Wakazi wa Kata ya Chamwino, Manispaa ya Morogoro, wameendelea kuishi katika mazingira yenye hatari kubwa za kiafya, kiusalama na kimazingira kufuatia kutofanyiwa usafi wa mara kwa mara maeneo yaliyopitiwa na miradi mikubwa ya serikali ikiwemo Bomba la Mafuta la TAZAMA na Grid ya Taifa ya Umeme...