Mwandishi na mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Hamis Mkotya, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo la Chemba.
Mkotya (Kushoto), amekabidhiwa fomu hiyo leo Jumatatu Juni 30, 2025 na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Chemba, Moza Abdallah.