"Niwakati tulipokuwa mafunzoni Monduli Machi, 1976 hadi Januari, 1977 ndipo nilipomfahamu vizuri Yusufu Rajabu Makamba na tukawa marafiki tangu wakati huo mpaka sasa. Nikatokea kuutambua vizuri uwezo wake wa uongozi. Nilivibaini vipaji vyake adimu vya kuhamasisha, kuunganisha watu, kujieleza na...