Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho chama tawala nchini Tanzania na chama cha pili kwa muda mrefu zaidi barani Afrika, baada ya Chama cha True Whig cha Liberia. Kilianzishwa mwaka 1977, baada ya kuunganishwa kwa Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP) cha Zanzibar.
Wamekuja na huu mzigo sijui wameagiza contena ngapi uko china
Na baadhi ya wabongo walivyo wapuuzi wata piga kula kisa kapewa kiatu na sio kuchambua sela
Jumanne wiki hii ndani ya ofisi za chama cha mapinduzi(ccm) moshi mjini,kulitokea tukio ambalo siyo la kistaarabu pale kada wa chama hicho,Ibrahim Shayo a.k.a Ibraline alipomporomoshea matusi makali mstahiki meya wa manispaa ya moshi,Zuberi Kidumo.
Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya...
Huko Babati kuna mgombea wa nafasi ya mwenyekiti wa kijiji,ameambulia kura moja kijijini kwake.
Cha ajabu ana mke na watoto kadhaa hapo kijijini
Kaibiwa kura? Familia imemtosa?
Mimi na wewe hatujui
Soma Pia: Dar: Vurugu wakati wa kupiga kura maoni kata ya Yombo Vituka
Serikali inapaswa kuangazia kwa makini hali ya mji wa Moshi, uliopo mkoani Kilimanjaro, ambao umekuwa ukivunja rekodi nchini Tanzania. Kuitwa mji wa kwanza kuingiza malori yenye uzito wa tani 80 katikati ya mji ni jambo linalohitaji uchambuzi wa kina. Hali hii inatishia si tu usalama wa...
Botswana Democratic Party ni chama tawala cha Botswana na kimeongoza nchi toka uhuru 1966 na CCM ambayo ilikuwa Tano kimeongoza Tanzania toka 1961.
Tofauti kubwa ni kwamba chama cha Botswana kimeleta maendeleo makubwa kwa nchi na kulinda rasilimali.
Chama hiki kimekomesha rushwa . Kwa upande...
Mwanaume aliyenukuliwa katika kipande kifupi cha video kwa kauli yake tata kuhusu jinsia yake baada ya kudai kuwa yeye ni mwanamke, licha ya kuwa ni mwanaume kwenye kampeni za Chama cha Mapinduzi huko Makate, ametoa ufafanuzi.
Eston Chaula amedai kuwa hakuwa na lengo baya na kauli yake bali...
Inavoonekana CCM wana utaalamu wa hali ya juu sana katika kucheza rough za uchaguzi.
Na dalili za wazi tunaziona kwenye chaguzi za kura za maoni ndani ya chama, na kama haufikiri kwa kina unaweza kudhani zile ni rough ndani ya CCM, lakini ukweli ni kwamba lile ni tangazo la wazi kwa upinzani...
Mfano mzuri ni huu Uchaguzi wa Serikali za mitaa huwezi kukuta CCM au hata Chawa wake akina Lucas, Choicevariable na Mchungaji Msigwa wakivizungumzia Vyama vingine zaidi ya CHADEMA
Tumeambiwa na Daktari Slaa kuwa CHADEMA iko ICU lakini mbona CCM bado inahangaika nao usiku na Mchana
CCM...
Zoezi la kupiga kura kwa ajili nafasi ya Mwenyekiti na Wajumbe mtaa wa Mwananyamala-Kisiwani jana, Oktoba 23 lilishindikana kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo baadhi ya majina kutokuwepo kwenye orodha ya wakazi, hivyo kusababisha uchaguzi kuhamishiwa Ofisi za CCM Kata ya Mwinjuma.
Soma...
Vurugu zimezuka kura za maoni Uchaguzi wa kumpata mgombea atakaekwenda kupeperusha bendera Serikali za mitaa Chama cha Mapinduzi mtaa wa Mwanga mkoani Kigoma mara baada ya wananchi kutoridhika na mchakato wa uchaguzi huo.Wajumbe hao wamalalamikia wizi wa kura uliofanywa na baadhi ya viongozi...
Katika Kata ya Ibadakuli, Manispaa ya Shinyanga, kumetokea sintofahamu kubwa kati ya diwani wa kata hiyo, Msabila Malale, na diwani wa Vitimaalumu, Zuhura Waziri, wakati wa zoezi la kura za maoni za chama cha Mapinduzi (CCM).
Tukio hili lilitokea jana wakati wagombea wa CCM walipokuwa...
Kata ya Msigani inapatikana Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Kata hii inajumla ya Mitaa mitano ambayo ni Mtaa wa Msigani, Mtaa wa Temboni, Mtaa wa Malamba Mawili, Mtaa wa Msingwa na Mtaa wa Kwa Yusufu.
Aidha kwa mwaka huu kumekuwa na muhamko mkubwa sana kwa wanachama wa CCM katika Kata...
Leo kwenye kipindi chao cha minyama kitenge ametoa maoni yake ya kwamba hivi sasa watu wanapenda kugombea nafasi ndani ya CCM kuliko awamu iliyopita kwa sababu awamu iliyopita kuna maeneo watu walipita bila kupingwa.
Kwa takwimu za uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020 vijana wengi walichukua form na...
Duniani kote hakuna kitu kinachoogopwa na serikali dhalimu kama idadi kubwa ya wapiga kura.
Baada ya Tume inayosimamia uchaguzi TAMISEMI kudanganya idadi halisi ya waliojiandikisha, kazi iliyo mbele yao kwa sasa ni namna gani watabadilisha hiyo idadi ziwe kura.
Kwa mfano; Mwanza, Sensa ya 2022...
Hii nchi zinaimbwa miradi kuchwa nzima kuanzia Madaraja,mara Barabara mara reli na kadhalika.
Ila huko huko kwenye hizo Barabara, Madaraja, reli kuna umasikini wa kutisha kabisa, Kule Kigongo Busisi vuka ingia hapo Sengerema kuna Poverty ya kutisha kabisa, Sogea hapo Geita kwa Msukuma kuna...
Wakuu Kwema!
Leo nimekutana na moja ya mwanasiasa kutokea chama cha Mapinduzi ( CCM ) akijipigia kampeni kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Tunafahamu kwamba CCM wametangaza ratiba za wanachama wao kuanza kuchukua fomu kuzijaza na kurududisha na kuanza kampeni za ndani na ndipo...
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda ni mmoja kati ya washiriki katika zoezi la kupiga kura za maoni kuchagua wawakilishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Wanachama wa CCM nchi nzima wanaendelea kutumia haki yao ya kupiga...
Wakuu ni rasmi sasa mnara wa babeli wa CCM unaaanza kuanguka.
Huko Kigamboni kwenye mkutano wao wa ndani ya chama umevurugika na kumetokea vurugu wakati wapo kwenye mchakato wa kura za maoni.
Soma Pia: Vurugu zaibuka Uchaguzi wa CCM Kibosha Mkoani Pwani
Hii ni ishara kuwa hata ndani ya...
Hali ya sintofahamu imeibuka katika kitongoji cha kwa Kibosha, kata ya Mapinga wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, baada ya zoezi la kupiga kura za maoni, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kuahirishwa kutokana na baadhi ya wanachama kudai uwepo wa mapungufu katika uchaguzi huo na kusababisha vurugu...
Viongozi wa kimila (Machifu), jijini Mbeya, wameiomba Serikali kuweka program ya elimu ya fedha kuwa endelevu ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kupata uelewa na kutatua changamoto mbalimbali za masuala ya kifedha.
Wametoa wito huo walipotembelea Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.