onesmo olengurumwa

Onesmo Olengurumwa
Onesmo Kasale Olengurumwa ni wakili msomi, ambapo alizaliwa mwaka 1980, katika kijiji cha Sakala, Kata ya Ogosorock, Loliondo, Wilayani Ngorongoro.

ELIMU

Onesmo alisoma katika Shule msingi sakala, na badaye alisoma masomo ya Sekondari katika shule ya Sekondari ya Arusha Catholic Seminary kwa kidato cha kwanza hadi cha 4 "O Level". Onesmo aliendelea na Elimu ya A level katika Shule ya Sekondari ya Dakawa Morogoro ambapo alisoma kidato cha 5 na 6 mwaka 2004

Onesmo Kasale Olengurumwa, ana digrii 2, ambapo ya kwanza ni digrii ya sheria toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na digrii ya pili ya uzamivu katika maswala ya utafiti na sera za umma (Masters in Research and Public Policy) chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Onesmo, kitaaluma ni wakili wa Mahakama kuu Tanzania baada ya kuhitimu katika Chuo cha mafunzo kwa Vitendo kwa wanasheria (Law School of Tanzania). Lakini pia amesoma kozi mbalimbali za haki za binadamu, sheria na utawala ndani na nje ya Tanzania.

FAMILIA na MAKAZI

Onesmo, ana familia, mke na watoto, makazi yake kwa sasa yapo Jijini Dar es Salaam na kijijini Sakala Loliondo.

KAZI

Wakili Msomi Onesmo Kasale Olengurumwa, amekuwa akifanya kazi za utetezi wa haki za Binadamu toka akiwa Chuo kikuu ambapo alikuwa Rais wa Chama cha Haki za Binadamu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Onesmo Olengurumwa aliwahi kufanya kazi katika Kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC) Kati ya mwaka 2010-2012.

Kwa sasa Wakili Msomi Onesmo Olengurumwa ni Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

USHIRIKI KATIKA MASUALA YA KIJAMII

Onesmo Olengurumwa, amekuwa Mtetezi wa muda mrefu wa haki za binadamu hapa Tanzania, ambapo anafahamika sana kwa misimamo yake katika masuala ya utetezi wa haki za binadamu na sheria. Amezunguka nchi nzima kusikiliza na kutatua changamoto za Watanzania wenye changamoto za haki zao.

Wakili Onesmo, ameshiriki na kujishughulisha kwa kiasi kikubwa katika kutetea haki za wanangorongoro hasa masuala migogoro ya ardhi. Amekuwa mstari wa mbele katika kuwaongoza na wakati mwingine kuwasemea wanangorongoro katika migogoro mbalimbali inayowakumba kwa miaka mingi.

SIASA na UONGOZI

Wakili Onesmo Olengurumwa amekuwa mwanachama na kada wa CCM toka 2005

Mwaka 2008 hadi 2012 alikuwa mjumbe wa Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha, kutokea Wilaya ya Ngorongoro,

Wakili Onesmo, pia aliwahi kugombea Uwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ngorongoro.

Wakili Msomi Onesmo Olengurumwa, kwa sasa ni Mkurugenzi wa THRDC

Wakili Msomi Onesmo Olengurumwa, Aliachana shughuli za kisiasa toka Mwaka 2010 na kujikita katika masuala ya utetezi wa haki za binadamu.

Hakuwahi kugombea nafasi yoyote ya kisiasa baada ya kuacha UVCCM mwaka 2012, Hata hivyo Wakili Onesmo amekuwa karibu sana na siasa za Ngorongoro kama mshauri wakati wa uchaguzi na katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo na kijamii.

Wakili Onesmo, ni mtu anayeipenda sana Wilaya yake ya Ngorongoro na watu wake, ambapo amekuwa msaada katika masuala mbalimbali ya kijamii na watu binafsi wanaopata changamoto za kisheria, ikiwa ni pamoja na kusaidia kwenye kesi mbalimbali.
  1. McLaren

    PostGE2025 Onesmo Olengurumwa wa THRDC: Kuna waliokamatwa kwenye maandamano ambao ni chini ya miaka 18. Tunashauri waliokamatwa wote waachiwe

    Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umetoa wito wa kuachiliwa huru kwa watu wote waliokamatwa au kushikiliwa kutokana na tuhuma zinazohusiana na Uchaguzi Mkuu wa 2025 Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, amesema tathmini ya awali inaonyesha kuwa zaidi ya...
  2. Mafyangula

    POTOSHI Olengurumwa: Katiba mpya inakwamishwa na CCM mtandao wanaonufaika na mfumo

    Wakuu Je, Olengurumwa aliyasema maneno haya au amemezeshwa? kwamba Katiba mpya inakwamishea na CCM mtandao wanaonufaika na mfumo.
  3. R

    GE2025 Wakili Olengurumwa: Amani ya nchi inalindwa kwa uwepo wa Misingi ya Demokrasia na Kusikiliza kero na Vilio vya Wananchi

    Wakili Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), amesema kuwa msingi wa kulinda amani ya nchi upo katika kujenga na kuimarisha misingi ya kidemokrasia na usawa wa kijamii na si vinginevyo Akizungumza na mtangazaji Wilberforce Ngoto...
  4. DuaZaMama

    GE2025 Olengurumwa: Harakati za Gen- Z ni sehemu ya historia ya demokrasia

    Wakili Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), amesema harakati za vijana na maandamano ya kudai haki si jambo jipya, bali ni mwendelezo wa historia ndefu ya mapambano ya kidemokrasia duniani. Akizungumza katika kipindi cha Maswali na...
  5. DuaZaMama

    GE2025 Wakili Olengurumwa: Katiba mpya inakwamishwa na wanaonufaika na mifumo iliyopo

    Wakili Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), amesema kuwa changamoto ya kupata Katiba mpya inachangiwa na watu wachache wanaonufaika na mifumo iliyopo na hivyo kuona mabadiliko kama tishio kwa masilahi yao binafsi. Akizungumza na...
  6. Mkalukungone Mwamba

    GE2025 Olengurumwa akosoa tamko la Mawakili wa Serikali kwa Kupinga Uamuzi wa TLS Kuhusu Maandamano ya Mawakili

    Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa, amekosoa tamko la Chama cha Mawakili wa Serikali (PBA) lililopinga uamuzi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kuwataka wanachama wake kuandamana nchi nzima kulaani tukio la kukamatwa kwa...
  7. Roving Journalist

    GE2025 Olengurumwa: Tamaa ya Fedha Kipindi cha Uchaguzi Inatufanya Tukose Viongozi Bora

    Wakili Onesmo Olengurumwa, ambaye ni Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), amesema kuwa tamaa ya kupokea fedha zinazotokana na rushwa wakati wa uchaguzi imekuwa chanzo kikuu cha Taifa kukosa viongozi bora. Amewahimiza wananchi kuachana na tamaa ya fedha...
  8. Roving Journalist

    Wakili Onesmo Olengurumwa: Kama Urais una ukomo, Ubunge pia uwe na ukomo

    Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa amesema ili kuongeza vijana kwenye nafasi za maamuzi ni vyema mbunge wa kuchaguliwa akaruhusiwa kuongoza kwa vipindi vitatu pekee(miaka 15) kisha baada ya hapo asigombee tena. Olengurumwa ameeleza...
  9. R

    PreGE2025 Olengurumwa: Ubunge uwe na ukomo wa miaka 15, vijana wapewe nafasi ya kushiriki siasa za nchi yetu

    Mbunge wa kuchaguliwa asizidi vipindi vitatu vya miaka 15 maana yake nini ni miaka 15 kama mbunge umeshindwa kutekeleza kwa wananchi utafanya nini? “Ubunge uwe na ukomo wa miaaka 15 vipindi vitatu maana yake ni nini kwa mtu ambaye alikuwa mbunge 2010, 2015,2020 maana yake huu ungekuwa uchaguzi...
  10. I

    PreGE2025 Olengurumwa : Tuwe na tume maalum ya kudumu ya kuchunguza matukio ambayo vyombo vya usalama vinatuhumiwa "wasijichunguze wenyewe"

    Kufuatia taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa May 4, 2025 kuhusu kufuatilia na kuchunguza tuhuma zilizotolewa na Mwananchi (ambaye jina lake linaendelea kufuatiliwa) kupitia Mitandao ya Kijamii, akiwatuhumu askari Wawili kuwa walimfuata kumtaka afanye nao kazi ya kijajusi huku wakitaka...
  11. Poppy Hatonn

    Olengurumwa asimulia alichoambiwa na Padre Kitima baada ya kumtembelea hospitali

    Kwa mazungumzo niliofanya naye ni kwamba, jana aliweza kuitisha vikao kwa viongozi wa dini zote kwaajili ya kutafakari ya jumbe zao walizozitoa wakati wa Idd na Pasaka na walikuwa viongozi trakibani 100 na wakamaliza vikao vyao salama na ndipo baadae jioni wakati anakwenda msalani katika eneo la...
  12. Roving Journalist

    PreGE2025 Onesmo Olengurumwa: Sina uhakika kama Watu wengi wanafahamu kuhusu Uandikishaji

    Wakili Onesmo Olengurumwa (Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania - THRDC) anasema: Hamasa ya Undikishaji imekuwa ndogo kwa kuwa utaratibu wa kuhusisha Wadau umekuwa mdogo, sina uhakika kama Watu wengi wanafahamu kuhusu Uandikishaji, zoezi linaweza kupita na Watu wakakosa...
  13. Mkalukungone Mwamba

    PreGE2025 Olengurumwa ataka mjadala wa Kitaifa kabla ya kugawa majimbo ya Kiuchaguzi

    Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Kutetea Haki za Binadamu (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa amesema utaratibu wa ugawaji majimbo unaotumika kwa sasa sio sahihi hivyo vigezo vinavyotumika viboreshwe au kuangaliwa upya kabla ya ugawaji wa majimbo utakaofanyika mwaka huu. Kupata matukio na...
  14. Q

    Onesmo Olengurumwa: Rais bado anayo nafasi ya kukaa na CHADEMA kusitisha maandamano kwa amani.

    Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Wakili Onesmo Olengurumwa akizungumza na televisheni ya mtandao ya Sauti Digital. "Sisi tulidhani na tulishauri sana kwamba serikali iwasikilize (CHADEMA), wawape ile fursa ya mazungumzo na bado tunaendelea kushauri...
  15. B

    Wakili Onesmo Olengurumwa ashinda kesi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

    29 July 2024 Mahakama ya Rufaa Tanzania Dar es Salaam, Tanzania Kesi ya Onesmo Olengurumo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Tanzania https://m.youtube.com/watch?v=M89ro2AWtds Mahakama ya Rufaa Tanzania yatengua hukumu ya Mahakama Kuu katika kesi ya msingi iliyofungiliwa Mahakama Kuu kupinga ...
  16. Q

    Olengurumwa: Uhaini waliopewa akina Dkt. Slaa unatia doa taifa na taswira ya Rais

    Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa amesema. Pamoja na serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu kupongezwa na wadau mbali mbali wa haki za binadamu katika maeneo mengi ikiwemo kutoa uhuru wa kujieleza na kutoa maoni uhuru, sakata la...
  17. N

    THRDC: Sheria na sera zipitiwe kubaini kama makundi ya watu wenye uhitaji maalum hayaachwi nyuma kidigitali

    Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa amesema kuna umuhimu wa kutafakari kwa mapana kauli mbiu ya Siku ya Wanawake kwa mwaka 2023 isemayo “Ubunifu na mabadiliko ya teknolojia: Chachu kuleta usawa wa Kijinsia” ili katika utekelezaji...
  18. The Sheriff

    Olengurumwa: Huenda baadhi ya ripoti za tume na kamati zinazoudwa hushindwa kuwekwa wazi kwa sababu ya hofu

    Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za binadamu Nchini (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa ametoa maoni kuwa uenda baadhi ya ripoti za Tume na Kamati mbalimbali ambazo huundwa kuchunguza masuala mbalimbali ushindwa kuwekwa wazi kwa kuwa taarifa zinaweza kuwa zinawagusa wenye mamlaka...
Back
Top Bottom