Meya mstaafu wa jiji la Dar es Salaam, Boniface Jacob, amesema kuwa alipokea taarifa kwamba Jumanne, tarehe 10 Septemba 2024, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, kupitia Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO), liliwasiliana na mawakili wa CHADEMA na kuwaeleza kuwa wanamuhitaji Katibu Mkuu wa chama...