Mgombea Urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan, akizungumza katika kampeni za Uchaguzi Mkuu katika eneo la Dakawa, Mvomelo, Mkoa wa Morogoro leo, tarehe 30 Agosti 2025, amesema lengo la Serikali ni kuona Tanzania ikijitegemea kiuchumi kufikia mwaka 2050, bila kutegemea mikopo mikubwa kutoka nje...