mwenge wa uhuru

Mwenge wa Uhuru
Mwenge wa Uhuru una muundo wa tochi ya mafuta ya taa ambayo inaashiria uhuru na mwanga. Mwenge wa uhuru ulinyanyuliwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro mnamo Desemba 9, 1961 na shujaa Brigedia Alexander Nyirenda ikiashiria kuangaza nchi na kuvuka mipaka kuleta matumaini palipo kukata tamaa, upendo palipo uadui na heshima palipo chuki.

Sababu ya huyu brigedia kunyanyua mwenge huu ni kuonesha fahari ya nchi na pia kuleta matumaini kwa Watanzania wote kwa kutokata tamaa, kupendana, kuheshimiana na kutogombana ikimaanisha kuwa na ushirikiano.

Mbio za Mwenge wa Uhuru hufanyika kila mwaka kuanzia maeneo mbalimbali nchini.
  1. B

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Susan Lyimo: Jambo pekee ambalo CCM wamebaki nalo ni kukimbiza mwenge mchana, wanadai unaleta amani basi waupeleke Congo

    Susan Lyimo Mwenyekiti wa BAZECHA amesema kuwa jambo pekee ambalo CCM wamebakiwa nalo ni kukimbiza mwenge mchana huku wakidai unaleta amani basi waupeleke Congo ukalete amani huko. Aidha amewataka wanaoitwa mabalozi huko vijijini huku wakiwa na bendera za CCM juu ya nyumba zao kuukuu...
  2. B

    JamiiForums Tanzania Kikwete aeleza umuhimu wa mwenge wa uhuru kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Mwenge wa Uhuru ni moja ya Tunu kubwa iliyopo kwenye Taifa kwani umekua kichocheo kikubwa cha maendeleo kwenye Taifa ikiwemo kuchochea mapambano dhidi ya ujinga, maradhi na umaskini kila...
  3. Mindyou

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Michael Msechu aingia Pwani kuhamasisha wananchi kuhusu ujio wa Mwenge wa Uhuru na amani kipindi cha Uchaguzi

    Balozi wa Mazingira na mhamasishajI Michael Msechu amehamasisha wakazi wa Mkoa wa Pwani kuhusu ujio wa Mwenge wa Uhuru wa Kitaifa 2025 na kuhamasisha umoja na maendeleo ya Miaka minne ya Rais Samia katika kukuza upendo na umoja miongoni mwetu. Soma pia: Mhamasishaji Peter Msechu aanza ziara...
  4. upupu255

    JamiiForums Tanzania Mwenge wa Uhuru 2025 kuzinduliwa Mkoani Pwani

    Mkoa wa Pwani umeteuliwa kuwa mwenyeji wa shughuli ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 zitakazozinduliwa Aprili 2, mwaka huu katika Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha Pwani sherehe zitakazohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, mikoa jirani na wilaya zote za Mkoa wa Pwani pamoja na...
  5. Cute Wife

    JamiiForums Tanzania Mwenge wa Uhuru wafikishwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, waimba Wimbo wa Taifa

    Wakuu, Mbio za mwenge zilihitimishwa tar 14, Oktoba na wakimbiza mwenge huo kutakiwa kukamilisha zoezi hilo kwa kufika katika kelele cha mlima huo pamoja na kuweka bendera ya taifa. Wajuba walikamilisha zoezi na hapa wanaimba wimbo wa taifa kwa uzalendo mkubwa uliotukuka! Pia soma: Rais...
  6. President of China

    JamiiForums Tanzania Kuwasha Mwenge kunaashiria "Illumination, enlightenment, and guidance." Mwenge wa Uhuru ni muhimu sana katika taifa letu

    Ishara kumi na mbili za dunia zimeunganishwa katika makundi manne (Moto, Ardhi, Hewa na Maji) Kwakuwa tunataka tuijue nchi yetu zaidi kwa leo sitaongelea kwa undani zaidi hizo ishara Kumi na Mbili na makundi yote hayo manne, bali leo nitaongelea pekee kuhusu Moto Kuwasha mwenge kunaweza...
  7. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Waziri Kikwete azindua zoezi la kupandisha Mwenge wa uhuru mlima Kilimanjaro kama ilivyoelekezwa na rais Samia

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Tanzania inapeleka mwenge wa uhuru juu ya mlima Kilimanjaro ili kuitangazia dunia kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni imara na pia itaendelea kulinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar...
  8. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania Video ya LIVE ya Rais Samia kwenye kilele cha mbio za Mwenge yaondolewa YouTube. Je, sababu ni kukohoa kwenye hotuba?

    Leo nilitaka kurudia kutazama tukio la jana la kilele cha Mbio za Mwenge na Kumbukumbu ya Miaka 25 ya kifo cha Hayati Mwalimu Nyerere, Oktoba 14 pale Mwanza, nimejiuliza maswali mengi kuhusu hili, kwanini video hiyo imeondolewa YouTube au kwasababu Rais Samia wakati akihutubia alikohoa mara...
  9. M

    JamiiForums Tanzania Kiongozi wa Mwenge kawa mkweli

    Muhtasari wa taarifa ya mbio za Mwenge 2024 imejaa ukweli mwingi. Wamejitahidi kubainisha kero na mahitaji ya wananchi kutoka mikoa mbalimbali. Sikusikia kero za wakazi.wa Dar ila kwa mujibu wa ripoti Wazanzibari wengi wameonyesha kuridhishwa na utendaji wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano na wa...
  10. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Rais Samia akishiriki kilele cha Mbio za Mwenge na Kumbukizi ya Miaka 25 ya kifo cha Hayati Mwalimu Nyerere

    Fuatilia yanayojiri kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 25 ya kifo cha Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kutoka uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, leo Oktoba 14, 2024. https://www.youtube.com/live/v8nSt4aSfdM?si=xHhzHPZ8Cjbg-3m9
  11. K

    JamiiForums Tanzania Maajabu kumbukumbu ya Hayati Mwalimu Nyerere kila mwaka Mwanza na sio Mara

    Nyerere anatumika kwa kiki za kisiasa na familia yake haifurahishwi na siasa kwenye swala la kitaifa. Sherehe za Nyerere zifanyike alikotokea Mara au kama kama ni kwa mzunguko basi zifanyike sehemu tofauti. Lakini hizi sherehe zimekuwa kama ni za Mwanza day! kufanya kampeni za siasa Mwanza...
  12. ngara23

    JamiiForums Tanzania Mwenge una Siri Gani? Viongozi Mwanza wanafanya miradi usiku kucha

    Mwenge wa uhuru tunavouchukulia inaweza ikawa tofauti na tunavyodhani. Nadhani viongozi wa mbio za Mwenge wanaenda ku report Kwa Rais mambo mazito, hawajali Mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi n.k. Wao wakikuta mambo ya ovyo wanakulipua juu. Mwenge kesho unaingia Ukerewe ila viongozi...
  13. Jumanne Mwita

    JamiiForums Tanzania Toka nakua na mpaka sasa sioni faida ya Mwenge wa Uhuru

    Kwa vyovyote vile nitakuwa wa mwisho na wakwanza kuajua faida za mwenge. Sioni faida wala umhimu wa huu mwenge kuwepo, mwenge umekuwa na karaha pale unapoenda sehemu yeyote. Kuna siku nimeitwa na mkuu wa Wilaya, wilaya flani akisema nitoe mchango wa mwenge nikamwambia mwenge unabajeti yake...
  14. Stephano Mgendanyi

    JamiiForums Tanzania Ngara: Mwenge wa Uhuru Wazindua Mradi wa Maji wa Tsh. Bilioni 3

    Mwenge wa Uhuru Wilayani Ngara umetembelea na kuzindua Mradi wa Maji Wenye Thamani ya shilingi Bilioni tatu chini ya Ufadhilii wa Benki ya Dunia kupitia LADP (Local Area Development Program) inayosimamiwa na NELSAP (Nile Equatorial Lake Subsidiary Action Program). Mhandisi Simon Ndyamukama...
  15. B

    JamiiForums Tanzania Mwenge wa Uhuru wamulika miradi ya maendeleo - Kibondo

    Jimbo la Muhambwe limepokea Mwenge wa Uhuru kutoka Halmashauri ya Kasulu Vijijini katika Uwanja wa Shule ya Msingi Busunzu 'B' ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa mbio za Mwenge wa Uhuru zinazoendelea nchini. Katika Jimbo la Muhambwe, Mwenge wa Uhuru umezindua Miradi ya Maji, Madarasa, Bweni na...
  16. I

    JamiiForums Tanzania MSAFARA WA MWENGE WA UHURU

    Swala la kufungwa kwa barabara na kusimama kwa shughuli za usafirishaji kwa masaa kadhaa wakati wa msafara wa Mwenge wa Uhuru limezua mjadala nchini Tanzania. Wakati Mwenge wa Uhuru una umuhimu wa kihistoria na kitamaduni, ukihusishwa na kampeni za kitaifa kama vile vita dhidi ya malaria, ujenzi...
  17. Stephano Mgendanyi

    JamiiForums Tanzania Mwenge wa Uhuru Wazindua Miradi Mingi Busokelo, Rungwe

    MBUNGE ATUPELE MWAKIBETE ASHIRIKI MBIO ZA MWENGE WA UHURU BUSOKELO, MIRADI MINGI YAZINDULIWA Mbunge Jimbo la Busokelo, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete ameungana na Viongozi mbalimbali kushiriki mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ambao tarehe 29/08/2024 umekimbizwa Halmashauri ya Busokelo, Wilaya ya...
  18. Stephano Mgendanyi

    JamiiForums Tanzania Mwenge wa Uhuru Musoma Vijijini Wazindua Miradi ya Bilioni 3.5

    MWENGE WA UHURU MUSOMA VIJIJINI: MIRADI YA THAMANI YA TSH 3.5 BILIONI YAKAGULIWA NA KUKUBALIKA Mwenge wa Uhuru ulipokelewa kwa shangwe nyingi mno kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) yenye Jimbo la Musoma Vijijini. Hiyo ilikuwa juzi, Jumatano, 31.7.2024 Miradi yote 7 ilikaguliwa...
  19. Lanlady

    JamiiForums Tanzania Mwenge wa uhuru utafutiwe nishati mbadala ya kuuwezesha kuwaka badala ya kutumia mafuta ya taa na utambi unaotoa moshi

    Bila shaka kichwa cha habari kinajieleza vizuri sana. Binafsi sina tatizo na falsafa ya uanzishwaji wa mbio za mwenge wa uhuru. Tatizo langu kubwa ni namna wanavyoweza kuathiri afya za wanaoukimbiza. Nishati inayotumika sio rafiki kwa afya za wanaoukimbiza na hata walio karibu nao mahali...
  20. figganigga

    JamiiForums Tanzania Kwanini Mkoa wa Mara wana Mwenge wao Tofauti na Mwenge wa Uhuru?

    Mkuu wa Mkoa wa Mara amewakaribisha viongozi, watendaji na wananchi wote kushiriki katika maadhimisho ya miaka 60 ya Mwenge wa Mwitongo yatakayofanyika nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwitongo tarehe 1 Agosti, 2024. Mwenge wa Mwitongo ni mwenge wa Kabila la Wazanaki...
Back
Top Bottom