upinzani Cameroon yatoa saa 48 kuachiliwa kwa wote waliokamatwa kwenye Maandamano ya Uchaguzi 2025

    Upinzani nchini Cameroon unaendelea kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika hivi karibuni Mgombea wa urais wa chama pinzani aliyeibuka mshindi wa pili, Issa Tchiroma Bakary, ametoa masaa 48 ya mwisho kwa mamlaka za nchi hiyo kuwaachia huru wote waliokamatwa wakati wa maandamano...
  5. JamiiForums Tanzania PostGE2025 Jaji Mwambegele ameuweka rehani ujaji wake kwa uchaguzi wa kupikwa!

    Jaji Jacobs Mwambegele sasa hivi lazima atatembea kichwa chini popote atakapokwenda. Simply put, Uongo ni dhambi. Kutengeneza majedwali ya uchaguzi ambayo hata yeye mwenyewe hayaamini, lakini akayatangaza, imempunguzia heshima mbele ya jamii. Kiongozi wa nje kuyadharau matokeo haya ya uchaguzi...
  6. JamiiForums Tanzania GE2025 ACT Wazalendo: Serikali ya Rais Samia imekosa uhalali wa kisiasa kuendelea kuongoza Tanzania, uchaguzi wa Oktoba 29 ni pigo kwa Demokrasia na taifa

    MSIMAMO WA ACT WAZALENDO KUHUSU MWENENDO NA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU 2025 Chama cha ACT Wazalendo kupitia kikao cha Kamati ya Uongozi Taifa kilichoketi 7 Oktoba 2025 kimefanya tathmini ya kina kuhusu mwenendo na matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025 ambao umekuwa pigo kubwa...
  7. JamiiForums Tanzania Ushahidi: Jinsi CCM "walivyoshinda uchaguzi" kwa kishindo cha 98%

    Mbinu zilizotumika kwenye "uchaguzi" wa mwaka 2020 ndizo walizopanga kuzitumia pia mwaka 2025. Lakini safari hii liliwakuta jambo ikabidi wabadili gea angani. Mwaka 2020 wasimamizi wa vituo waliletewa matokeo ya bandia na ARO Kata wakati upigaji wa kura halali ukiendelea. Hizo kura za mchongo...
  8. JamiiForums Tanzania Kipi Kifanyike Nchini Tanzania Baada ya Vurugu za Uchaguzi na Maandamano Yaliyosababisha Vifo?

    Kufuatia vurugu za uchaguzi na maandamano yaliyosababisha vifo nchini Tanzania, hatua madhubuti zinahitajika kuchukuliwa ili kurejesha amani, utulivu, na kuimarisha demokrasia. Hali kama hii mara nyingi huashiria mgogoro wa kisiasa na kijamii unaohitaji mbinu za kina na shirikishi kushughulikia...
  9. JamiiForums Tanzania GE2025 Larry Madowo: Nimetumiwa mamia ya video, baada ya wiki kadhaa tutatoa ripoti ya Uchaguzi wa Tanzania

    "Nimetumiwa mamia ya video, nimeongea na watu wengi wakiwemo waandishi wa habari, baada ya wiki kadhaa tutatoa ripoti ya uchaguzi wa TZ." - Larry Madowo
  10. T

    JamiiForums Tanzania Je, Tanzania bado ni salama kuwa mwenyeji wa AFCON 2027 baada ya matukio ya uchaguzi mkuu?

    AFCON 2027 Nitashangaa sana kuona CAF inaicha Tanzania kuwa mwenyeji wa AFCON 2027 baada ya yote yaliyotokea Nashauri CAF waiondoe Tanzania mapema kabisa katika nchi mwenyeji wa AFCON 2027
  11. W

    JamiiForums Tanzania Balile alipanick Media za Tanzania kupewa taswira ya toilet paper kabla ya uchaguzi. Mbona sasa hivi yuko kimya?

    Mwezi Julai 2025, aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM na kipindi cha Power BreakFast, Masoud Kipanya, alichora Cartoon ambayo mtu yupo chooni alafu Toilet paper imeandikwa MEDIA, akiwa na maana kuwa Media zinatumika vibaya kwa maslahi ya wachache na si kwa maslahi ya jamii nzima kutokana na...
  12. JamiiForums Tanzania PostGE2025 Tume Uhuru ya Taifa ya Uchaguzi INEC yatoa orodha wabunge viti maalum CCM wapo 113, CHAUMMA 2

    Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa orodha ya majina ya wabunge wanawake wa viti maalum 115 kati ya 116, huku ikibakiza nafasi moja ambayo jina litatangazwa baada ya kufanyika uchaguzi jimbo la Fuoni na jimbo la Siha uliohairishwa. Katika orodha iliyotolewa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepata...
  13. A

    JamiiForums Tanzania Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ili kulinda hadhi yake na Majaji wengine ajiuzulu

    Kufuatia kufanyika Kwa uchaguzi, ambao haukukidhi viwango vya Haki. Ni vizuri Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, anajiuzulu na kuyakana haya matokeo. Na Majaji wakatae teuzi kwenye vyombo ambavyo, hawa taweza kufanya kazi ipasavyo kama hakuna mabadiliko ya Sheria yatakayo wawezesha kufanya...
  14. JamiiForums Tanzania PostGE2025 Mnyika, Japo Uchaguzi Sio Huru, Wa Haki na Halali, lakini Usimwite Rais Haramu!. Baada ya Kuapishwa ni Rais Halali Kisheria japo Sio Ki Haki!

    Wanabodi, Tanzania tuna changamoto kubwa sana ya kutafsiri sheria, kuna tofauti kubwa kati ya uhalali wa kisheria na haki ni vitu viwili tofauti. Mimi japo ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea, ila pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, ila sio wakili wa...
  15. M

    JamiiForums Tanzania GE2025 Waangalizi wa AU: Uchaguzi wa Tanzania ulivurugwa

    Waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Afrika wamesema kwamba uadilifu wa uchaguzi mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29 uliathiriwa, wakitaja matukio ya kujazwa kwa kura katika vituo kadhaa vya kupigia kura. Ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa umoja huo ulisema hapo jana waangalizi wake walishuhudia...
  16. K

    JamiiForums Tanzania Haya ndiyo matumizi ya Tsh 600B za uchaguzi!!! Tusishangae vijana kuchoma nchi

    Wakati vijana wanamaliza vyuo na mikopo, nchi nayo inakopa sio kwa kuwasaidia vijana wetu bali inakopo na kutumia pesa kununua ma range rover , VX na chaguzi kama hizi. Serikali imetumia Tsh Billion 600 kwenye huu uchaguzi ambao tumeona waziwazi kura zinaibiwa, kura hata hazijahesabiwa, vurugu...
  17. JamiiForums Tanzania GE2025 Maandamano na Vifo Uchaguzi 2025: Polisi waonya kuhusu kusambaza “Picha na Video zenye kuleta taharuki”

    Polisi Tanzania wameonya wananchi kuepuka kusambaza picha mtandaoni ambazo “zinaweza kusababisha taharuki” kufuatia kurejeshwa kwa huduma ya intaneti baada ya maandamano yaliyoibuka kutokana na uchaguzi. Baada ya internet kurudi, video na picha zilizosambaa kwenye mitandao ya Kijamii zinaonesha...
  18. JamiiForums Tanzania GE2025 Media za Tanzania zilivyoripoti matukio ya Uchaguzi Mkuu 2025; Je, tatizo ni uwezo wa Wanahabari au uhuru umesiginwa?

    Wakati Uchaguzi Mkuu wa Tanzania ulipofanyika tarehe 29 Oktoba 2025, huku Huduma za Mtandao wa Intaneti zikiwa zimezimwa, Vyombo vya Habari vikuu (Mainstream Media) kama televisheni na redio, pamoja na Vyombo vya Habari vya Mtandaoni, vilitarajiwa kutoa taarifa sahihi na zenye uwiano kuhusu yale...
  19. K

    JamiiForums Tanzania Obama alisema kuhusu uchaguzi

    https://youtu.be/nxFeUMLXz8s?si=sl2tKt4ZiZ006nNV
  20. R

    JamiiForums Tanzania GE2025 Hasira za wananchi kwa Media za Tanzania kukaa kimya kuhusu Mauaji na vurugu zilizokuwa zinaendelea Uchaguzi Oktoba 29

    Media za Tanzania zinapaswa kulaumiwa sanaa kwa kilichotokea na kinachoendelea kutokea haiwezekani media za nje ndiyo zitoe ripoti kuhusu maovu na mauaji yaliyotokea kwa vijana wetu, uchafu unaofanywa na serikali ya huyu mama lakini media za ndani zipo kimya kazi kupaka mafuta Kwa hali hii...
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…